Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu ndiyo maana ya mnada.Nyumba ya thamanii ya zaidi milioni 50, inauzwa 30.
Watampaa kidogo, maana najua gharama zote za mnada watakata kwenye hiyo pesa iliyobaki! Unaweza kuta akapewa Kama 2M hivi! Bank wezi sana!!Hivi hyo hela inayozidi wakipiga mnada wanakurudishia au... Assume deni ni 5.2m nyumba imeuzwa 30m hyo 24+m wanarudisha au?
Hii story ina walakini. Ni ya upande mmoja. Pengine ukimsikiliza mwanaume utakuta mkopo walichukuwa wote kwa kukubaliana kabisa lakini baadae wakafarakana. Nashangaa Tanzania mambo yameamuliwa na mahakama halafu mkuu wa wilaya anahusishwa. Tanzania ni sehemu ambayo watu ni wagumu mno kulipa mikopo na wakishakopa wanakuwa wajeuri sana.Nyumba ya thamanii ya zaidi milioni 50, inauzwa 30.
Mambo ya ndoa ni magumu na yanapohusisha mali yanakuwa magumu zaidi. Kutokana na uzoefu niliopata kwenye mahusiano na ndoa, katu sitakaa nilaumu mwanandoa yoyote kwa kusikiliza maelezo ya upande mmoja.Unaweza kuta mchongo wote ni wa Mume, maana hawako tena pamoja na huyo Mwanamke kampeleka Mume wake Mahakamani kwa ajili ya kudai malezi!ya Watoto, Sasa Jamaa kaamua Mambo kijasusi sana!!
Nyumba inauzwa milion 5 sio milion 30Hivi hyo hela inayozidi wakipiga mnada wanakurudishia au... Assume deni ni 5.2m nyumba imeuzwa 30m hyo 24+m wanarudisha au?
Dunia ishabadirika ndugu, mwanamke anaonekana ni mtu wa kusafiri...kama inavyoonekana mwanaume kamkomoa, siku hizi watu wanatafuta mwanamke wa wa muda ana.act kama mke wake wana sign document zote ( wakijua ni mke wake kumbe sio kweli) kinachofuata hela inatoka,Naona watu mnaanza kumlaumu mwanaume, ila kwa mtiririko huu wa story huyo mama alijua kila kitu na yeye ndo anataka kufanya utapeli.
Hakuna bank inayokopesha bila consent ya mke au mume wa mkopaji.
Na mtu unavyokopa ukaweka rehani nyumba hivi unakuwa unategemea usipolipa nini kitokee?
Amekiri kuwa alikuwa analifahamu hilo deni!!Mikono mikopo mikopo...inaumiza Sana..hata hivyo huyo mume hakufanya vizuri kutomshirikisha aliyekua mke wake..sasa wanapenda kuteseka ni watoto.
Mwanaume kakopa ki Siri Siri bila mke kuhusika katika Documents hizo na kisheria dada wa watu anayo haki nyumba ni Yao sio ya mme tuSijaona hoja kwa huyo mama muandishi wa habari.
Ni kweli kuna mkopo na anajua na figure anaijua. Hoja kwamba ametengana na mume hiyo unahusikaka vipi na Bank?
Na ni ngumu mwanandoa kuweka nyumba dhamana Bank bila mwenza ku sign.
Sina vimelea vya Usukuma ipa twende mbele, turudi nyuma benki waliyokopa ipo owned na Sukuma Gang?Mizizi ya Sukumagang bado inachipuka. Mwandishi wa habari wa Raia Mwema wamemkalia kooni kisa hapendi vitisho.
Yeye anafanya kazi zake kwa weledi bila woga. Mfumo unataka kumtoa roho. Wakati anakesi ya mahakamani ya 2020 aloandika kuhusu Tanzania kuwa na awagonjwa wa Corona, leo nyumba yake inataka kuuzwa na mahakama kufidia deni la mumewe alofariki.
Uhuru wa vyombo vya habri upo wapi?
Awali alikamatwa Mei 2020 na kukaa mahabusu ya polisi Central kwa siku 14 kwa amri ya utawala wa awamu ya tano kwa tuhuma za kuposti taarifa za wagonjwa wa Covid19 kukimbia Amana Hospital. Akapekuliwa nyumbani kwake kana kwamba ndo mwenye kutunza corona.
Hadi sasa simu za Maria Victor, bado ipo polisi kwa miaka miwili sasani.
Pia soma;
Dar: Kundi la WhatsAppp lamfikisha Mwanahabari Maria Victor Mahundi mahakamani
Alikamatwa Mei 2020 na kukaa mahabusu ya polisi Central kwa siku 14 kwa amri ya utawala wa awamu ya tano kwa tuhuma za kuposti taarifa za wagonjwa wa Covid19 kukimbia Amana Hospital. Pamoja naye Mhariri na Mkurugenzi wa Raia Mwema Mbaraka Islam naye alikamatwa na wote walipekuliwa nyumbani...www.jamiiforums.com
Benki yapiga mnada nyumba ya mwandishi wa habari wa Gazeti la RAIA MWEMA kisa deni la Tsh. Milioni 5.2
Nyumba hii ambayo ni mali ya Mary Victor Mahundi, mwandishi wa habari wa Gazeti la Raia Mwema la Dar es Salaam imepigwa mnada kwa Tsh. Milioni 30 ili kufidia deni la benki la Tsh. Milioni 5.2 ambalo alikuwa akidaiwa mume wa mwanahabari huyo. Inaelezwa kuwa nyumba hiyo iliyopo Tabata, Kata ya...www.jamiiforums.com