Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Tunafanyaje Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi na Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa?

madai ya tume huru yameanza 2020 kakaribia uchaguzi? kama member wa JF anakuwa hivi namna hii,hoko nje kukoje
Yani ndio mnakumbuka tume huru leo na huyo Membe wenu?
Mlipokuwa busy kuanzisha mijadala ya kijinga kama vile rais hajui kingereza, Bashite, tetemeko la kagera na upuuzi mwingine kama huo tuliwaambia huo muda mngeutumia kudai tume huru.
Ona sasa siku hizi mko busy na kigogo eti anatoa siri za Magufuli! Upumbavu mtupu. Na msipoangalia huyo Membe ndio mgombea wenu mwaka huu!

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Jecha alifuta, matokeo na Maalim alisusia uchaguzi na hakuna lililobadilika.. Shein amepiga miaka yake mitano saafi kabisa.. Ukisusa wenzio wala na hakitafanyika kitu.
Hapo ndio ushauri wa Bagonza kuwa sabasaba hii tuandamane kupeleka ujumbe kuwa tunataka tume huru ya uchaguzi unapoonekana wa maana.
Pengine hayo ni maono
 
Na ufe tu, upinzani gani wa kudai tume huru ukikaribia uchaguzi, kwa nini hawakudai tangu mwanzo? wameshaona mambo yanaenda kombo wanatafuta njia ya kutokushiriki uchanguzi.
Pole haki ya kudai tume huru ni ya msingi, unaposhindana na mgombea ambae pia ni refa, kibendera, kamisaa .........
 
Maswali kajiuliza mwenyewe na kutoa mwenyewe majibu sahihi - kwa wakati ule na SASA! Suala la Waangalizi au Watazamaji wa Kimataifa, WAJE TU, hakuna aliyewazuia. Kama wanaogopa kitu ambacho hakipo, COVID - 19, hiyo ni shauri yao. Na woga huowalionao hao Watazamaji wa Uchaguzi wa Nje, wanapewa na watu kama akina Membe na akina Zitto kwa nia na lengo la kutaka kuonyesha kuwa hali si shwari hivyo Uchaguzi wa 2020 hauwezi kufanyika hapa nchini! Huo ni uongo na uzushi usio na mashiko. Anayetaka kuja kuangalia MWEREKA na MWISHO wa wapinzani aje aone; awasiliane tu na mamlaka husika ili apate vibali na aje ashuhudie MBWAGO wa vipenzi na vibaraka wao. Nawasilisha.
 
Wanaodai Tume huru ya Uchaguzi wataje mapungufu yaliyomo kwenye Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT (1977) na kuyafafanua. Isitoshe wanaodai Tume huru walikuwa wabunge, hivyo basi wangeweza kujenga hoja ya kurekebisha vifungu vya Ibara hiyo vinavyoinyima Tume uhuru wa kutekeleza majukumu yake.
 
And this Guy want to be the leader of the free Country
 
Pamoja na suala la kutokuwa na tume huru ya uchaguzi linachomakama pasi, Membe anatakiwa atulie maana alishiriki 100% kuchakachua bunge la katiba ambalo lingetupatia tume huru ya uchaguzi
 
Wala Membe asijaribu kuongelea tume huru. Tume huru ilihitajika muda mrefu. Wakati akiwa serkalini hakuiongelea, maana ilimpa nafuu. Sasa kaondoka CCM inakuwa na umuhimu. Huyo Membe ni muongo na mnafiki wa kutupwa. Alikuwa anaenda nje, akikutana na diaspora anawadanganya atapeleka mswaada bungeni wa uraia pacha. Akifika TZ hahangaiki, mpaka alitoka madarakani bila kuwafanyia diaspora chochote. Sitashangaa akianza kujinadi kuwa alishughulikia na kufanikiwa lakini Maghufuli akakataa!
 
Ukweli ni kuwa siasa ni ajira, kwa hiyo kila mgombea awe upinzani au ccm anafanyia tumbo lake na familia yake.
 
Huyu jamaa anachowaza ni kuwa wabongo hatuwezi inabidi tuwe na wasimamizi wa nje, very poor mindset
 
Wapinzani hawapo kwa ajili ya matumbo yako Mbona CCM kutwa kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwahujumu kwa kila Mbinu na sasa wakurugenziccm wanatembea na matokeo mifukoni ikifika siku ya kutangaza watawatangaza washindi feki wasio chaguo la wapiga kura, Nchi inaelekea kuongozwa na wabunge chaguo la wakurugenziccm siyo chaguo la wananchi.
 
Mda uliopo ni mwingi unatosha kuunda tume huru ya uchaguzi na kutodai zamani siyo kigezo cha kutodai sasa
 
Wapinzani wa kweli wapo wengi ndiyo maana kutwa CCM huwabambikia kesi kuwapiga risasi wapinzani, upinzani ungekuwa haupo kweli usingekuta CCM inaingia gharama kubwa kuwadhoofisha kwa kila hali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…