Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Nitagombea Urais Upinzani ukinipa ridhaa

Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Nitagombea Urais Upinzani ukinipa ridhaa

Gmox

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2014
Posts
319
Reaction score
478
Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Tanzania na kada wa chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa miongo mingi Bernard Membe anasema ikiwa Vyama vya Upinzani vitaungana na kumpa ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais, basi atakuwa tayari kupambana na Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Membe amesifia sehemu ya utendaji kazi wa Magufuli, lakini ameyataja baadhi ya mambo ambayo anasema ikiwa hayatabadilishwa, basi yataitumbukiza nchi matatani. Katika mahojiano haya maalum na mwandishi wa BBC Sammy Awami kutoka nyumbani kwake, katika kijiji alichozaliwa Membe alianza kwa kutoa tathmini ya uongozi wa Rais Magufuli.

Chanzo: BBC
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Tanzania na kada wa chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa miongo mingi Bernard Membe, anasema ikiwa vyama vya upinzani vitaungana na kumpa ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais, basi atakuwa tayari kupambana na Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba mwaka huu
Tundu Lissu na Nyalandu watafute majimbo hiyo ni Gia Angani tayari!
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Tanzania na kada wa chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa miongo mingi Bernard Membe, anasema ikiwa vyama vya upinzani vitaungana na kumpa ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais, basi atakuwa tayari kupambana na Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba mwaka huu
Kama ni kweli basi wamemfikisha walipotaka awe, Membe finished!
1593677963878.png
 
Safi sana, hii ndo kauli ya kiume tuliyokuwa tukiingoja.

Kwenye siasa za nchi yetu hakuna dhambi kubwa kama kumuacha Magufuli apite bila kuwa challenged.

Magufuli inabidi awe Challenged na ashindwe kwa kura za wananchi, akiamua kufanya ya Jecha afanye lakini huku akijua wananchi walimkataa, labda hiyo. itamfanya awe humble la sivyo atatuvuruga sana!
 
Kama ni kweli basi wamemfikisha walipotaka awe, Membe finished!
View attachment 1495153
Hivi vyma vya upinzani ni jalala? Kila anayetofautina na CCM anakimbilia huko! Pia upinzania hutaki kujifunza kwa UKAWA ambao walipata nguvu ya Lowasa na Sumaye lakini leo wote wamerudi nyumbani kwao!

Watafute mgombe wao wenyewe si mtu ajinadi tena kwa kuwapa masharti ya kuungana! Hivi ni rahisi ACT kuungana na CHAADEMA , CUF, NCCR?
 
Back
Top Bottom