Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Nitagombea Urais Upinzani ukinipa ridhaa

Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Nitagombea Urais Upinzani ukinipa ridhaa

Kumbe mnamchukulia Lowasa kama Tapeli ?!

Inamaana hamtambui mchango mkubwa alofanya wa kuja na hamasa ya wanachama wapya pamoja na kuwa boost kuweza kupata wabunge wengi na madiwani?

Mnazani bila Lowasa mngeweza kufika pale?

Ama kweli shukrani za Punda mateke!

Kwa mtu asiyejua siasa ndio anaweza kusema kura za cdm zililetwa na Lowassa. Cdm ilikuwa imejipanga, tena huyo Lowassa ndiye aliyekuja cdm kupandikiza siasa za kikondoo. Hivi ni nani kakuambia kura zanaletwa kwa kusema "kipaombele changu ni elimu, elimu, elimu". Alaaniwe Mbowe na kundi lake kumkaribisha huyo mzee muhuni toka ccm.
 
Upinzani wasidanganyike, alichofanya lowassa kinatosha bora wapambane wenyewe
Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Tanzania na kada wa chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa miongo mingi Bernard Membe anasema ikiwa vyama vya upinzani vitaungana na kumpa ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais, basi atakuwa tayari kupambana na Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Membe amesifia sehemu ya utendaji kazi wa Magufuli, lakini ameyataja baadhi ya mambo ambayo anasema ikiwa hayatabadilishwa, basi yataitumbukiza nchi matatani. Katika mahojiano haya maalum na mwandishi wa BBC Sammy Awami kutoka nyumbani kwake, katika kijiji alichozaliwa Membe alianza kwa kutoa tathmini ya uongozi wa Rais Magufuli.

Chanzo: BBC
 
Mngemjua vizuri kwanza Bernard kuliko kushangilia,binafsi siamini kama anabifu na JPM au CCM.......ila ni mbinu za siasa tu........ngoja niishie hapo tu
 
Kwa mtu asiyejua siasa ndio anaweza kusema kura za cdm zililetwa na Lowassa. Cdm ilikuwa imejipanga, tena huyo Lowassa ndiye aliyekuja cdm kupandikiza siasa za kikondoo. Hivi ni nani kakuambia kura zanaletwa kwa kusema "kipaombele changu ni elimu, elimu, elimu". Alaaniwe Mbowe na kundi lake kumkaribisha huyo mzee muhuni toka ccm.

Sawa nyie mkataaeni Membe halafu tuone matokeo baada ya Uchaguzi yatakavyokuwa.

Hatuombei mabaya ya kushindwa lakini mambo siyo rahisi kama mtu mwingine anavyoweza kuzani.

Hiyo sera/hoja ya elimu ya Lowasa huoni imesaidia kuchukuliwa na serikali na sasa watoto wanasoma bure hadi kidato cha 4?!

Binafsi nimejifunza na kuweza kutambua uzuri wa ja(ma)mbo katika hali yoyote ile.

Ni kwa bahati mbaya sana watu wengi ama kwa kutokujua hukimbilia kuona mabaya au madhaifu badala ya mazuri ya mtu au hali fulani.

Ingekuwa kheri kwetu tungejizoesha kuona mazuri kwanza na kuanza kuamua.
 
Mkuu naona umekimbilia kuni attack bila sababu, kwa tulioiona thread dakika chache baada ya kupostiwa aliandika ile haya moja tu. Kaongezea maelezo baadae, anyway huyo Membe Kuna watu wa mataifa ya mbali waliwekeza kwake pesa nyingi sana akiwaaminisha atapindisha meza. Sasa CCM wamemwekea ngumu kibabe, Sasa kaa mkao ukisikia anakuja CDM style ya Lowassa usishangae, hakuna kinachoshindikana kwenye shilingi. Zamu hii ndo mtaelewa kuwa hakuna upinzani wa maana Tanzania.

Inawezekana hakuna chama cha maana cha upinzani kutokana na mazingira yaliyopo, ila sio upinzani boss. Tunajitambua vizuri kupita maelezo. Na uzuri sasa hivi tunaweza kufanya siasa na wananchi bila hata kutegemea vyama vya siasa, iwe upinzani, au hao wezi wa kura ccm. Wananchi walishaamka, Magufuli ndio anashurutisha wananchi warudi kwenye siasa za kina Nyerere, za karne iliyopita.

