Bernard Membe, aliyekuwa mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo kwenye Uchaguzi 2020, ajiondoa kwenye chama hicho

Bernard Membe, aliyekuwa mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo kwenye Uchaguzi 2020, ajiondoa kwenye chama hicho

Bernard Membe ambaye alikuwa mwanachama na mshauri wa ACT-Wazalendo ametangaza kujiondoa katika chama hicho

Membe, katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 aligombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hiko ambapo alifanya kampeni mikoa michache

Aidha, Membe, mwanachama mwenye kadi namba 2 ya ACT- Wazalendo amesema atajiondoa rasmi Januari 1, 2021

Kihistoria Membe aliingia ACT-Wazalendo mwaka 2020, akitokea CCM
Source of this information please!
Tafadhali Tupe chanzo cha hii taarifa, or attach a
video!
 
1607204437268.png

Mission accomplished.
 
Membe hajawahi kuwa mpinzani msidanganye watu, alikuwa muigizaji tu ndio maana akakosa impact baada ya kushtukiwa.
Membe hatokaa aisahau cdm maishani mwake maana cdm ndiyo ilikuwa ya kwanza kumpotezea Membe
 
Leo katika kipindi cha DW KISWAHILI Kulikuwa na mahojiano ambayo mmoja wa PANELISTS mama yetu Annanilea Nkya aliongelea suala la UDHAIFU WA VYAMA VYA UPINZANI NA VIONGOZI WAO........

Leo hii mzee Membe analidhihirisha hilo....

Ukitafakari juujuu utaona kama TATIZO LIKO CCM...la hashaa...tatizo liko UPINZANI....

Ni sawa na mwanamume mkubwa na mtimilifu kichwani aseme kuwa ALIBAKA kwa sababu ya UREMBO WA BINTI ALIYEMPITIA MBELE YAKE....🤣

2015 Mbowe anabadili gia...
2020 Zitto Kabwe anamrecruit mh.Membe.....

TAFAKARI
 
hivi membe ameisaidiaje ccm kwenye uchaguzi huu ? kuwa mkweli
Mkuu Yani hata hujui kuwa lengo la Membe kupelekwa kule ilikuwa nikufanya juu chini ili CDM na ACT wazalendo wasiungane katika Uchaguzi?

Hata hujiulizi kwanini baada ya kupitishwa kuwa Mgombea halisi hakutaka hata kupiga kampeni Wala kuwanadi Wagombea wake wa ubunge na udiwani wa ACT?

Unafikiri bila Membe hiyo combination ya Zitto+ Lissu+ Maalim CCM wangepumua?

Halafu leo kirahisi tu unakuja kusema Membe hakuisaidia CCM katika Uchaguzi, are you serious?

Kweli nimeamini Watanzania wengi bado hawaijui siasa na mbinu zake.
 
Back
Top Bottom