CreativityCode
Senior Member
- Aug 8, 2020
- 158
- 653
Kwa dhati ya moyo wangu napenda kukiri kuwa mimi ni admirer wako toka ukiwa Waziri wa mambo ya Nje wa Tanzania.
Lakini kwa hali ya Siasa ilivyo nchini mwetu na kiu ya watanzania kuondokana na kivuli kizito kilichodumu kwa zaidi ya miaka 59 cha umasikini uliokithiri, ujinga, maradhi, ukiukwaji wa haki za binadamu, uonevu, umwagaji wa damu isiyo na hatia, ukosekanaji wa mfumo na dira kwa nchi yetu, ukurupukaji, ufinyu wa fikra, uungu mtu na mengine yanayofanana na hayo nakusihi kwa moyo mkunjufu umuachie Tundu Lissu ili atuvushe kipindi hiki cha uchaguzi na hatimaye awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Najua wewe kama alivyo Tundu Lissu una uelewa mpana wa masuala ya kimataifa na pengine unamzidi kwa sababu ya utumishi wako uliotukuka wakati ukiwa Waziri wetu wa Mambo ya Nje. Lakini nikiangalia kwa undani zaidi nadhani Tanzania inamuhitaji zaidi Tundu Lissu kuliko wewe kwa sababu chache zifuatazo.
MOSI
Tundu Lissu ni mpinzani halisi asiyetokana na CCM wa kizazi hiki hivyo akiwa Rais Tanzania itaondokana kabisa na vimelea vya CCM na kuwa na mfumo mpya kabisa. Tutapata mabadiliko ya kweli kutoka kwa Tundu Lissu.
PILI
Tundu Lissu ameonesha uwezo mkubwa sana nami kanishangaza, sikuwa namfahamu hivi hapo kabla, kitendo chake cha bila woga kumpinga John Magufuli ili asigombee Urais kwa sababu ya kukiuka sheria ya uchaguzi ni cha kipekee. Hakuna mtanzania yeyote yule aliyefahamu mapungufu yaliyogunduliwa na Tundu Lissu kwenye mchakato wa kutafuta wadhamini na fomu ya John Magufuli. Kitendo chake cha kwenda mbali zaidi na kusema maelekezo ya tume ya uchaguzi yanapingana na sheria ya uchaguzi, zaidi mgombea aliyefuata maelekezao ya Tume na siyo sheria ya uchaguzi kaingia chaka ni cha kipekee.
Imetufumbua macho watanzania. Baada ya Tundu Lissu kufafanua mapungufu ya mchakato wa John Magufuli kupata wadhamini na ujazwaji wa fomu ndipo nilipoelewa dhana halisi kuwa sheria ni msumeno licha ya kuwa na elimu ya juu na umri wa kati ya utu uzima na ujana. Sheria ni msumeno kweli kweli kwa maana kwa uhalisia isingekuwa mabavu na uonevu John Magufuli alikuwa aondoke. Hata hivyo hata akigombea amekwishapoteza uhalali mbele ya macho ya watanzania na dunia kwa ujumla.
TATU
Kupigwa risasi zaidi ya 16 ni zaidi ya kufungwa kwa Mandela na mashujaa wote duniani. Siyo rahisi kabisa, wengi tunafumba macho na kukebehi lakini kunusurika kifo siyo jambo dogo. Fikiria apigwe risasi kama hizo baba yako ama ndugu yako yeyote yule. Wekeni kumbukumbu Tundu Lissu atakuja kupata tuzo la amani la dunia, hili naliona. Tundu Lissu ni zaidi ya akina Mandela na Gadhi. Yuko levo ya binti mdogo Malala aliyenusurika kuuliwa na Talebani kisa anatetea haki za binti kupata elimu kwenye nchi yao ambayo inafuata sharia.
ANGALIZO
Kupigwa risasi haiwezi kamwe kuwa kigezo cha kuchagua mtu awe Rais wa Nchi, lakini tunaangalia reaction baada ya kupigwa risasi. Je, ameendeleza mapambano, ama kaogopa? ujasiri ndiyo kigezo kikubwa hapa.
Kwa sababu hizi tatu nashawishika kusema Tundu Lissu anatufaa zaidi kuliko wewe kipenzi changu Bernard Kamillius Membe.
MUNGU AWABARIKI, NAWAOMBEA AMANI WATANZANIA WENZANGU KWENYE KIPINDI HIKI KIGUMU