TANZIA Bernard Kamilius Membe afariki dunia
Ila kusema ukweli, membe alikuwa anaumwa kitambo sema mambo ya pesa tu. Nakumbuka 2018 au 2019 nilikutana nae nmb pale lindi akiwa na gari yake flani ya kibabe hivii; alionekana dhaifu sana.

Nilikutana nae tena Dar, 2022 mwanzoni, alikuwa amedhoofu zaidi......kuna kitu kilikuwa kinamsumbua yule, trust me!!
 
Wewe tulia,muhusika kaondoka. Familia wala haitaendelea na hili. Wao wanaachana nalo hili.Ninajua kuna kurithi wadai na wadaiwa.Ila kwa hili la kesi ya Musiba,Familia inaliacha linaondoka na aliyepeleka kesi.
Kwa hiyo YONO haitatekeleza hukumu?
 
Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Taarifa za awali zinaeleza Membe alipata changamoto ya Kifua na kupelekwa Hospitali ya Kairuki alfajiri ya leo May 12, 2023 na baadaye kufariki.

Benard Membe alipata kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli.

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.

UMEME WA MOYO RIP MZEE, WEMA HAWAFI
 
Back
Top Bottom