Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu naomba nikuulize swali na naomba unijibu toka moyoni., Ikitokea CHADEMA na muungano wa vyama vya upinzani wakakubali kumsimamisha Membe Kama mgombea wao wa uraisi reaction yako itakuwa ni nini!?Wao ACT sio kumpokea tu Membe, hata wakitaka wahamie nyumbani kwake kabisa, lakini sisi wapiga kura wa upinzani tunaojitambua, hatuko tayari kurudia kosa la Lowassa. Na sana sana hatuko tayari kujitokeza kupiga kura kwa tume hii ya kihuni.
Mkaribisheni huko huko Ccm ashindane Mwenyekiti wenu.C
Uchaguzi ulopita CDM walipata wabunge na madiwani wengi sababu ya uwepo wa Ukawa na Lowasa.
Mkaribesheni Membe faida mtazopata ni nyingi kuliko hasara.
Mkuu siku zote unafikra nzuri sana Ila sio kila mtu anafikiri kama wewe. Kwa mfano 2015 ulikuwa unapinga ujio wa Lowassa na kupewa nafasi Kama mgombea, Ila uliona umati uliochukuliwa na upepo wa ""Mabadilikooo Lowassa., Lowassa Mabadilikooo"" huku wakizungusha mikono?????, Najaribu kukupa picha ya wapiga kura wa TZ ambao wengi wao thinking capacity is very low. Kwahiyo unaposema sisi tuliowengi sielewi unamaanisha wananchi hawahawa au wa kutoka bara jingine??!?
Membe ni kama Lowassa tu,atashindwa uchaguzi then atarudi zake kwao CCM mchezo umeisha.Haya mambo yananichanganya sana / au tumpe Membe au Lissu kiukweli mimi sijausoma mchezo vzr
Nakueleza waliopiga kura 2015 hawakupata muda wa kujiuliza maana wakibadilishwa gia angani na Mbowe na genge lake. Hali ile ilikuwa kama unapiga hizi nyimbo za injili zenye midundo ya bolingo, mara ghafla unaweka wa Koffi olomide, ni wazi watu wataendelea kucheza, lakini baada ya muda watajua mashairi sio ya Yesu. Kilichoendelea kwenye chaguzi zetu za marudio, uchaguzi wa serikali za mitaa, na Lowassa kurudi ccm, kumewafanya watu kujiuliza mara mbili mbili hizi siasa za kihuni. Ndio maana unaona kwa sasa, wapiga kura wengi wa upinzani, hao uliiwaona 2015, wakigoma kushiriki uchaguzi.
Nakuhakikishia bila tume huru ya uchaguzi, tegemea wapiga kura wachache sana, kwani ccm haina mvuto zaidi ya kushurutisha kukubalika, na iwapo wapinzani hasa cdm wataweka mgombea asiye na mvuto nje ya Tundu Lissu, hamasa itakuwa chini sana. Hilo litapelekea wapiga kura kuwa wachache, au wa wastani lakini wasio na hamasa, kwani kiu yao ya mabadiliko itakuwa haijatimia.
Kwangu mimi wakifanya hivyo sitapiga kura na nitawaona wapinzani ni mataahira kwa 100%.Mkuu naomba nikuulize swali na naomba unijibu toka moyoni., Ikitokea CHADEMA na muungano wa vyama vya upinzani wakakubali kumsimamisha Membe Kama mgombea wao wa uraisi reaction yako itakuwa ni nini!?
NB:. Assume imekuwa hivyo ili jibu lako lisiegemee kuniambia haiwezekani, hata 2015 watu walijiapiza kwa kila namna Lowassa hawezi kuja CHADEMA.
Membe ni kama Lowassa tu,atashindwa uchaguzi then atarudi zake kwao CCM mchezo umeisha.
Pandikizi tu hilo.
Akiruhusu upuuzi wa Membe kugombea kupitia Chadema nita-confirm Rasmi Mbowe ni pandikizi la CCM na hana tofauti na wakina Mbatia,Mrema,Cheyo,Shibuda etc.We muache Mbowe aje alete utopolo tutamvunja mguu wa pili.
