Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo

Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo

Huyu Mali zake ziuzwe, ikishindikana kulipa deni, akawe civil prisoner. Membe anapeleka application for execution mahakamani, pamoja na njia nyingine za execution, anaomba kumfunga, mahakama inasikiliza, inakubali, inawasiliana na magareza, magereza wanatoa rates za kumuhudumia mfungwa kwa siku, membe anatia mzigo kwenye akaunti za magereza, musiba anaingizwa stoo. Kwa mujibu wa CPC, miezi sita, na anaweza kulimwa sita mingine.

Kwa kuwa ana Mali, hawezi kupeleka maombi ya kutangazwa amefilisika under the Bankruptcy Act mpaka Mali zote zikaushwe
 
Wanabodi,

Huu ni wito wangu na ushauri wangu wa bure kwa Bernard Membe, asibishane na Maaskofu, amsamehe tuu huyu mwana fani mwenzetu, wakati alipofanya makosa yale, hakuwa yeye, alikuwa ni possessed na demons hivyo kuwa kama kichaa
Mkuu Paskali
NInaona kama Membe anashinikizwa na siyo kushauriwa kupitia hoja yako.

Unaposema asipowatii maaskofu yatamkuta...... je kusamehe ni Lazima au Hiyari ya mtu?

Marehemu baba yangu alinkusia kuwa, ukipewa ushauri una hiyari ya kuupokea na kuutumia ama kuukataa. Lakini kama ushauri huo unashinikizwa sana uufuate ni wazi kuna mushkeli kwenye ushauri huo....
 
Wanabodi,

Huu ni wito wangu na ushauri wangu wa bure kwa Bernard Membe, asibishane na Maaskofu, amsamehe tuu huyu mwana fani m

Paskali
Kweli kabisa. Pia wanasiasa wanatakiwa wavumiliane na kusamehana, na kutokukumbuka yaliyopita ili viongozi wajao wasiwe watu wa visasi na kukomoana. Maana ikiendelea hivi TANZANIA kila kiongozi akiingia atakuwa mtu wa visasi, hivyo hatutoimarika Bali ni kurudi nyuma kimaendeleo na kimtazamo.

MH. BERNAD MEMBE ni kiongozi mstaafu mkubwa sana na kio kwenye jamii, hivyo anatakiwa kuachana nalo hili ili iwe Mfano Kwa wengine wanaopenda visasi. Maana sasa uongozi TANZANIA hatujui mtawala ajae atakuwa na visasi na nani? Na je atakuja na mtazamo Gani?

Ni fumbo kwakweli. MH. BERNAD MEMBE ACHANA NA HILI, SAMEHE NA UTAKUWA UMEWEKA MFANO MKUBWA KWA JAMII NA VIONGOZI WALIOPO NA WAJAO KWA UJUMLA.
 
Membe usisikikilize wahuni,wakati huyu Musiba anaporomosha matusi, vitisho na kashfa kwa viongozi wa CCM na wale wa upinzani hawa wahuni walikuwa wapi kumkemea na kumuonya mhuni mwenzao? Membe kataa wahuni huyo musiba lazima awajibishwe kwa ufedhuli wake,wahuni siyo watu.
 
Mbona hao maaskofu hawakumshauri wakati anatoa matusi.
Membe hakuna kusamehe kazia hapo hapo au maaskofu wako upande wake hawafai kuwa wasuluhishi maana anayesuluhisha hastahili kuwa na upande
Ni unafiki na woga wa kidunia bila kumuogopa Mungu

Kama wanamuogopa Mungu na kujua makosa Yale yalikuwa yanatendeka na wakamuogopa Rais basi

Unafiki mbaya sana
Kama unasimamia haki kata kotekote sio upande mmoja
Mkuu una hoja hapo na mimi nakazia
 
Pasco, sio siri kuwa askofu Pengo na Malasusa walikuwa watu wa karibu sana na Magufuli.
Kuna habari (hazina ushahidi) kuwa Musiba alikuwa anatumwa/anamfurahisha Magufuli na utawala wake.
Kiunganishi hiki cha msamaha kati ya marafiki wa JPM na Musiba huoni kinaleta muunganiko mchafu usio pendeza?
Wakati mzee Membe na wenzake wanaambiwa watashughulikiwa hadi makalio yawe makubwa hao unaosema wasikilizwe hawakujua family man Membe anadhalilika kwa uchungu kiasi gani na kumkanya rafiki yao?
 
Pasco, sio siri kuwa askofu Pengo na Malasusa walikuwa watu wa karibu sana na Magufuli.
Kuna habari (hazina ushahidi) kuwa Musiba alikuwa anatumwa/anamfurahisha Magufuli na utawala wake.
Kiunganishi hiki cha msamaha kati ya marafiki wa JPM na Musiba huoni kinaleta muunganiko mchafu usio pendeza?
Wakati mzee Membe na wenzake wanaambiwa watashughulikiwa hadi makalio yawe makubwa hao unaosema wasikilizwe hawakujua family man Membe anadhalilika kwa uchungu kiasi gani na kumkanya rafiki yao?
Well said.
 
Naona ni kama vile Membe yupo katikati, asiposamehe uwezekano wa kulipwa kile kiasi chote cha pesa na Musiba ni mdogo, au awe tayari kulipwa kidogo, unless Membe awe alishafanya uchunguzi juu ya mali anazomiliki Musiba.

Kama Musiba akishindwa kulipa bado itabidi Membe amgaramie Musiba akiwa gerezani, hii yote naiona mitego kwa Membe.
Kumbuka Musiba is a judgment debtor, yaani ni mfungwa mtarajiwa.

Membe ana haki zote, kwenye hili namuunga mkono. Maumivu ya kutakanwa, kuchafuliwa, kufedheshwa ni yeye anayejua.

Hao waomba msamaha wasilikuze hili jambo kwa kusababisha undue pressure kutetea mhalifu/mshenzi Musiba - NO is also an answer.
 
Back
Top Bottom