Nadhani kama unafuatilia vizuri, wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa wananchi tulisema hatuko tayari kushiriki uchaguzi katika mazingira yaliyopo, hasa kwa ule uhuni wa kitoto, ushenzi na ukatili wa wazi kwenye chaguzi za marudio. Baadhi ya viongozi wa upinzani kama Mbowe, Halima Mdee, Zito, na wanaccm wengi, walihimiza kujiandikisha lakini hatukutokea. Na hata sasa, wananchi wengi hawajajitokeza kujiandikisha, ama kuhakiki kwani watu wamechoka kufanywa wapuuzi. Tegemea wapiga kura wachache sana safari hii, bila tume huru vya uchaguzi, tena wengi wao ni wanaccm wenye uelewa mdogo, na wale wanaccm washabiki maandazi. Lakini hamna mwanaume kabisa anayesimamisha vizuri, atashiriki huo uhanithi bila tume huru ya uchaguzi.
 
Zito kamkaribisha kabla..Simuamini(zito) hata aseme Nini.Nikikumbuka uanzishwaji wa Act na tuhuma za kupewa pesa za kampeni kipindi Cha jk naona hii ya member Ni ile ile Mbinu ya ccm kugawa Kura za upinzani. Wapinzani kataeni kata kata kumpa nafasi huyo mtu, Akitaka aje km mwanachama na mshauri Basi.Akili yangu inagoma kbs huyo bwana kuja upinzani...kuna Jambo naamini kbs hatulijui.Watanzania hasa nyie viongozi wa vyama pinzani TAKE CARE.
 
Wapinzania natarajia kuona mkimpokea na kumpa nafasi ili awasaidie.
 
Karibu Membe tunyukane kwa hoja
Mlimchukua lowasa mkajikuta mmeangukia pua, huyu pia bwana membe mnataka mfanye trial and error na hakika mtajuta pia,

halafu sio ya kwamba vyama vya upinzani mmekosa watu wa kumtingisha jemedali magu, wakina lissu mbona wana uwezo wa kumtingisha upinzani kajitoa sana lissu mpaka anakaribia kutoa uhai wake..
 
Sawa nyie mkataaeni Membe halafu tuone matokeo baada ya Uchaguzi yatakavyokuwa.

Hatuombei mabaya ya kushindwa lakini mambo siyo rahisi kama mtu mwingine anavyoweza kuzani.

Hiyo sera/hoja ya elimu ya Lowasa huoni imesaidia kuchukuliwa na serikali na sasa watoto wanasoma bure hadi kidato cha 4?!

Binafsi nimejifunza na kuweza kutambua uzuri wa ja(ma)mbo katika hali yoyote ile.

Ni kwa bahati mbaya sana watu wengi ama kwa kutokujua hukimbilia kuona mabaya au madhaifu badala ya mazuri ya mtu au hali fulani.

Ingekuwa kheri kwetu tungejizoesha kuona mazuri kwanza na kuanza kuamua.

Sera ya elimu bure ilikuwa ni ya cdm uchaguzi wa 2010, mbali ya sera hiyo pia walihubiri sera ya kila mwananchi kujenga nyumba bora, na kuachana na nyumba za tembe, kwa ahadi ya kushusha vifaa vya ujenzi. Ccm walisema sera ya elimu bure haiwezekani, lakini ilibidi waiweke kwenye ilani yao, maana walijua cdm wakiitumia kwenye kampeni ya 2015 ingekula kwao.

Hivyo sera ya elimu bure sio ya Lowassa kama mgombea wa urais, bali ni sera ya cdm, tena bure yao ni kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu. Lakini kwakuwa umeanza siasa juzi, chini ya awamu hii ya tano, ndio unajua haya ni mambo mageni. Sisi tumeamua kuangalia mabaya, ni jukumu lako kuangalia hayo mazuri. Ili umeme uwake lazima kuwe na nyaya mbili, wa positive na negative.
 
