TANZIA Bernard Kamilius Membe afariki dunia
Tumefika hapa kwasababu wapo wajuaji waliogoma kusahau yaliyopita, wayaache yaende, wakajiona wamekaa juu wamefika, wao kila siku ikawa ni kumuimba marehemu mtangulizi, wakajisahau wakidhani kifo kina undugu au urafiki, leo kifo kimewakumbusha hakina mwenyewe.

Sio wakati wa kulaumiana tena, maisha ni fumbo, tujifunze kuyaacha yaliyopita yapite, lakini sio kujisahau na kujipachika majina ya ajabu kama wazuri hawafi au Mungu fundi, leo majina hayo hayo yanarudishwa upande wa pili, ni vyema wahusika wayapokee kama walivyoanza kuwapa wenzao, time to feel a test of your own medicine.
Kwa mara ya kwanza nakupa Like yangu.

Watulie na wayapokee. Mwingine anadondoka kesho mchana
 
Wewe tulia, muhusika kaondoka. Familia wala haitaendelea na hili. Wao wanaachana nalo hili.Ninajua kuna kurithi wadai na wadaiwa.Ila kwa hili la kesi ya Musiba,Familia inaliacha linaondoka na aliyepeleka kesi.
Watu waliumia mno wakati msiba wa mpendwa wao JPM upo Chato, sasa wao wanalia, na je, WanaJPM wacheke kama walivyofanya wao?
 
Ila kusema ukweli, membe alikuwa anaumwa kitambo sema mambo ya pesa tu. Nakumbuka 2018 au 2019 nilikutana nae nmb pale lindi akiwa na gari yake flani ya kibabe hivii; alionekana dhaifu sana.

Nilikutana nae tena Dar, 2022 mwanzoni, alikuwa amedhoofu zaidi......kuna kitu kilikuwa kinamsumbua yule, trust me!!
Magonjwa yetu haya haya ya kisasa mkuu?
 
Back
Top Bottom