Hatimaye Wazee na makada wenzangu wakongwe chamani Makamba, Kinana na Membe wameitwa kujitokeza mbele ya Kamati Ndogo ya Maadili ya chama hapa Dodoma. Kamati hii inaongozwa na Mzee Phillip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara.
Nimeshawasili hapa Dodoma tayari kuwapa 'support' wazee wenzangu na waliowahi kuwa viongozi wangu chamani na Serikalini. Wakifika, tutakutana hapa Dodoma na kujipanga ipasavyo kabla ya wao kujitokeza mbele ya Kamati ya Mangula. Tutajipanga kihoja, kiintelijensia na kadhalika.
Wakifika, tutapata fursa ya kisasa kutafakari mwenendo wa CCM yetu na kujiandaa kushauri kupitia wao mbele ya Kamati watakapojitokeza. Pamoja na kupokea barua za wito, hakuna ambaye hadi sasa anayajua mashtaka yanayomkabili mbele ya Kamati. Watashtukizwa!
Kwa namna mambo yalivyo, iko wazi kuwa, CCM haina jambo lolote la kuwafanya Makamba, Kinana na Membe. Hakuna hata mashtaka mahsusi kuwahusu na wao kujiandaa kwa utetezi wao hadisasa. CCM inafanya siasa tu. Inauaminisha umma kuwa ipo na inafanya kazi. Si zaidi!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma, Tanzania)