Tunakujua kwa muda mrefu. Hujawahi kuyumba katika kile unachokiamini. Mara zote umekuwa ngangari katika mawazo yako. Membe mara zote umekuwa ukililia namna uchumi unavyozorota, biashara zinakufa, ajira vijana wetu hawapati, na walio kwenye ajira private sector nao wanajikuta kupoteza ajira zao kutokana na kampuni hizo kufunga biashara. Hiki ndio kimekuwa kilio chako kwa muda mrefu.
Leo najua unaenda kuwambia ukweli kuwa hawa viongozi waliovamia chama chetu ndio wametufikisha hapa tulipo mpaka tunaanza kuona mambo ya ajabu ya nchi washirika wetu kama USA, EU wanaanza kutuweka kwenye black list countries. Eti leo hii tuko sawa na Sudan, eti leo hii tuko sawa na Afghanistan.
Katika kamati hiyo ya leo is only Mangula ndio anakijua chama. wengine wote wageni, ni wa kuja. hawakijui chama zaidi yako na hawaijui mfumo either wa kawaida ama ule wa ukachero kama wewe. Hivyo, hawataweza kuwa na any input zaidi zaidi wataeleza kuwa umeonyesha kiburi hivyo watakupiga ban ya kiezi 8 usishiriki siasa ili uchaguzi wa August ndani ya chama upite salama!
Otherwise, tunakutakia kila la kheri. Wana CCM tulio wengi tuko na wewe Mkombozi wetu. Nenda Membe, nenda katuwakilishe Comrade, tuko na wewe pamoja katika hatua na katika sala!