Bernard Membe aitwa kwenye Kikao cha Kamati ndogo ya Udhibiti wa Nidhamu CCM

Bernard Membe aitwa kwenye Kikao cha Kamati ndogo ya Udhibiti wa Nidhamu CCM

Nakuhakikishia kwamba kuna baadhi ya wajumbe wa hicho kikao ambao wametumwa kumhoji Membe hawajui na wala hawakujua 80% ya atakayoongea na watapigwa na butwaa , unyama unaotendwa ndani ya ccm wanaoufahamu ni watu 50 tu , Membe ni mmojawapo
Unavyongea/andika kwa kujiamini.
 
@Influenza,

barua kaandikiwa yeye, alafu yeye aanze kutangaza kwa umma kwani anaogopa nini kama anajiamini, mambo yake nayo yametuchosha, amalizane nao kisha kama anona kuna musada anataka kwa jamii ndo aandike, mbona anapotaka kufanya mambo yake ya kila siku haweki mtandaoni?

CCM aliingia mwenyewe na kuicha au kuivulimia ni wazo lake mwenyewe. Angetaka tujue angesema nimeitwa lakini sitaenda wachukue uamuzi wowote, ingekuwa na maana, atuache tupumue, bado tuna misiba mingi Arusha na JKT, tuna mawazo ya wapendwa wetu.
Huna haja ya kuusoma
 
Kama watakuwa fair naamini kikao kitakuwa nyepesi sana. Wanaweza kuanza kwa maswali lakini wakamaliza kwa kupiga soga.

Ingawa sijui hiyo Kamati ya Nidhamu ina wajumbe gani lakini huyu Mwana diplomasia na kachero mbobezi siyo level ya viongozi wa CCM tulionao sasa. Ni wasiwasi wao tu juu ya uwezekano wa Membe kuchukua fomu ya kugombea URais wa JMT kupitia CCM hapo Oktoba 2020.

Wasiwasi ni mkubwa kwa vile joto ni kali ndani ya CCM, asilimia 90% hawakubali Mwenyekiti wa CCM Taifa anavyoendesha nchi
 
Influenza, Sipati picha,
Inavyokuwa vigumu kufanya mahojiano na mtu anayekuzidi maarifa,ufahamu,ujuzi,akili,mwenye strong personality zaidi yako.
Wacha Kachelo aende akawakimbize hapo kikaoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ni lazima ajishikize na CCM maisha yake yote?

Kwanini asiachane na siasa tu kuliko kung'ang'ana na hilo lichama la majizi?

Au bado ana mgao huko?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hakuna mwanaccm mwizi anayeweza kuishi nje ya ccm, iwe Magufuli, JK, Mkapa au nani, wote salama yao ni kubaki ndani ya ccm. Ufahamu ccm sio chama cha siasa, bali ni kikundi cha mauaji kinachojificha ndani ya siasa.
 
Hakika nimeamini w/me wa Kusini ni watu wa kujiamini sana, angalia jamaa alivyoandika.

Hakuna cha kujiamini pale - ame-tweet akiwa na lengo la kutafuta public sympathy,basi!

We jiulize kulikuwa na ulazima gani kueleza Dunia kwamba amepata barua ya kuitwa kuhojiwa 06/02/2020 sijui saa ngapi? Hizo ni dalili za woga, sio ujasiri.

Membe unikumbusha Mrs Clinton ambaye mpaka sasa doesn't believe alishindwa na D.Trump, mama huyo hakubali yaishe bado anaendeleza kampeini zake za chini chini kujaribu ku-undermine Trump come rain come shine!!
 
Nadhani swala hili la Inchi yetu kuchafuka Kimataifa linampa faraja kubwa kwa sababu katika kipindi chake hatujawahi kushutumiwa.

Hii kutokushutumiwa kwa Kiongozi yeyote katika kipindi chake ni sifa moja kubwa kwake kwa sababu alikuwa Waziri wa mambo ya nje.

Kama tulivyoandika mwanzo, Membe aheshime taratibu za chama chake cha CCM za kuachiana miaka kumi kumi ya kikatiba katika nafasi ya Urais na baada ya hapo ni ruhusa kwake kujitokeza katika kuwania Urais.

Sasa hivi awe Karibu na Rais aliyeko madarakani ili amsaidie katika mambo ya Inchi za Nje.

Prof. Kabudi ni msomi mzuri na mwenye hoja lakini anasahau kuwa yuko kwenye Siasa ambako kunatakiwa itifaki na Diplomasia kuliko kuangalia ukweli uko wapi utafikiri anafundisha Darasani.

Mambo ya mafunzo ya Darasani na Diplomasia za Kimataifa ni tofauti kabisa. Anatakiwa kuwa na jicho la busara na si jicho la kumkodolea Trump na kumuona kama mkosaji.
 
Si mlisema hawana ubavu wa kumuita Membe?

Ccm si kama chadema kwamba kila mtu ni kambare

Sent using Jamii Forums mobile app
Ccm kwa kuhamisha magoli ni mafundi sana! Yaani mmeamua kuwaita kipindi hiki tuache kujadili ya Pompeo na marufuku ya Tramp eti tujadili kuitana kwenu kunywa mvinyo dodoma!
Wenye akili walishabaini agenda yenu ya kutusahaulisha kibano Cha WB, Pompeo na Trump!
 
Back
Top Bottom