Inawezekana hakuna chama cha maana cha upinzani kutokana na mazingira yaliyopo, ila sio upinzani boss. Tunajitambua vizuri kupita maelezo. Na uzuri sasa hivi tunaweza kufanya siasa na wananchi bila hata kutegemea vyama vya siasa, iwe upinzani, au hao wezi wa kura ccm. Wananchi walishaamka, Magufuli ndio anashurutisha wananchi warudi kwenye siasa za kina Nyerere, za karne iliyopita.

Nadhani kama unafuatilia vizuri, wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa wananchi tulisema hatuko tayari kushiriki uchaguzi katika mazingira yaliyopo, hasa kwa ule uhuni wa kitoto, ushenzi na ukatili wa wazi kwenye chaguzi za marudio. Baadhi ya viongozi wa upinzani kama Mbowe, Halima Mdee, Zito, na wanaccm wengi, walihimiza kujiandikisha lakini hatukutokea. Na hata sasa, wananchi wengi hawajajitokeza kujiandikisha, ama kuhakiki kwani watu wamechoka kufanywa wapuuzi. Tegemea wapiga kura wachache sana safari hii, bila tume huru vya uchaguzi, tena wengi wao ni wanaccm wenye uelewa mdogo, na wale wanaccm washabiki maandazi. Lakini hamna mwanaume kabisa anayesimamisha vizuri, atashiriki huo uhanithi bila tume huru ya uchaguzi.
Mkuu siku zote unafikra nzuri sana Ila sio kila mtu anafikiri kama wewe. Kwa mfano 2015 ulikuwa unapinga ujio wa Lowassa na kupewa nafasi Kama mgombea, Ila uliona umati uliochukuliwa na upepo wa ""Mabadilikooo Lowassa., Lowassa Mabadilikooo"" huku wakizungusha mikono?????, Najaribu kukupa picha ya wapiga kura wa TZ ambao wengi wao thinking capacity is very low. Kwahiyo unaposema sisi tuliowengi sielewi unamaanisha wananchi hawahawa au wa kutoka bara jingine??!?
 
Mkuu hitaki democrasia itawale?

Membe ataenda ACT na lengo la zito si kushinda urais bali awape nguvu ya kushinda viti viwili vitatu vya ubunge kwa ajili ya ruzuku ya kuwawezesha Seif na Zitto wasife njaa

Wao ACT sio kumpokea tu Membe, hata wakitaka wahamie nyumbani kwake kabisa, lakini sisi wapiga kura wa upinzani tunaojitambua, hatuko tayari kurudia kosa la Lowassa. Na sana sana hatuko tayari kujitokeza kupiga kura kwa tume hii ya kihuni.
 
Hivi vyma vya upinzani ni jalala? Kila anayetofautina na CCM anakimbilia huko! Pia upinzania hutaki kujifunza kwa UKAWA ambao walipata nguvu ya Lowasa na Sumaye lakini leo wote wamerudi nyumbani kwao! Watafute mgombe wao wenyewe si mtu ajinadi tena kwa kuwapa masharti ya kuungana! Hivi ni rahisi ACT kuungana na CHAADEMA , CUF, NCCR?
Baba wa Taifa alisha sema upinzani madhubuti utatoka CCM. Yetu macho.
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Tanzania na kada wa chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa miongo mingi Bernard Membe anasema ikiwa vyama vya upinzani vitaungana na kumpa ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais, basi atakuwa tayari kupambana na Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Membe amesifia sehemu ya utendaji kazi wa Magufuli, lakini ameyataja baadhi ya mambo ambayo anasema ikiwa hayatabadilishwa, basi yataitumbukiza nchi matatani. Katika mahojiano haya maalum na mwandishi wa BBC Sammy Awami kutoka nyumbani kwake, katika kijiji alichozaliwa Membe alianza kwa kutoa tathmini ya uongozi wa Rais Magufuli.

Chanzo: BBC

Ni kweli kuna mazuri yaliyofanywa, katika kutangaza nia na kugombea hakuna haja ya kuwa na jazba, kitu cha muhimu eleza sera zako na nini utakifanya kwa watanzania
 
Back
Top Bottom