Bernard Membe, aliyekuwa mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo kwenye Uchaguzi 2020, ajiondoa kwenye chama hicho

Hivi tangu lini DGIS Mstaafu akanyea kambi?,
zile story za kumbakumba sijui kitu gani,yalikuwa maigizo tu,au ni secrets codes kwa wanaojua,
Mission zao zinakuwaga tofauti,kubadili upepo,au kujua upepo unaelekea wapi,
Baada ya hapo hata Awards zao wont come to light,
 
Huu ndo Upinzani wa Tanzania na tabia zake;

Kupokea makada wakongwe wa CCM Yani wale wa CCM damudamu
Kisha wanawapa vyeo vya juu ndani ya Chama mfano, wajumbe wa kamati kuu na n.k
Wanawapa nafasi za kugombea nafasi za juu kabisa kama Urais.

2015 ilitokea CDM baada ya Mzee mwenye nywele nyeupe kucheza na Akili zao.
2020 ikatokea kwa ACT wazalendo baada ya Jasusi mbobezi kucheza na Akili zao.
2025 tutegemee kada mwingine kwenda kucheza na Akili za Hawa wapinzani wetu.

Hivi nyie vyama vya Upinzani huwa hata hamjiulizi swali Hili; kwanini makada wakongwe wa chama Cha kijani hujifanya kuhamia kwenu wakati wa harakati za kampeni na Uchaguzi tu?
 
Mkuu Yani hata hujui kuwa lengo la Membe kupelekwa kule ilikuwa nikufanya juu chini ili CDM na ACT wazalendo wasiungane katika Uchaguzi?

Hata hujiulizi kwanini baada ya kupitishwa kuwa Mgombea halisi hakutaka hata kupiga kampeni Wala kuwanadi Wagombea wake wa ubunge na udiwani wa ACT?

Unafikiri bila Membe hiyo combination ya Zitto+ Lissu+ Maalim CCM wangepumua?

Halafu leo kirahisi tu unakuja kusema Membe hakuisaidia CCM katika Uchaguzi, are you serious?

Kweli nimeamini Watanzania wengi bado hawaijui siasa na mbinu zake.
mbona collabo ilipigwa ?
 
Hapa mkiwalaumu wapinzani mtakuwa mnawaonea. Upinzani ndio walimtumia na sio vingine. Chadema hawakushughulika nae na ACT-WAZALENDO wakaamua kumuacha mgombea wao na kum support Lissu waziwazi. Na kwa sababu palikuwa na vyama viwili vya upinzani vyenye nguvu ilikuwa vigumu kukabiliana nao.

Amandla...
 
Upinzani Waligundua kwenye sekeseke lile la Airport,
Maigizo yakaanzia pale,ila ilikuwa too late,
Uzuri walioufanya Walisave vifaranga wachache kuliwa na mwewe,if u what i mean
 
Bernard Membe ambaye alikuwa mwanachama na mshauri wa ACT-Wazalendo ametangaza kujiondoa katika chama hicho

Membe, katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 aligombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hiko ambapo alifanya kampeni mikoa michache

Aidha, Membe, mwanachama mwenye kadi namba 2 ya ACT- Wazalendo amesema atajiondoa rasmi Januari 1, 2021

Kihistoria Membe aliingia ACT-Wazalendo mwaka 2020, akitokea CCM
Kiukweli kabisa hili ni Joka tuu la Mdimu, hakuna kitu pale!. Tulimshauri hakusikia...

P
 
Mkuu Yani hata hujui kuwa lengo la Membe kupelekwa kule ilikuwa nikufanya juu chini ili CDM na ACT wazalendo wasiungane katika Uchaguzi?

Hata hujiulizi kwanini baada ya kupitishwa kuwa Mgombea halisi hakutaka hata kupiga kampeni Wala kuwanadi Wagombea wake wa ubunge na udiwani wa ACT?

Unafikiri bila Membe hiyo combination ya Zitto+ Lissu+ Maalim CCM wangepumua?

Halafu leo kirahisi tu unakuja kusema Membe hakuisaidia CCM katika Uchaguzi, are you serious?

Kweli nimeamini Watanzania wengi bado hawaijui siasa na mbinu zake.
Membe mnampa kichwa tu, kamwe hajawahi kuwa tishio. This time upinzani ulijua kuwa accommodate watu wa aina yake bila kuleta madhara. Kilichopelekea wasiungane wala siyo Membe bali ni sheria ya vuama iliyotungwa kimkakati.
 
Bado nangoja bao la dakika ya tisini. Wapinzani walimbwaga siku nyiiingi.
 
Tatizo sio Membe bali uwezo wenu wa kuusoma mchezo wa siasa za bongo. Mnapita mule mule!
vyama ya siasa vipo kwa mujibu wa katiba ambayo ndio inayo inachezewa..... mchezo ni kutoheshimika kwa katiba ya nchi wanaichezea mpaka sikukuu ya Uhuru (tunu ya taifa) inakua anasa na kero.... watoto wetu hawata ihitaji tena kwa hili linaloendelea..... katiba yetu ni mchezo mchafu ndio maana haisomeki
 
Huu ndo Upinzani wa Tanzania na tabia zake;

Kupokea makada wakongwe wa CCM Yani wale wa CCM damudamu
Kisha wanawapa vyeo vya juu ndani ya Chama mfano, wajumbe wa kamati kuu na n.k
Wanawapa nafasi za kugombea nafasi za juu kabisa kama Urais.

2015 ilitokea CDM baada ya Mzee mwenye nywele nyeupe kucheza na Akili zao.
2020 ikatokea kwa ACT wazalendo baada ya Jasusi mbobezi kucheza na Akili zao.
2025 tutegemee kada mwingine kwenda kucheza na Akili za Hawa wapinzani wetu.

Hivi nyie vyama vya Upinzani huwa hata hamjiulizi swali Hili; kwanini makada wakongwe wa chama Cha kijani hujifanya kuhamia kwenu wakati wa harakati za kampeni na Uchaguzi tu?
Ambaye mpaka sasa amecheza kadi zake vema na mnashindwa kumshitukia ni Mwalim Seif (huyu ni CCM kindakindaki)
 
Back
Top Bottom