Bernard Membe aitwa kwenye Kikao cha Kamati ndogo ya Udhibiti wa Nidhamu CCM

Bernard Membe aitwa kwenye Kikao cha Kamati ndogo ya Udhibiti wa Nidhamu CCM

Kwa nini viongozi wengi na wanachama wa CCM wanamuunga mkono sana Membe hata kama hawasemi hadharani?

Jana kuna mtu CCM kindakindaki na ni tegemeo katika uenezi na utetezi wa Sera (yaani sio hawa mavuvuzela) katika maongezi ya kawaida alisema, mfano umshikishe msahamu Samia au Majaliwa na sio hadharani kisha muulize sema ukweli wako Membe au jiwe nani unamuunga mkono Watakujibu Membe.

Huo ndio ukweli, hivyo kuna haki mbaya sana kuliko wakati wowote ndani ya CCM.
 
Umehama toka kwa Lissu? Kachero usiyejua hata njia ya kupita kupata Urais!
KUna watu hawafundishiki, huyu ni mmoja wao.
 
Chakaza,
Sio CCM tu. Hata ukiwauliza makamanda watakujibu hivohivo.
Mwenyekiti anasubiria kwa hamu kitakachotokea afanye BIASHARA.
 
Mangula usicheze na msiba shauri yako, utarudi kijijini kuuza nyanya, wewe toa ubatizo wa moto uendelee kubaki mjini
 
Inamaana kuna uwezakano wa dharura kutokea na kikao kuarishwa na kikiairishwa kimeairishwaaaa
Hakiwezi kuahirishwa mbona hakuna cha ajabu kitakachoongelewa hapo mnafikiri kuna jipya?

Ni mwedo wa kuwaonya tu wasiwe wanafiki na mambo yaendelee hamna mbishi hapo wote kama mkate kwenye chai
 
Mumewapima afya zao kwanza? Wamehakikishiwa usalama wao? Hoteli watakazofikia, vyakula na vinywaji watakavyokunywa, usafiri watakaotumia, viti watakavyokalia, vyoo watakavyojisaidia, sehemu zote watakazoshika, n.k. Nakumbuka ya Kolimba miaka mingi sana iliyopita.
 
Back
Top Bottom