TANZIA Bernard Kamilius Membe afariki dunia
Usikute ni maandalizi ya 2025?
Membe amezaliwa mwaka 1953 na amefariki mwaka 2023, ni miaka 70 net.

Huyo tayari amekula chumvi na anaweza kufa kwa pressure tu katika umri huo, na ni bora ufe kuliko pressure ikuletee major stroke ni mateso matupu kwako na familia yako, unaanza kuhudumiwa kama mtoto Mchanga kubadilishwa pampas na kulishwa.

Kwa tuliopoteza wapendwa wetu kwa maumivu makali, Membe amekufa kifo chema bila mateso wala familia kuteseka.

Ni unafki tu unatusumbuwa lakini wengi tunatamani mwisho mwema kama wa Membe, ni wachache wanaopata bahati hiyo.

Mabere Marando yupo hai lakini ni sawa na mfuko tu, sasa yote ya nini hayo?
 
View attachment 2618772

Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya Nje kwenye Serikali ya awamu ya nne, Benard Membe amefariki Dunia. Taarifa za awali zinaeleza Membe alipata changamoto ya Kifua na kupelekwa Hospitali ya Kairuki alfajiri ya leo May 12, 2023 na baadaye kufariki.

Benard Membe alipata kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Mtama na alihitimisha safari hiyo mwaka 2015 na kujaribu kuwania tiketi ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM), tiketi ambayo alipewa hayati John Magufuli.

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.
Haya haya haya tafakuri Kali mmeachiwa. Wema hawafi ila wabaya wanakufa who is who?
 
Kufa siyo kiboko bali kufa ni faradhi!!

Ni mtu mjinga tu anayewaza kwamba kufa ni udhaifu!!
Kaka Allen Kilewella! Umeniumiza moyo kwa tahadhari uliyotoa! Lakini huwenda na wewe umesahau kwamba, wewe ni miongoni mwa walio/wameendelea kukashifu sana kuhusu Magufuli kwa kufa kwake

Nimefurahi kusikia kwa kinywa chako leo kwamba, haifai tuishi kwa namna hiyo, anza kujisikia vibaya kukashifu wasioongea tangu saa hii

Mungu aturehemu
 
View attachment 2618772

Mwaka 2018 aliandikwa na gazeti la Tanzanite akituhumiwa kuweka ajenda ya kutaka Rais Magufuli asipewe nafasi ya kuwania Urais 2020, ambapo alifungua kesi ya madai ya kuchafuliwa na kushinda kesi hiyo, alikazia hukumu iliyomtaka mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba alipe Tsh. bilioni 9 ndani ya siku 14.
Is just a coincidence or it related to the case mentioned above☝️☝️☝️☝️?

Kuugua ghafla asubuhi ya leo na kufa hapohapo?

Jamani ni maswali tu. I am just curious.

Wasiojua kufunga midomo na kutunza siri zao walitanguliaga kupima upepo mapema👇👇👇👇

 
Tumefika hapa kwasababu wapo wajuaji waliogoma kusahau yaliyopita, wayaache yaende, wakajiona wamekaa juu wamefika, wao kila siku ikawa ni kumuimba marehemu mtangulizi, wakajisahau wakidhani kifo kina undugu au urafiki, leo kifo kimewakumbusha hakina mwenyewe.

Sio wakati wa kulaumiana tena, maisha ni fumbo, tujifunze kuyaacha yaliyopita yapite, lakini sio kujisahau na kujipachika majina ya ajabu kama wazuri hawafi au Mungu fundi, leo majina hayo hayo yanarudishwa upande wa pili, ni vyema wahusika wayapokee kama walivyoanza kuwapa wenzao, time to feel a test of your own medicine.
Duuuuuuh. Kwa mala ya kwanza Leo nimekupongeza. Lakini Hadi Leo wapi watu wanashangilia hata kama adui yako kafa Huwa tunaacha yote yaliyopitaaa, sio kutoa FURAHA na kumhusisha mungu eti ni fundii. Tujifunze kuwa wapole, mbele ya haki Kila mtu ataenda Kwa wakati wake.
 
Kama Taifa tunatakiwa tutoke kwenye siasa hizi za chuki zilizozalishwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015. Baada ya Uchaguzi ule na John Pombe Magufuli kuingia madarakani, kulitokea uhasama mkubwa sana kati ya watu waliokuwa wanamuunga mkono na wale waliokuwa wanapingana na staili yake ya utawala.

Leo Baada ya kutangazwa kwa Kifo cha Bernard Camilius Membe, unaona kabisa limeibuka kundi la watu humu JF ni kama wanahanikiza furaha yao kwa kifo cha Membe. Watu hao ambao wanajificha nyuma ya kuonesha furaha kwamba Cyprian Musiba hatalipa tena hela alizotakiwa kumlipa Membe, lakini kwa undani unaona kinachowafurahisha zaidi ni kuona mmojawapo wa wapinzani wa Magufuli naye Kafariki.

Wakumbuke kwamba ni wao waliokuwa wanasema wakati wa msiba wa Magufuli kwamba "hakuna atakayeishi milele" na Leo ni ushahidi mwingine kwamba hakuna atakayeishi milele.

Watu wafanye maridhiano dhidi ya nafsi zao!!
Wazuri hawafi....Makamba sr. Naye tunamsubiri
 
Back
Top Bottom