Bernard Membe: Sitaomba msamaha!

Bernard Membe: Sitaomba msamaha!

Unajuwa Mh wetu kuna mambo alipaswa yapotezea Ila kwa hili naona kama ni hatari sana Membe kuna kitu anajuwa nauwenda kinamuuma sana sote atujuwi. Ila ugumu unakuja nani wakumvika paka kengele? Hujipendi? Nakama ukimgusa hauwez tikisa Nchi? ,,nani wako nyuma yake na wana agenda gani? Je ukigusanisha moto na milipuko haviwez tokea?

Hamna lolote, usitake kumpamba wakati hana lolote. Jeuri yake ilikuwa wakati yuko madarakani akaishia kuchezea katiba ya wananchi. Saa hii analambishwa mchanga tu. Yaani hapo alipo hana tofauti na binti wa kazi toka Tukuyu? Hata huyu Magufuli anayeonekana leo mwenye nguvu na asiyetishiwa lolote, ngoja atoke madarakani uone kama atakuwa na lolote la maana.
 
Ni Upuuzi tu kumuomba, Kumpigia magoti binadamu mwenzio badala ya Mungu
.

Eti unaomba msamaha kwa mtu anaye vuna dhambi kila siku na kufanya maovu?

Wakina Lissu na watu waliopotea akiwa Rais mbona yeye ajaomba msamaha?

Kamwe hata mimi siwezi kuomba msamaha kwa kumsema mtu kwamba anaongoza nchi ovyo tena kwenye simu eti kisa nimesema mshamba kwani ushamba ni tusi?

Wasio na pakushika tu na mafisadi ndio wanaweza kujikomba kama walivyofanya Kinana, Makamba, Ngeleja na Nape.

Akwillina, Azory, Ben Saanane, Mawazo, Lwejabe na wengine hata kama familia zao hazijaombwa msamaha.

R. I. P.
Upinzani umekufanye usifikilishe akili yako hata kidogo. Hivyo lolote linalosemwa kuhusu kuiponda ccm unlichukua kama lilivyosemwa. Kama una umri mkubwa kidogo (25+ years) kwa kipindi hicho cha miaka kama mitano iliyopita ungewa kufikilia kuwa wafuatao walikuwa ni wanachama wa CCM?
1. Katibu mkuu wa ccm
2. Katibu mwenezi wa ccm (polepole)
3. Waziri wa elimu (Ndalichako)
4. Mkurugenzi TBC (Ryoba)
5. Waziri wa maji (Kitila mkumbo)
6. RC kilimanjaro (Anna Mghwila)

Kwa hiyo hizo kauli za Membe wala usizishabikie. Elewa ccm wana watu waliyosomea siasa hivyo wanao uwezo mkubwa wa kukuaminisha ndivyo sivyo. Shughulisha ubongo wako kijana acha kutumia wanasiasa kufikiria badala yako.

Tena unamkuta mtu mzima na meno 32 ndani ya kinywa chake, bila ya aibu anasema eti binti Karume (shangazi) na binti Salungi eti ni wana harakati!! Fikra finyu sana. Hivi kwa wadhifa wa family ya Karume huyo binti Karume ingeshindikana nini kupewa ajila yoyote anayoitaka serikalini? Au hata huyo binti Sarungi? Hao watu wawili kuna maudhi gani wamefanyiwa na serikali ya chama cha nyumbani kwao (CCM) hadi waichukie?

Kwa akili za aina hii CCM itatawala zaidi ya miaka 100.
 
Mwamba wa Kusini amenena moja kwa moja kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Kuna maswali?



View attachment 1470338

Atasifiwa na vijana wa chadema, lakini mambo yakienda vibaya hawatamsaidia hata mchango tu, yeye aendelee kukomaa kama makamanda, ipo siku masikio yatazibuka ila muda utakuwa umeisha, inabaki historia tu kuwa alikuwa mbishi kwa viongozi wake wa chama.
 
