Mudawote
JF-Expert Member
- Jul 10, 2013
- 10,771
- 14,129
Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Tanzania na kada wa chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa miongo mingi Bernard Membe anasema ikiwa vyama vya upinzani vitaungana na kumpa ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais, basi atakuwa tayari kupambana na Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba mwaka huu.
Membe amesifia sehemu ya utendaji kazi wa Magufuli, lakini ameyataja baadhi ya mambo ambayo anasema ikiwa hayatabadilishwa, basi yataitumbukiza nchi matatani. Katika mahojiano haya maalum na mwandishi wa BBC Sammy Awami kutoka nyumbani kwake, katika kijiji alichozaliwa Membe alianza kwa kutoa tathmini ya uongozi wa Rais Magufuli.
Chanzo: BBC
Hahahahaha wapinzani mjiandae tena, mmeletewa tena mtu, hahahaha, akishashindwa uchaguzi 2020, taaratibu atarejea CCM huku akiwa mpole na kuomba msamaha hahahaha, wapinzani wa Tanzania itawachukua muda sana kuuelewa huu mchezo!