Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Nitagombea Urais Upinzani ukinipa ridhaa

Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Nitagombea Urais Upinzani ukinipa ridhaa

Membe ni nani hasa wakutoa sharti? Hapo ndipo upinzania unapohidharaulisha. Lowassa alikuja na sharti la kuwa mgombea urais akapewa nafasi akachomoka na nguvu ya Chadema ambayo ilianza kuonekana dhahiri

Huyu naye anakuja na sharti jingine kwamba ni wapinzani waungane kwanza labda tujiulize hao wapinzania anaowataka waungane ni kina nani hasa?

ACT WAZALENDO, CHADEMA, TLP, TADEA, CHAUMA, NCCR MAGEUZI au upinzania gani hasa?

ACT WAZALENDO wanaweza kuwa tayari kuunganisha nguvu na CHADEMA lakini so kinyume chake. Tayari Katibu Mkuu Be. John Mnyika alishasema wao wanakikaribisha chama chochote kushirikiana nao na sio wao kushirikiana na chama chochote.

Wasalaam

Hata wangetaka kuungana, hilo kwa sasa haliwezekani maana muda wa kisheria umeshapita.
 
Nitashangaa sana endapo upinzani watamchukua Membe kama mgombea wao. Watakua hawakomi hawa. Wanasahau kuwa Membe ni shushushu mbobevu.
 
Siasa za bongo bwana" Nyumba ajenge Mbowe kuhamia ahamie Membe"
 
Eti vyama vikiungana kumpitisha atagombea, Chadema ingieni tena kwenye huu mtego halafu mtakipata fresh
 
CCM hawaminiki,,,mkijua Lowasa yupo wapi basi hamtafanya kosa tena,,Lissu Anatosha ,,,,Kama upinzani WA Nchi hii unategema Makapi ya CCM ndo yawe presidential material of all time basi tutasubiri Sana!.
 
Hapa nakuunga mkono kwa asilimia mia moja. Haiwezekani mtu akae kwenye chama chake muda wote, kisha akikosa nafasi ndio aje upinzani, halafu atake nafasi ya juu. Wakati huo huo wapinzani tukiwa hatujasahau maumivu ya Lowassa, na wabunge wengine waliokuwa ccm kabla ya uchaguzi 2015, na walipopata ubunge kupitia upinzani, wakaribuniwa warudi ccm kwa gharama za kuuchafua upinzani. Tulipofikia panatosha.
Nilikuwa na mawazo haya 2015 na niliwachukia Sana Cdm na Lowasa na nilimpigia Magu kura lakini sasa naona nilikosea Sana.
Swala kuu 2015 lilikuwa mabadiliko ina maana tumeridhika? Nadhani issue ni kumchallenge Magu ambaye ameshajisahau sana tofauti na wakati anapiga kampeni 2015.
Kwa hiyo ni muhimu kumtumia mtu yeyote mwenye uwezo wa kuthubutu kung'oa huyu jamaa.
Kuna wale wanasema Lowasa alipandikizwa!!! Ina maana Lowasa alikuwa hautaki urais? Lowasa alikuwa serious kuchukua nchi. Kama ni makosa ya kumpokea Lowasa yalishafanyika hata kumkataa Membe haitasaidia.
 
Magu lazima awe challenged .
2015 alisimama kunadi ilani ya ccm na akashinda Hawa watu wote waliopotea na akina Lisu ni kwa kiasi gani walikuwa wanamnyima kutekeleza aliyoyaahidi?
Nchi hii tuna mifumo mtu akikosea tuna mahakama kwa Nini uumize watu kwa kudhani tu kwamba wametumwa na mabeberu.
Kama wanankosea tuna mahakama. Mimi hiki kitu Cha watu kupotea kimeniuma Sana. Huwa najaribu kukaa kwenye nafasi ya walioumia nasononeka Sana.
Lazima tujenge siasa za kujali utu hivi vitu tunavyojitamba vimefanyika havina dhamani ya Maisha ya watu.
 
Nilikuwa na mawazo haya 2015 na niliwachukia Sana Cdm na Lowasa na nilimpigia Magu kura lakini sasa naona nilikosea Sana.
Swala kuu 2015 lilikuwa mabadiliko ina maana tumeridhika? Nadhani issue ni kumchallenge Magu ambaye ameshajisahau sana tofauti na wakati anapiga kampeni 2015.
Kwa hiyo ni muhimu kumtumia mtu yeyote mwenye uwezo wa kuthubutu kung'oa huyu jamaa.
Kuna wale wanasema Lowasa alipandikizwa!!! Ina maana Lowasa alikuwa hautaki urais? Lowasa alikuwa serious kuchukua nchi. Kama ni makosa ya kumpokea Lowasa yalishafanyika hata kumkataa Membe haitasaidia.

Mkuu hakuna anayemkataa Membe kuja upinzani, ila aende TADEA achukue fomu. Hayo mambo ya wanaccm kusubiri miezi mitatu kabla ya uchaguzi kisha kuingia upinzani, na wao kutaka kugombea urais sisi sio wapinzani wajinga wa hivyo. Huyo Membe adai tume ya uchaguzi kwa nguvu zake zote, ila sio kutaka kugombea urais.
 
Hakika. Umenena maneno ya upako.
 
Mkuu hakuna anayemkataa Membe kuja upinzani, ila aende TADEA achukue fomu. Hayo mambo ya wanaccm kusubiri miezi mitatu kabla ya uchaguzi kisha kuingia upinzani, na wao kutaka kugombea urais sisi sio wapinzani wajinga wa hivyo. Huyo Membe adai tume ya uchaguzi kwa nguvu zake zote, ila sio kutaka kugombea urais.
Tatizo hawataki kujitolea lakini ni upi uamuzi sahihi kwa awakati huu?
2015 ilibaki kidogo hii nchi ikombolewe japo Lowasa alipokewa kimakosa lakini ukombozi ni ukombozi.
Kwakweli Hawa wazee uzalendo hawana kabisa hawataki kujitolea hata kwa kuwa washauri wa kuweka mikakati.
 
Akiulizwa swali la kichokozi na muandishi wa BBC Ndugu Benard ameeleza wazi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu anayo haki ya kuamrisha vyombo vya ulinzi na Usalama ,kuelekeza na kuvitaka vifanye nini.
 
Back
Top Bottom