Kwa mujibu wa taarifa ya Oakland Institute ni kwamba Wananchi wa eneo la hifadhi ya Ruaha walipeleka malalamiko WB Kisha kufunguliwa Kwa kesi Kwa manyanyaso waliyofanyiwa na maafisa wa TANAPA ikiwemo kuporwa mifugo Yao kwenye zoezi la kutaka kupanua eneo la hifadhi ya Ruaha ambapo zaidi ya wana Vijiji 21,000 wangepoteza Makazi Yao pamoja na Mali zingine.
World Bank cancels $150m tourism project in Tanzania after abuse claims
World Bank cancels $150m tourism project in Tanzania after abuse claims
Swali.
Yaani Kituo Cha Haki za Binadamu Tanzania na TLS hawaoni haya Ili wawasaidie Wananchi Hadi Wazungu ndio waje? Au hizo taasisi wenyewe kwao Wanasiasa wa Chadema ndio wanastahili Huduma zao pekee?
Mradi wa REGROW ulikuwa ni ufadhili wa Benki ya Dunia wa $150mln( Takribani Bilioni 350) uliolenga kukuza Utalii hifadhi za Kusini.
My Take
Kama taarifa hii ni kweli basi naishauri Serikali ,kama inataka kuongeza Ukubwa wa eneo la hifadhi ya Ruaha iwahamishe Wananchi Kwa Staha kama wanavyofanya huko Ngorongoro badala ya kuwafurusha.
Ngorongoro wanahamishwa kaya pamoja na mifugo Yao ,wanalipwa fidia na wanapewa maeneo,Kwa nini wasifanye hivi Ruaha?
Aidha Serikali iwachukulie hatua Askari wa TANAPA ambao walishiriki kuwatendea ndivyo sivyo Wanavijiji Hadi kutufikisha hapa Kwa kukosa weledi.
Pia soma
Benki ya Dunia Yatoa "Ultimatum" ya Siku 30 Kwa Tanzania Kumaliza Mgogoro wa Ukiukwaji wa Haki za Binadamu kwenye Mradi wa Regrow