Benki yapiga mnada nyumba ya mwandishi wa habari wa Gazeti la RAIA MWEMA kisa deni la Tsh. Milioni 5.2

Benki yapiga mnada nyumba ya mwandishi wa habari wa Gazeti la RAIA MWEMA kisa deni la Tsh. Milioni 5.2

Sijaona hoja kwa huyo mama muandishi wa habari. Ni kweli kuna mkopo na anajua na figure anaijua. Hoja kwamba ametengana na mume hiyo unahusikaka vipi na Bank?

Na ni ngumu mwanandoa kuweka nyumba dhamana Bank bila mwenza ku sign.
conjugal house huwa haiwekwi dhamana isipokuwa kwa idhini ya mke na mme kama hilo halikufanyika basi anaweza kushinda hiyo kesi
 
Huyo mwanamke aache uongo bank ukisitisha tu Marejesho lazima waanze usumbufu ikiwa ni pamoja na kuja kwenye kitu ulichoweka dhamana haiwezekani mda wote huo asijui hilo jambo anatoa tu visingozio
 
Huyo mwanamke aache uongo bank ukisitisha tu Marejesho lazima waanze usumbufu ikiwa ni pamoja na kuja kwenye kitu ulichoweka dhamana haiwezekani mda wote huo asijui hilo jambo anatoa tu visingozio
What if huyo mumewe alikuwa anarejesha bila mwanamke kujua then after certain period of time akasitisha na bank ndo wakaamua kuchukua hatua baada ya kuona kimya?
Tusimlaumu huyu mwanamke, tuangalie kwanza hali aliyonayo na watoto kabla ya kumpa lawama huku ikionekana kabisa aliyechukua mkopo ni mwanaume.
 
Naona watu mnaanza kumlaumu mwanaume, ila kwa mtiririko huu wa story huyo mama alijua kila kitu na yeye ndo anataka kufanya utapeli.

Hakuna bank inayokopesha bila consent ya mke au mume wa mkopaji.

Na mtu unavyokopa ukaweka rehani nyumba hivi unakuwa unategemea usipolipa nini kitokee?
Kaka yangu kakopa na mkewe hajui chechote mpaka kamaliza mkopo
 
Hata hivyo mabenki ya Tanzania kwa kushirikiana na madalali hupenda kukikmbilia kupiga minada nyumba za wakopaji kama kukomoana tu. Hutoa notisi fupi sana, yaani wiki mbili bila hata grace period.
 
What if huyo mumewe alikuwa anarejesha bila mwanamke kujua then after certain period of time akasitisha na bank ndo wakaamua kuchukua hatua baada ya kuona kimya?
Tusimlaumu huyu mwanamke, tuangalie kwanza hali aliyonayo na watoto kabla ya kumpa lawama huku ikionekana kabisa aliyechukua mkopo ni mwanaume.
Ok
 
Mwandishi wa habari wa Raia Mwema wamemkalia kooni kisa hapendi vitisho.

Yeye anafanya kazi zake kwa weledi bila woga. Mfumo unataka kumtoa roho. Wakati ana kesi ya mahakamani ya 2020 aloandika kuhusu Tanzania kuwa na wagonjwa wa Corona, leo nyumba yake inataka kuuzwa na mahakama kufidia deni la mumewe aliyefariki.

Uhuru wa vyombo vya habari upo wapi?

Awali alikamatwa Mei 2020 na kukaa mahabusu ya Polisi Central kwa siku 14 kwa amri ya utawala wa awamu ya tano kwa tuhuma za kuposti taarifa za wagonjwa wa Covid19 kukimbia Amana Hospital. Akapekuliwa nyumbani kwake kana kwamba ndio mwenye kutunza corona.

Hadi sasa simu za Maria Victor, bado ipo polisi kwa miaka miwili sasa.

Pia soma;


Haina uhusiano kabisa na deni la benki.
 
Nadhani hapo kuna kukomoana tu ....5m mbona linalipika kabisa ......pole sana familia
 
Baadhi ya wanawake wanaujinga fulani hasa wanapopata vimafanikio kidogo kiburi+jeuri ingenoga sana tungepata na stori ya upande wa pili,mala nyingi inaishia kutesa watoto tu
 
View attachment 2436797
Nyumba hii ambayo ni mali ya Mary Victor Mahundi, mwandishi wa habari wa Gazeti la Raia Mwema la Dar es Salaam imepigwa mnada kwa Tsh. Milioni 30 ili kufidia deni la benki la Tsh. Milioni 5.2 ambalo alikuwa akidaiwa mume wa mwanahabari huyo.

Inaelezwa kuwa nyumba hiyo iliyopo Tabata, Kata ya Kinyerezi, Mtaa wa Kichangani ilipigwa mnada siku chache zilizopita na tayari mwandishi huyo na familia yake wametakiwa kutoka ndani ya nyumba ndani ya siku 14, leo Desemba 5, 2022 ikiwa ni siku ya 9 kati ya siku alizopewa kuhama.

Mary amesema taarifa hiyo ni ya ukweli na kudai kuwa alikuwa akifahamu juu ya deni hilo la mumewe lakini hakuwa anajua kilichokuwa kikiendelea hadi kufikia hatua ya nyumba hiyo kupigwa mnada.

“Nilikuwa Dodoma katika shughuli zangu za uandishi wa habari, nikapokea simu kutoka Serikali ya Mtaa kunijulisha kuwa nyumba yangu inapigwa mnada.

“Niliporejea nikapata nakala ya barua ya taratibu za nyumba kupigwa mnada moja ikiwa imetumwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya na benki wamefuata taratibu nyingine zote inavyotakiwa, lakini hilo deni ni la mume wangu ambaye kwa sasa hatupo naye pamoja.

View attachment 2436799
“Nimewasiliana na Mkuu wa Wilaya kumueleza hali ninayopitia kwa kuwa hii nyumba si ya mume wangu peke yake ni mali ya familia, yeye (mume) kwa sasa hayupo nasi anaishi sehemu nyingine, inamaanisha kuwa tutatakiwa kuondoka ndani ya siku hizo 14, na kuwa watatuletea mabaunsa na kututoa kwa nguvu. Mkuu wa Wilaya ameniambia anashughulikia suala langu.

“Wakati huohuo, napambana kutafuta msaada wa kisheria ili kuweka zuio kabla ya hakimu na Majaji kwenda likizo ya kufunga mwaka, kwa kuwa sikushirikishwa katika huo mchakato wao wa mnada,” anasema Mary.

Nyaraka za benki zinaonesha kuwa deni lililosalia ni Tsh. 4,759,368 (Milioni 4.7), asilimia 10 ya deni ni Tsh. 475,936, hivyo jumla deni ni Tsh. 5,235,304.

Mary ameongeza kuwa: "Naomba kama kuna yeyote ambaye anaweza kunipa msaada wa kisheria anisaidie katika hilo kwa kuwa hapa nawazi nitaishi vipi na wanangu, kwanu hata huyo mume bado nina kesi naye kwa kuwa alibadili nyaraka na kuofanya nyumba ionekane ya kwake peke yake wakati hii nyumba ni ya familia, nina watoto, nitaenda wapi mimi na watoto wangu!
View attachment 2436800

View attachment 2436801

5.2m, umesahau riba
 
Nimeona hili tangazo kwa kuchelewa ila inauma sana Kuuziwa Nyumba kwa sababu ya deni la shs Milioni Tano?
Natamani angepata wasamaria wa kumchnagia hata nusu ili akope tena nusu akomboe Nyumba
 
Back
Top Bottom