Tumefika hapa kwasababu wapo wajuaji waliogoma kusahau yaliyopita, wayaache yaende, wakajiona wamekaa juu wamefika, wao kila siku ikawa ni kumuimba marehemu mtangulizi, wakajisahau wakidhani kifo kina undugu au urafiki, leo kifo kimewakumbusha hakina mwenyewe.
Sio wakati wa kulaumiana tena, maisha ni fumbo, tujifunze kuyaacha yaliyopita yapite, lakini sio kujisahau na kujipachika majina ya ajabu kama wazuri hawafi au Mungu fundi, leo majina hayo hayo yanarudishwa upande wa pili, ni vyema wahusika wayapokee kama walivyoanza kuwapa wenzao, time to feel a test of your own medicine.