Ni vigumu kunielewa maana umeamua kuvutia upande wako. Na una Imani na uelewa wa wapiga kura as if wanajitambua. Okay., Tume haiko huru kama unavyodai, Ila wapinzani watashiriki Kama kawa bila kujali. Wapiga kura watakuwa wachache Kama unavyodai Ila uchaguzi utafanyika, unadhani wapinzani wanategemea nini kushiriki?, Na matokeo yatakuwaje kwa mtazamo wako!?Nakueleza waliopiga kura 2015 hawakupata muda wa kujiuliza maana wakibadilishwa gia angani na Mbowe na genge lake. Hali ile ilikuwa kama unapiga hizi nyimbo za injili zenye midundo ya bolingo, mara ghafla unaweka wa Koffi olomide, ni wazi watu wataendelea kucheza, lakini baada ya muda watajua mashairi sio ya Yesu. Kilichoendelea kwenye chaguzi zetu za marudio, uchaguzi wa serikali za mitaa, na Lowassa kurudi ccm, kumewafanya watu kujiuliza mara mbili mbili hizi siasa za kihuni. Ndio maana unaona kwa sasa, wapiga kura wengi wa upinzani, hao uliiwaona 2015, wakigoma kushiriki uchaguzi.
Nakuhakikishia bila tume huru ya uchaguzi, tegemea wapiga kura wachache sana, kwani ccm haina mvuto zaidi ya kushurutisha kukubalika, na iwapo wapinzani hasa cdm wataweka mgombea asiye na mvuto nje ya Tundu Lissu, hamasa itakuwa chini sana. Hilo litapelekea wapiga kura kuwa wachache, au wa wastani lakini wasio na hamasa, kwani kiu yao ya mabadiliko itakuwa haijatimia.
Mkuu naomba nikuulize swali na naomba unijibu toka moyoni., Ikitokea CHADEMA na muungano wa vyama vya upinzani wakakubali kumsimamisha Membe Kama mgombea wao wa uraisi reaction yako itakuwa ni nini!?
NB:. Assume imekuwa hivyo ili jibu lako lisiegemee kuniambia haiwezekani, hata 2015 watu walijiapiza kwa kila namna Lowassa hawezi kuja CHADEMA.
BBC hapo???Muwe mnaweka na vyanzo vya habari zenu, sio mnakurupuka tu na kuanzisha thread.
Membe angepata heshima kubwa kama angejitokeza kuwa mbele kuleta mapinduzi bila ya kuweka masharti ya kupewa nafasi ya uongozi katika chama chochote au sehemu yoyote.
Hii ingewaonyesha watu kwamba anachukizwa na yaliyopo huko CCM, kwa hiyo yeye atachangia kwa vyovyote iwezekanavyo kuyaondoa.
Huo ndio ungekuwa msisitizo wake.
Na baada ya kufanya hivyo kazi na kuleta mafanikio, basi, angefikiriwa kupewa nafasi yoyote ya uongozi mbali ya hiyo ya urais.
Kauli mbiu iwe: "Kazi Kwanza, Malipo ni Baada ya Kazi."
Umekuja Sasa hivi saa 8, unajua saa 5 wakati anapost thread aliishia wapi?, Hujui watu JF wanaletaga habari nusunusu waonekane wa kwanza kupost baadae wanaongezea story?., Mimi sio mjinga kumwambia hivyo, alileta story robo mwanzoni.Mkurupukaji ni wewe, hujaona chanzo
BBC hapo???
Ni vigumu kunielewa maana umeamua kuvutia upande wako. Na una Imani na uelewa wa wapiga kura as if wanajitambua. Okay., Tume haiko huru kama unavyodai, Ila wapinzani watashiriki Kama kawa bila kujali. Wapiga kura watakuwa wachache Kama unavyodai Ila uchaguzi utafanyika, unadhani wapinzani wanategemea nini kushiriki?, Na matokeo yatakuwaje kwa mtazamo wako!?
Hahaha, yaleyale ya Lowassa kukubaliana na mshindi wa CCM.Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Tanzania na kada wa chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa miongo mingi Bernard Membe anasema ikiwa Vyama vya Upinzani vitaungana na kumpa ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais, basi atakuwa tayari kupambana na Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba mwaka huu.
Membe amesifia sehemu ya utendaji kazi wa Magufuli, lakini ameyataja baadhi ya mambo ambayo anasema ikiwa hayatabadilishwa, basi yataitumbukiza nchi matatani. Katika mahojiano haya maalum na mwandishi wa BBC Sammy Awami kutoka nyumbani kwake, katika kijiji alichozaliwa Membe alianza kwa kutoa tathmini ya uongozi wa Rais Magufuli.
Chanzo: BBC