Benki za kwenye simu ni zaidi ya Benki Kuu!

[emoji123][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Huyo kijana ovyoo sanaa🤣🤣🤣kama anadhani wakala ndo anamkopesha bhasi wakala ampe hela bila kutoaaa
 
We jamaa mbona kichwa ngumu sana ukikopa shongesha pesa inatoka kwao inaingia kwenye namba yako uwe tigopesa mpesa airtelmoney au halopesa wewe uliyokopa ndio unaenda kutoa kwa wakala pesa ambayo ipo tayari kwenye simu yako ni logic simple tu mimi siwezi kukutumia hela wewe ambayo sina kwenye akaunti yangu ndio mana hata wakati wa kulipa deni lako humlipi wakala unalipa kwenye lipa namba ya shongesha na huwezi kulipa kama huna hela kwenye akaunti yako na wao hawawezi kukukopesha kama hawana hela kwenye akaunti yao
 
Swali analouliza OP ni la msingi sana kiuchumi. Na limeumiza vichwa vya wasomi hadi wengine wametoa conspiracies.
Nyie mnaoshangaa swali lake mnanishangaza kama kweli mnaujua uchumi wakati ni mjadala common na unaoumiza kichwa kwenye sekta hiyo, mimi sio mchumi hivyo siwezi jipambanua kumjibu ila simshangai kabisa kwanini anataka maelezo ya kina.

Hii mikopo ya simu iko backed na banks mmetaja kama NMB.
NMB ina capital iliyotumika kuianzisha, capital ilizaa faida na dividend policy yake kwa miaka kadhaa ikawa ni kuongeza mtaji. Na baadae shares zake zikapanda kutokana na kufanya vizuri (speculation ilitumika, sio pesa halisi iliwekwa) na NMB pia ikanunua assets na ikawa na wateja wengi.

Tukiweka hela NMB tunakuwa "tunaikopesha" benki, tunaipa itushikie. Yenyewe inaamua ikushikie ilale na hela au izitumie ukizitaka ikupatie, mabenki huwa hayalalii hela.
Pale sasa NMB inaenda kukopesha hela zetu kwa wanaotaka (ambao ni wachache na wana vigezo, wakati kuweka hata mwendawazimu anaweza).

Inapokopesha mtu, inabaki na matumaini ya kurudishiwa hela pamoja na riba, hayo matumaini yapo kwenye loan contract na tena kuna bima ya mkopo na aliyepewa bado ana dhamana. NMB inakuwa na security deposit BOT kwa ajili ya bad debts ambazo kama sisahau zinachezea kwenye 6% hivi ya mikopo. Hiyo security deposit ndio lazima iwe cash imewekwa na benki, hela ndogo sana ukilinganisha na transactions zao.

NMB ikihitaji kukopesha zaidi inauza assets zake ipate cash, inauza shares zake au inachukua mkopo na yenyewe kwa gharama ndogo. Kwenye kuchukua mkopo inaenda na loan contracts ilizonazo mfano kwa Wells Fargo Bank ya Marekani.

Kwa mzunguko huu kumbe kuna sehemu nyingi benki inatumia hela isiyo yake bali ya wateja au kufanyia biashara 'matarajio ya wateja'
🛑 Kama si hivyo, kwanini benki huwa inatoa riba kwa mtu anayeweka fixed account?
Kumbe sasa hata hii hela ambayo haiko fixed account huwa wanaitumia, lakini wanaikata operation cost na wanapata faida bure kwa kuitumia.

🛑 Kwanini huwa kuna bank run? Situation inayotokea pale watu wote waamue kuchukua hela zao walizoweka benki, benki hufeli. Kama benki inakopesha hela zake yenyewe na si za watu, kwanini walioweka hela wakizitaka kwa pamoja benki inakufa?

🛑 Kwa mfumo wa fractional reserve banking, benki inaweza kopesha hata zaidi ya mara 10 ya hela iliyonayo cash (kiasi kizidi security deposit yake Central Bank). Sasa hii mara 10 ya hela inatoka wapi na tukikomaa kusema benki inakopesha hela zake tu.
 
