Uchaguzi 2020 Bernard Kamilius Membe: Nitagombea Urais wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo

Hebu orodhesha hao wenye AKILI wenzako angalau 854 tu
 
Labda ungejifunza kwanza kuandika kabla ya kuanza kufikiria mambo mengine, ni muhimu zaidi, ...
Hahaha aisee kweli nimechanganya neno kura nimeandika kula. Najua kuandika vizuri sana, hiyo ni speed tu ya kuandika inapelekea small mistakes kama hizo. Na hua sirudii kusoma nachoandika it's a waste of time
 
Kama kweli Membe anania ya kuiangusha ccm asiwe mbinafsi amuunge Tundu lissu uraisi 2020.

Ni aibu kwa Membe kugawanya kura za upinzani.

Hakuna mtu ambae alimpigia kura lowasa anaeza fanya mistake nyengine tena na chadema wakimuunga Membe km mgombea ndio mwisho wao.
 
Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu apigwa risasi
Imechapishwa: 07/09/2017 - 15:46

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu
Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu youtube
Ujumbe kutoka:
RFI
1 Dakika
Mwanasiasa wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa serikali ya Tanzania Tundu Lissu, amepigwa risasi akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma, polisi wamethibitisha.

MATANGAZO YA KIBIASHARA
Chama chake cha CHADEMA kimethibitisha tukio hili lililofanyika Alhamisi mchana wakati mwanasiasa huyo akiwa ndani ya gari lake akitokea bungeni kuhudhuria vikao vya bunge vinavyoendelea.

Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amesema, Lissu anaendelea kupata matibabu ya dharura lakini hali yake sio nzuri.

“Tupo hapa Hospitalini, hali yake sio nzuri,” Mbowe aliambia kituo cha Televisheni cha ITV nchini humo.

Madaktari wanaomhudumia wanasema mwanasiasa huyo ambaye pia ni rais wa Chama cha Mawakili cha Tanganyika, amepigwa risasi, tumboni, mgongoni na mguuni.

Haijabainika ni akina nani waliompiga risasi mwanasiasa huyo.

Viongozi wa serikali mkoani Dodoma wanasema wanachunguza tukio hilo.
 
Duu
 
Tuambieni amewafanyia nini watanzania na sio mambo ya huko ng'ambo. Hatuchagui mtu wa kutumikia mataifa ya nje.

Ila Membe hana kabisa mvuto wa kisiasa. Hata hachangamshi.
 
Wapinzani ni lazima Tuungane
 
Usipomwelewa Membe unapata tabu... jamaa anakauli fulani ivi tata... 'Sisi' ... "wenzangu", " kisiki"...... n.k

Kisiki cha mpingo sio yeye tu, fuatilia mahojiano yake na Ulimwemgu, aliweka wazi, Wanaume anaowakubali ....Visiki vya mpingo.


Membe anajua hashindi akisimam, ila anachotaka ni kuwasaidia wapinzani na serikali ione uwezo wake.
 
Membe hana msaada wowote ule,Membe ni Lowassa part 2.FULL STOP

Atagawa kura za upinzani,atashindwa kwny uchaguzi kama kawa na akimaliza kazi yake atarudi zake kwao Ccm kama kawa.
 
Upinzani bana ....miaka yote akili zinawakaa vizuri kweli ....lakini kipindi cha uchaguzi ni kama wanapigwa ganzi! Watafanya yale yale alafu watakuja na ulalamishi ule ule!
 
Na kuondoa hiyo hofu yako, kama umemfatilia , amewahi kukiri yupo tayar kumuunga mgombea yoyote watakayekubaliana.

Anaweza kusimama, akasimama Lissu, lkn mwisho akaamua kumuunga Lissu... nani anajua???? .


Hapa nilazima wapinzani wakae vzuri wajadiliane.


Kama wasipoungana, CCM haitatikiswa hata kidogo.


Membe hana msaada wowote ule,Membe ni Lowassa part 2.FULL STOP

Atagawa kura za upinzani,atashindwa kwny uchaguzi kama kawa na akimaliza kazi yake atarudi zake kwao Ccm kama kawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…