Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Nitagombea Urais Upinzani ukinipa ridhaa

Hahaha, yaleyale ya Lowassa kukubaliana na mshindi wa CCM.

Ushauri wa bure;

Ni bora wapinzani wasishiriki uchaguzi mgombea wa ccm apite kuliko kupokea masalia kutoka ccm wanaokuja kudhoofisha Ari ya Upinzani
Lowassa alikubali ushindi wa CCM asubuhi na mapemaa huku akileta story sijui tutakwemda ICC(Nadhani walituona ni wapumbavu wa kiwango cha lami).
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Tanzania na kada wa chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa miongo mingi Bernard Membe anasema ikiwa Vyama vya Upinzani vitaungana na kumpa ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais, basi atakuwa tayari kupambana na Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Membe amesifia sehemu ya utendaji kazi wa Magufuli, lakini ameyataja baadhi ya mambo ambayo anasema ikiwa hayatabadilishwa, basi yataitumbukiza nchi matatani. Katika mahojiano haya maalum na mwandishi wa BBC Sammy Awami kutoka nyumbani kwake, katika kijiji alichozaliwa Membe alianza kwa kutoa tathmini ya uongozi wa Rais Magufuli.

Chanzo: BBC

Tafadhali KK ya CHADEMA..Msikilizeni Membe...
 
Inawezekana hakuna chama cha maana cha upinzani kutokana na mazingira yaliyopo, ila sio upinzani boss. Tunajitambua vizuri kupita maelezo. Na uzuri sasa hivi tunaweza kufanya siasa na wananchi bila hata kutegemea vyama vya siasa, iwe upinzani, au hao wezi wa kura ccm. Wananchi walishaamka, Magufuli ndio anashurutisha wananchi warudi kwenye siasa za kina Nyerere, za karne iliyopita.

Nadhani kama unafuatilia vizuri, wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa wananchi tulisema hatuko tayari kushiriki uchaguzi katika mazingira yaliyopo, hasa kwa ule uhuni wa kitoto, ushenzi na ukatili wa wazi kwenye chaguzi za marudio. Baadhi ya viongozi wa upinzani kama Mbowe, Halima Mdee, Zito, na wanaccm wengi, walihimiza kujiandikisha lakini hatukutokea. Na hata sasa, wananchi wengi hawajajitokeza kujiandikisha, ama kuhakiki kwani watu wamechoka kufanywa wapuuzi. Tegemea wapiga kura wachache sana safari hii, bila tume huru vya uchaguzi, tena wengi wao ni wanaccm wenye uelewa mdogo, na wale wanaccm washabiki maandazi. Lakini hamna mwanaume kabisa anayesimamisha vizuri, atashiriki huo uhanithi bila tume huru ya uchaguzi.
Watu wanataka madaraka iwe kwa kupiga kura au kwa kususa, wao wanachotaka ni kutawala. Ukisusa wao wakatawala na ukatii sheria hakuna tatizo hata ukisusa kila awamu usiende kupiga kura.
 
Inawezekana hakuna chama cha maana cha upinzani kutokana na mazingira yaliyopo, ila sio upinzani boss. Tunajitambua vizuri kupita maelezo. Na uzuri sasa hivi tunaweza kufanya siasa na wananchi bila hata kutegemea vyama vya siasa, iwe upinzani, au hao wezi wa kura ccm. Wananchi walishaamka, Magufuli ndio anashurutisha wananchi warudi kwenye siasa za kina Nyerere, za karne iliyopita.

Nadhani kama unafuatilia vizuri, wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa wananchi tulisema hatuko tayari kushiriki uchaguzi katika mazingira yaliyopo, hasa kwa ule uhuni wa kitoto, ushenzi na ukatili wa wazi kwenye chaguzi za marudio. Baadhi ya viongozi wa upinzani kama Mbowe, Halima Mdee, Zito, na wanaccm wengi, walihimiza kujiandikisha lakini hatukutokea. Na hata sasa, wananchi wengi hawajajitokeza kujiandikisha, ama kuhakiki kwani watu wamechoka kufanywa wapuuzi. Tegemea wapiga kura wachache sana safari hii, bila tume huru vya uchaguzi, tena wengi wao ni wanaccm wenye uelewa mdogo, na wale wanaccm washabiki maandazi. Lakini hamna mwanaume kabisa anayesimamisha vizuri, atashiriki huo uhanithi bila tume huru ya uchaguzi.
Najua kabisa ushindi wa upinzani kwenye uchaguzi bila tume huru ni ngumu lakini kususia uchaguzi na kumpa Magufuli ushindi wa mezani ni hatari kubwa. Wapinzani wanatakiwa wajitutumue kwa kadri wawezavyo kum-challenge Magufuli. Lengo liwe ni kumpa wakati mgumu. Pamoja na kuwa atahakikisha anatumia vyombo vya dola kupata ushindi lakini kuna wakati mwingine nguvu ya wananchi ikiwa kubwa wanaogopa. Pia hata wakiiba lakini atajiuliza mara mbili mbili namna anavyoongoza. Hili la wapinzani kususia ni kuwa Magufuli ameshalitafutia solution tayari: i.e. Chama cha NCCR Mageuzi. Atahakikisha anawashirikisha kwenye uchaguzi kwa gaharama yake, na kuwapa baadhi ya majimbo ili ionekane kuwa uchaguzi ulifanyika na waliosusia hawana sababu za msingi. Mwizi akienda kuiba sehemu akikutana na upinzani mkali, hata kama ataiba lakini kesho atajiuliza mara mbili kama arudi tena, lakini akikuta mteremko kesho atarudi tena. Na mwisho hata kama wapinzani hawatashinda lakini uchaguzi ujao watakuwa wamejifunza mengi na watapata wagombea wengi watakatiwa motisha na uungwaji mkono ulioonyeshwa.
 