Tufanye hiyo elfu kumi umetokomea nayo hujalipa, waliokukopeshaje wataipata vp hy pesa ambayo ww umeipata physical.?
Naam ndio maana kuna insuarance na kuna wakati benki zinakufa...., ila walishafanya hesabu ya wangapi huwa wanatokomea, na sababu Bongo Afrika wengi wanatokomea ndio maana Riba ni kubwa (Ku offset risks) kwahio wale wanaotokomea wanalipiwa na faida za wale wanaolipa na bado mara nyingi Benki inabaki na faida...

Kama Benki zikifeli basi Kodi zetu kama wananchi ndio tutatoa ili kunusuru hizo Benki (They are too Big to fail) kama yaliyofanyika USA wakati wa credit crisis....

Hio ndio Capitalism 2.0 (Ni Socialism in disguise) wakipata faida ni wao wakipata hasara ni wananchi

 
Nini kiwazuie wakopesha mitandaoni kukukopesha pesa ambazo hawana? Maana wanakuandikia mkopo lakini keshi unaenda kuchukua kwa wakala. Wao hawatoi hata mia.
We nae, hiyo msg unayotumiwa ya songesha inapunguza akiba Yao , mfano Voda Wana akiba ya shilling elf 10 waliopata Finca microfinance kwaajili ya songesha, uki songesha 1000 wanakutumia msg lkn wao wanabaki na 9000 jaribu kuelewa
 
Sasa jiulize kwa nn zinakufa then linganisha na alichokiandika mtoa mada ndio utajua unapokopa bank, songesha, mgodi n.k wao wanatoa pesa physical Ila Kwako inakuja kama soft-money mana kilichowaunganisha mpaka ukapata mkopo n simu/akaunti na sio kwamba umepewa mkopo mkononi.
 
M nakopamkpaka laki 5 mkuu tigo
 
Sasa jiulize kwa nn zinakufa then linganisha na alichokiandika mtoa mada
Moja kwanza mimi nimeongea zaidi ya mada ya mto Mada, sababu mtoa mada kuna vitu vingi (premises ambazo ameweka amekosea) anadhani hio biashara ni Mitandao per se kumbe mitandao inatoa platform na kisheria hairuhusiwi kufanya kila kitu lazima kuwe na Bank inayosimamia hayo mambo

Kwamba kwanini zinakufa.., moja ni sababu zimekwenda beyond kile kiasi ambacho wanakopa ili wakopeshe, hence kutokukopesheka tena...., Pia kama wananchi wakiacha / wakipunguza imani na Banking system hivyo kila mtu kutaka pesa yake the whole banking system will go under (na ndio hapo wananchi / kodi zako kupitia serikali zitatumika kuhakikisha Benki hizi zinapewa pesa ili ziendelee kukopeshana)
ndio utajua unapokopa bank, songesha, mgodi n.k wao wanatoa pesa physical Ila Kwako inakuja kama soft-money mana kilichowaunganisha mpaka ukapata mkopo n simu/akaunti na sio kwamba umepewa mkopo mkononi.
Benki wana pesa zao (ingawa wanaruhusiwa kukopesha zaidi ya pesa walizonazo (call it overdraft) mitandao pia inalazimishwa kisheria pesa zao / za wateja wachague benki ya kufanya nao kazi ili wao ndio waweze kuzitunza / kuzimanage....

Kwahio tukiongelea mikopo yote Songesha na hata mikopo ambayo sio kama hio Banks hizi zinaweza kutoa zaidi ya kilichopo kwenye kapu lao kwahio hata kama wana uwezo wa kukopa laki moja (kilichopo) wanaweza wakakopesha hata milioni moja.... na sababu this is digitally na unaweza ukakuta akaunti zote digitally zipo kwenye benki moja kinachobadilika ni figures from one account kupewa positivie na nyingine minus the same amount.... (After all in this day and age we do not even need hard cash).., Those digits ndio cash yenyewe.... (hata gerezani wanaweza wakakubaliana kwamba sigara moja ni worth so much hivyo kutumika kama currency)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…