Hata Msigwa alikuwa na mbwembwe kama hizi za Membe, nadhani unajua kilichotokea.
. Huwa tunawaonya kila siku msiwaamini wanasiasa aina ya Membe.
Wanaume kama nyie ndio mliojazana Bongo mnapenda sana kulamba miguu ya wanaume wenzenu "ndio mzee" nyingi na kusaka vyeo wakati Watanzania wanaangamia kwa utawala mbovu wa kiharamia na usikute ww ni kijana kabisa lkn unatetea uonevu.
 
Safi sana kachero mbobevu..songa mbele hvyo hvyo...yaan mtoto wa mjini kama ww umpigie magoti mzirankende??? kausha tu
 
Wanaume kama nyie ndio mliojazana Bongo mnapenda sana kulamba miguu ya wanaume wenzenu "ndio mzee" nyingi na kusaka vyeo wakati Watanzania wanaangamia kwa utawala mbovu wa kiharamia na usikute ww ni kijana kabisa lkn unatetea uonevu.
Maisha yanaangamiaje?

Unafikiri utaona hela kama kila siku umashinda hapa jf?

Ukute hapo kipinde kile Msigwa anamdindishia Kinana ulikuwa unashangilia sana, na juzi alipoomba msamaha ukajiona bwege tu, ila ndio utafanyaje saaa
 
kwenye kikao cha saa saba mchana siku ya mchakato wa kuteua majina ya uraisi july 2015 kuna makubaliano yalifanyika kuwa jpm atawale miaka mitano halafu amwachie membe!!!sasa naona jpm kagoma anataka atawale hadi pale moyo wake wa betri utakaposimama ndio uwe mwisho wa utawala wake!!!tusubiri tuone!!!
Una hasira sana!.

Kwani wewe unategemea Magufuli? Si unategemea Lisu ndio awe rais au?
 
NJIA SAHIHI MBALIMBALI ZITUMIKAZO KUOMBA MSAMAHA

Kuna njia nyingi ambazo mtu abayejua kuwa amekosea au ametenda dhambi anaweza kuzitumia anapoamua kutaka kuomba msamaha...

Njia hizo ni:-

I. Tambua kuwa umemkosea Mungu na Mwanadamu, Hivyo anza kuomba msamaha kwa Mungu kwanza kisha nenda kwa mtu uliyemkosea.

II. Kujutia makosa na kulia mbele ya uliyemkosea ambaye ni Mungu na mwanadamu. Machozi hugusa na huonyesha uchungu wa mtu.


III. Yamkini si rahisi Wewe mwenyewe kuomba msamaha hivyo hauna budi kuwaomba watu au mtu kukuombea msamaha kwa uliyemkosea.

IV. Kumshawishi kwanza mtu yule uliyemtendea kosa. Kwa mfano Kumnunulia Zawadi, kumsaidia kitu, Kujipendekeza kwake, ili iwe rahisi kumuomba msamaha.

V. Kumrudia rudia mtu yule unayemuomba msamaha ili akusamehe ikiwa utaona hajakusamehe, huwezi jua kama anakupima kama ulimaanisha kuja kwake kumuomba msamaha?

VI. Kusujudu au kupiga magoti mbele ya yule uliye mkosea. Hii pia huonyesha kujutia makosa na unyenyekevu kwa uliyemkosea.

VII. Kumuandikia barua au ujumbe wa kumuomba msamaha uliye mkosea ikiwa itaonekana ni vigumu kuonana naye. Japo msamaha wa ana kwa ana unafaa zaidi.

Tambua kuwa unaweza tumia njia zaidi ya moja wakati wa kuomba msamaha ili kutimiza kusudi lako la kusamehewa. Tambua kuwa unaweza kuja kuomba msamaha halafu ukashindwa kusamehewa kwa sababu ya kutumia njia mbaya ya uombaji msamaha, mfano kauli au maneno yako yanaweza kukusaidia usamahewe au yasikusaidie na kukufanya usisamehewe.

Hivyo uwe makini sana wakati wa kuomba msamaha.
 
Back
Top Bottom