Benz inayopumua: Jiunge nami tujifunze mengi

Jina la hilo gari unalotumia aisee nimestuka sana maana ni moja ya mashine nazozikubali mno Mercedes Benz Germany wana kiwanja cha mpira cha Timu moja wanatumia hilo jina...
 
@mods please ikiwapendeza naomba nisaidie kufuta huu uzi.
Sikutegemea utageuka wa ngono.

Napenda pets.SANA,
Nina mbwa pia.Wana akili kuliko baadhi yetu mandingo.

Niliamini Kuna wapenzi wenzangu wa paka hapa tufurahie na kufundishana kuhusu wanyama ila baada ya kupost ndio nimekumbuka niko Afrika ambako wanyama hawana thamani.

Naona bandiko limegeuka la mambo ya ngono na hilo sio lengo na sijisikii amani kuendelea na huu uzi.

Niwaage tu kwa KUOMBA tuache kunyanyasa wanyama.Na wao wanaumia kama wewe tu.
Kuna watu wameokolewa kifo na pets wao.

Juzi tu kuna mbwa kaokoa kichanga kilichofukiwa na mamake kife ila mbwa huyo huyo akikatiza mitaa ya Tz Kuna wajinga watampiga mawe.

Waafrika sisi ni wakatili na tunachowafanyia wanyama ndicho tunachofanyiana gizani.

My dream ni siku moja nifungue kituo cha kulelea paka waliotelekezwa.
Pia nitafurahi siku moja sheria za kutetea wanyama zikifanyiwa kazi.
Wajinga wote wanaoopiga piga paka ovyo wanatakiwa kukaa gerezani,sio watu wazuri.

Nakasirishwa sana na mawatu yanayohusisha paka na ushirikina,Naona kichwani wamejaa funza.Waafrika tuko nyuma sana ya Muda..
Tunawaza ngono tu na kuzaa zaa hovyo vitoto vingi vingi tusivyoweza kuvihudumia na kuvisomesha na vyenyewe vnaishia kurithi imani za kishirikina.
So sad!
 
Paka ni viumbe wazuri na waajabu sana, kwa mwenye kuwaelewa.

Wengi wanasema mbwa ni rafiki mkubwa wa binadam, mimi binafsi nasema paka ni rafiki mkubwa wa binadam.

Paka ana sifa nyingi nzuri za kulelewa na binadam kuliko mbwa. Mimi nimekuwa na paka tangu utotoni na siwezi kuishi bila paka nyumbani kwangu, ndani na nje ya Tanzania.

Machache kuhusu paka wangu wa shamba Tanzania.

Anajuwa kama kunakuja wageni, ana ishara zake na namna ya sauti anazotoa, mimi naelewa kuna kuja wageni.

Anakamata na kuua wadudu wabaya, kama nyoka, tandu, nge na kuwapanga mlangoni kwa nje ya nyumba, ili kunionesha kazi anayoifanya nimsifie. Anawaua tu hawali kabisa. Namsifia na kumpa dagaa nyama, basi hapo atatoa sauti fulani ambayo mimi nimeitafisiri anamshukuru Mungu na mimi kwa zawadi. Hiyo sauti huwa haitowi mpaka utapompa chakula.

Tumwacheni paka Mercedes ajielezee zaidi.

Karibu sana Merecedes Benz. aka Benzie
 
Nakuelewa sana dada yangu bravo🙏
 
Mapenzi yake kwa paka yalizidi.
Kuna aliyefanya surgery awe paka.
Mimi napenda sana paka,ni sehemu ya familia, ni wanyama wazuri

Nope, she was traumatized akaona bora aishi kama nyau...
 

Umeshawahi kufika Mburahati?
 
Paka ni mnyama mzuri sana na mwenye kuvutia, ana akili nyingi, akiwa kwenye familia anajua na yeye ni mmoja wa familia so ana behave as one, kuna mdau huko juu kasema ukimpa paka samaki na wewe ukawa unakula samaki anaacha wake analilia wako hahaha kwani hiyo tabia si hata watoto wadogo wanayo?
Kinachonifurahisha kuhusu paka ni ubinafsi na uchokozi wao, yeye anaweza akakaa sehemu yoyote kwenye kochi ila ole wako wewe ukae sehemu yake atalia hadi utoke, atapanda kwenye dressing table yako na kuangusha kila kitu halafu atakuangalia like utanifanya nini i'm the boss here.

Benzie ni paka mrembo😍
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…