Benki yapiga mnada nyumba ya mwandishi wa habari wa Gazeti la RAIA MWEMA kisa deni la Tsh. Milioni 5.2

Benki yapiga mnada nyumba ya mwandishi wa habari wa Gazeti la RAIA MWEMA kisa deni la Tsh. Milioni 5.2

Unakopa bank gani? Unakopa ili ufanye nini? Umeshirikisha familia? Riba yao ni kiasi gan? Masharti/Vigezo vyao je? Jiulize haya kwanza
Tatizo hakumshirikisha mke wake, mbona mke wake angekopa kazini na kulipa deni la bank!
 
Kisheria bank haiwezi kuuza collateral ya marehemu kuna insurance ambayo huwa inafanya kazi pale mkopaji anapofariki au kupata ulemavu au magonjwa ya kudumu labda km alikopa kwenye micro credit
 
Hii kesi tusijaji upande mmoja,

Huenda Kuna kitu nyuma ya pazia huyu MKE anatuficha.

Hakuna mwanaume mjinga wa kiasi hicho kwa nyumba ya thamani iyo afu akakopee mkopo wa million 5.

I smell something fishy
 
Naona watu mnaanza kumlaumu mwanaume, ila kwa mtiririko huu wa story huyo mama alijua kila kitu na yeye ndo anataka kufanya utapeli.

Hakuna bank inayokopesha bila consent ya mke au mume wa mkopaji.

Na mtu unavyokopa ukaweka rehani nyumba hivi unakuwa unategemea usipolipa nini kitokee?
Huyu mwanamke aache kuficha ficha vitu
Kuna kitu kinaendelea ndan ya wanandoa hao
 
Unaweza kuta mchongo wote ni wa Mume, maana hawako tena pamoja na huyo Mwanamke kampeleka Mume wake Mahakamani kwa ajili ya kudai malezi!ya Watoto, Sasa Jamaa kaamua Mambo kijasusi sana!!
Yah! Jamaa kapiga kwenye mshono
Hii ndo dawa ya wanawake wanaojifanya bush lawyers
 
View attachment 2436797
Nyumba hii ambayo ni mali ya Mary Victor Mahundi, mwandishi wa habari wa Gazeti la Raia Mwema la Dar es Salaam imepigwa mnada kwa Tsh. Milioni 30 ili kufidia deni la benki la Tsh. Milioni 5.2 ambalo alikuwa akidaiwa mume wa mwanahabari huyo.

Inaelezwa kuwa nyumba hiyo iliyopo Tabata, Kata ya Kinyerezi, Mtaa wa Kichangani ilipigwa mnada siku chache zilizopita na tayari mwandishi huyo na familia yake wametakiwa kutoka ndani ya nyumba ndani ya siku 14, leo Desemba 5, 2022 ikiwa ni siku ya 9 kati ya siku alizopewa kuhama.

Mary amesema taarifa hiyo ni ya ukweli na kudai kuwa alikuwa akifahamu juu ya deni hilo la mumewe lakini hakuwa anajua kilichokuwa kikiendelea hadi kufikia hatua ya nyumba hiyo kupigwa mnada.

“Nilikuwa Dodoma katika shughuli zangu za uandishi wa habari, nikapokea simu kutoka Serikali ya Mtaa kunijulisha kuwa nyumba yangu inapigwa mnada.

“Niliporejea nikapata nakala ya barua ya taratibu za nyumba kupigwa mnada moja ikiwa imetumwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya na benki wamefuata taratibu nyingine zote inavyotakiwa, lakini hilo deni ni la mume wangu ambaye kwa sasa hatupo naye pamoja.

View attachment 2436799
“Nimewasiliana na Mkuu wa Wilaya kumueleza hali ninayopitia kwa kuwa hii nyumba si ya mume wangu peke yake ni mali ya familia, yeye (mume) kwa sasa hayupo nasi anaishi sehemu nyingine, inamaanisha kuwa tutatakiwa kuondoka ndani ya siku hizo 14, na kuwa watatuletea mabaunsa na kututoa kwa nguvu. Mkuu wa Wilaya ameniambia anashughulikia suala langu.

“Wakati huohuo, napambana kutafuta msaada wa kisheria ili kuweka zuio kabla ya hakimu na Majaji kwenda likizo ya kufunga mwaka, kwa kuwa sikushirikishwa katika huo mchakato wao wa mnada,” anasema Mary.

Nyaraka za benki zinaonesha kuwa deni lililosalia ni Tsh. 4,759,368 (Milioni 4.7), asilimia 10 ya deni ni Tsh. 475,936, hivyo jumla deni ni Tsh. 5,235,304.

Mary ameongeza kuwa: "Naomba kama kuna yeyote ambaye anaweza kunipa msaada wa kisheria anisaidie katika hilo kwa kuwa hapa nawazi nitaishi vipi na wanangu, kwanu hata huyo mume bado nina kesi naye kwa kuwa alibadili nyaraka na kuofanya nyumba ionekane ya kwake peke yake wakati hii nyumba ni ya familia, nina watoto, nitaenda wapi mimi na watoto wangu!
View attachment 2436800

View attachment 2436801
Kiasi kilichobaki kwenye mauzo nani alipewa.?
 
Mikono mikopo mikopo...inaumiza Sana..hata hivyo huyo mume hakufanya vizuri kutomshirikisha aliyekua mke wake..sasa wanapenda kuteseka ni watoto.
Kopa kwanza kwa malengo, halafu uone kama hiyo mikopo inaumiza. Labda kama unakopa Bayport au Platinum.
 
Dunia ishabadirika ndugu, mwanamke anaonekana ni mtu wa kusafiri...kama inavyoonekana mwanaume kamkomoa, siku hizi watu wanatafuta mwanamke wa wa muda ana.act kama mke wake wana sign document zote ( wakijua ni mke wake kumbe sio kweli) kinachofuata hela inatoka,

Ndio wananaza kufuatilia mgogoro huo wa kisheria..hapa kazi. Ipo
Hiii ilitokea sehemu kama ulivyosema
 
Wabongo mnapenda sana kupepeta midomo kuliko kusoma taarifa kamili.

Hiyo taarifa inaonesha huwa jamaa yake kawafanyia makusudi.
Kacheza mchezo kwa aliyekuwa mama watotot wake
Huyu mwanamke aliolewa na taahira jamaa anawatesa watoto wake akijua anamtesa mwanamke😆😆
 
Kisheria bank haiwezi kuuza collateral ya marehemu kuna insurance ambayo huwa inafanya kazi pale mkopaji anapofariki au kupata ulemavu au magonjwa ya kudumu labda km alikopa kwenye micro credit
Uko sahihi. Siku hizi Mikopo ya Bank ina insurance protection kwa kushirikiana na Makampuni ya Insurance. Kwa maaba kuwa premium inayokatwa kutoka kwa mkopaji, Bank ina transfer risk kwenye Insurance Company amboyo ina turn inalipa kama imetokea ulivyoeleza.
 
Tunapojadili
Tukumbuke pia huu mkopo mume kauchukua benki inayoitwa FINCA MICROFINANCE[emoji38]
 
Kacheza mchezo kwa aliyekuwa mama watotot wake
Huyu mwanamke aliolewa na taahira jamaa anawatesa watoto wake akijua anamtesa mwanamke[emoji38][emoji38]
Kama hujawai kukutana na mbilinge za wanawake wa ki-beijing huwez kuelewa alichofanya jamaa.

Tatizo Hii story tumeskiliza upande mmoja
 
Back
Top Bottom