TANZIA Bernard Kamilius Membe afariki dunia
Bush lawyer, pesa za marehemu ni mirathi ya familia, vitu vikipigwa mnada pesa inakwenda kwenye account ya mahakama, baada ya mirathi Msimamizi wa mirathi anajaza fomu ya kugawanya pesa za marehemu zilizopo kwenye bank zote kwa wanufaika wa mirathi.

Endeleeni kudanganyana, Membe amejenga msingi mzuri wa kuwatia adabu waropokaji wote.
Naona ni propaganda tu, siku 5 za kupiga mnada zilipita muda mrefu tu. Gazeti la raia mwema likaandika yono wamepigwa marufuku kufanya mnada. Nikaona ni sarakasi tu

Kuna kitu ambacho pengine hatujui kwa hawa watu, sisi kazi yetu kushangilia tu
 
f3929c7f-e3d6-4597-8e59-0bf4f5370ae8.jpg

Mtumeeeeeee
Muuuungu ehhhh untashaaa!
Jamani uwiiiiiiiiiii
 
Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Taarifa za awali zinaeleza Membe alipata changamoto ya Kifua na kupelekwa Hospitali ya Kairuki alfajiri ya leo May 12, 2023 na baadaye kufariki.

Benard Membe alipata kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli.

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.

R.I.P B.C Membe
 
Muda mwingine hata Ukimsamehe Adui yako Mkubwa kwa mabaya yote aliyokufanyia huwa ni Kinga tosha ya Ulinzi wako kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuna mahala Mwenyezi Mungu atakubariki pakubwa kwa huko Kusamehe Kwako.

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa.
 
Back
Top Bottom