Bernard Membe, aliyekuwa mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo kwenye Uchaguzi 2020, ajiondoa kwenye chama hicho

Bernard Membe, aliyekuwa mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo kwenye Uchaguzi 2020, ajiondoa kwenye chama hicho

Kazi aliyotumwa hakuikamilisha hata robo, badala yake jamaa wakaona bora wajiongeze na "kura za kwenye mabegi meusi" kutafuta ushindi wa maigizo.

Sasa atulie kidogo halafu aombe msamaha arudi nyumbani, kwani mwenyekiti wao ana "huruma sana" anajua kuwasamehe.
 
Aidha, Membe, mwanachama mwenye kadi namba 2 ya ACT- Wazalendo amesema atajiondoa rasmi Januari 1, 2021
Chanzo cha taarifa hii ni kipi?

Kama ni kweli, kwanini asubiri mpaka 1 Jan 2021 badala ya kujiondoa leo? ACT wamtimue tu maana hana msaada wala faida kwenye chama.

Kama ni kujitoa alipaswa kufanya hivyo siku zile viongozi wake wanahamasisha wanachama wao ‘wamkate’ kwenye sanduku la kura na badala yake wampigie kura Lissu. That was humiliation.
 
Huyu ndio walimleta ili awe Rais wetu. Maaajabi.

Watu wana utani kama walitegemea kushinda kwa njia ile
 
Bernard Membe ambaye alikuwa mwanachama na mshauri wa ACT-Wazalendo ametangaza kujiondoa katika chama hicho

Membe, katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 aligombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hiko ambapo alifanya kampeni mikoa michache

Aidha, Membe, mwanachama mwenye kadi namba 2 ya ACT- Wazalendo amesema atajiondoa rasmi Januari 1, 2021

Kihistoria Membe aliingia ACT-Wazalendo mwaka 2020, akitokea CCM
Katika watu ambao sijawahi kuwaelewa ni huyu Membe... Watu walimjaza maneno mtandaoni na akajaa kwelikweli
 
Huyo nae ni garasa hana impact yoyote kwenye siasa za sasa labda kwa ccm wenzie wazee wa kubebwa na system.
Sass hapo CCM inahusikaje?

Ccm imefukuza Mwanachama wake, wazee wa shobo wakashoboka wakaona wameokota Dodo kwenye Mpera!
 
Mzee wa dakika ya 89 na ushee....

Mara ya mwisho nilisikia yuko busy anaunda baraza la mawaziri.
 
Back
Top Bottom