Kwani unaweza kupambana na wala rushwa ,madawa ya kulevya bila kutumia dolla ,mahakama na bunge?
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Tanzania na kada wa chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa miongo mingi Bernard Membe anasema ikiwa Vyama vya Upinzani vitaungana na kumpa ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais, basi atakuwa tayari kupambana na Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Membe amesifia sehemu ya utendaji kazi wa Magufuli, lakini ameyataja baadhi ya mambo ambayo anasema ikiwa hayatabadilishwa, basi yataitumbukiza nchi matatani. Katika mahojiano haya maalum na mwandishi wa BBC Sammy Awami kutoka nyumbani kwake, katika kijiji alichozaliwa Membe alianza kwa kutoa tathmini ya uongozi wa Rais Magufuli.

Chanzo: BBC

Naogopa hayo maneno ya mwandishi hapo kwenye dakika 3:41
 
Politics on politics. Kadi aliyonayo ni ya CCM; kila anapozungumza mambo ya SIASA huzungumzia Chama Changu CCM halafu uteuzi anataka toka kwa ACT/CHADEMA!!!! Ni lini alikatwa POSHO /Mshahara wake kuvichangia hivyo vyama?
 
Membe ni nani hasa wakutoa sharti? Hapo ndipo upinzania unapohidharaulisha. Lowassa alikuja na sharti la kuwa mgombea urais akapewa nafasi akachomoka na nguvu ya Chadema ambayo ilianza kuonekana dhahiri

Huyu naye anakuja na sharti jingine kwamba ni wapinzani waungane kwanza labda tujiulize hao wapinzania anaowataka waungane ni kina nani hasa?

ACT WAZALENDO, CHADEMA, TLP, TADEA, CHAUMA, NCCR MAGEUZI au upinzania gani hasa?

ACT WAZALENDO wanaweza kuwa tayari kuunganisha nguvu na CHADEMA lakini so kinyume chake. Tayari Katibu Mkuu Be. John Mnyika alishasema wao wanakikaribisha chama chochote kushirikiana nao na sio wao kushirikiana na chama chochote.

Wasalaam
 
Kama kweli ana nia ya kuongoza mapambano ya kuleta demokrasia ya kweli basi na atusaidie kumnadi na kumtetea Commander LISSU!
👊 ✌️✌️✌️💥
 
Faida za kumkubali Membe ni nyingi kuliko hasara kama ilivyokuwa kwa Mamvi.

Membe ataleta hamasa ya wanachama na wasiowanachama kupigia kura ya ndiyo kwa madiwani , wabunge na hata kugawana /kupunguza kura za urais.
Kumbe mnajua mshashindwa mnataka tu kupunguza kura?.
 
Najua kabisa ushindi wa upinzani kwenye uchaguzi bila tume huru ni ngumu lakini kususia uchaguzi na kumpa Magufuli ushindi wa mezani ni hatari kubwa. Wapinzani wanatakiwa wajitutumue kwa kadri wawezavyo kum-challenge Magufuli. Lengo liwe ni kumpa wakati mgumu. Pamoja na kuwa atahakikisha anatumia vyombo vya dola kupata ushindi lakini kuna wakati mwingine nguvu ya wananchi ikiwa kubwa wanaogopa. Pia hata wakiiba lakini atajiuliza mara mbili mbili namna anavyoongoza. Hili la wapinzani kususia ni kuwa Magufuli ameshalitafutia solution tayari: i.e. Chama cha NCCR Mageuzi. Atahakikisha anawashirikisha kwenye uchaguzi kwa gaharama yake, na kuwapa baadhi ya majimbo ili ionekane kuwa uchaguzi ulifanyika na waliosusia hawana sababu za msingi. Mwizi akienda kuiba sehemu akikutana na upinzani mkali, hata kama ataiba lakini kesho atajiuliza mara mbili kama arudi tena, lakini akikuta mteremko kesho atarudi tena. Na mwisho hata kama wapinzani hawatashinda lakini uchaguzi ujao watakuwa wamejifunza mengi na watapata wagombea wengi watakatiwa motisha na uungwaji mkono ulioonyeshwa.

Uko sahihi kabisa. Mimi binafsi sio muumini wa kususia uchaguzi. Ila sijafikia hitimisho hili kwa bahati mbaya. Hivi unapata picha gani, unapoteza muda wako, kisha unalinda kura, halafu yule uliyepoteza muda wako anahama kwenda kuunga mkono juhudi, hilo ni moja. Kwenye chaguzi za marudio tuliona wizi, ushenzi na ukatili wa wazi ili ccm kutangazwa washindi, tukashauri vyama vikafungue kesi mahakamani ili haki ipatikane, lakini hilo halikufanyika. Tumeona wasimamizi wa tume wakifunga ofisi, na kuacha kupokea fomu za wapinzani na ushahidi upo, hayo nayo kesi hazifunguliwi. Sasa kama nguvu ya umma haitumiki, basi tutumie njia ya mahakama, hayo yote hayafanyiki, hapo nashiriki kupiga kura ili iweje, zaidi ya kwenda kubariki uhuni?

Sasa katika hayo mambo machache unashiriki uchaguzi ili upate nini labda? Bora kutokupoteza muda, maana sio lazima uongozi upatikane kwa njia ya box la kura. Tulikuwa tumeanza kudai tume huru ya uchaguzi kabla ya Katazo la Covid 19, lakini sasa tumekaa kimya kwenye hilo, huku tukitaka kuendelea kushiriki uchaguzi kwa mbinu zile zile, tukitarajia matokeo tofauti. Mkuu mimi sio wa akili hizo.
 
Back
Top Bottom