Wanabodi,
Huu ni wito wangu na ushauri wangu wa bure kwa Bernard Membe, asibishane na Maaskofu, amsamehe tuu huyu mwana fani mwenzetu, wakati alipofanya makosa yale, hakuwa yeye, alikuwa ni possessed na demons hivyo kuwa kama kichaa kabisa! ni shetani alikuwa akimiliki na akimtumia!, hivyo baada ya kuombewa, mapepo yamemtoka, ametambua makosa yake, ametubu, ameomba msamaha, as a human being, anastahili msamaha, hivyo natoa wito kwa Bernard Membe, amsamehe tuu mtu huyu, hakujua atendalo!, Ila maadam ameombewa msamaha na Maaskofu, Membe ukikaidi maaskofu...
Mimeandika haya, baada ya kusoma mahali humu kuhusu
Tetesi: - Membe awakatalia Kardinali Pengo na Askofu Malasusa kumsamehe Musiba.
Duh..., kama mwandishi huyu, ambaye mimi nilimuona kama ni mwandishi kilaza, kanjanja na kichaa kabisa
Kichaa mmoja, anaweweseka sana juu ya Zitto, kamtungia uongo, umebuma, Zitto tuko nae hapa Dodoma, anamiliki mali kama hizo!, then huyu jamaa ni kichwa sana!. Ametuheshimisha sana, hivyo najiunga na Maaskofu, Membe amsamehe tuu!.
Kitendo cha Membe kutowatii maaskofu kitamgharimu sana!. Kuna kiongozi fulani aliwahi kuwadharau maaskofu, najua ni nini kilikuja kumtokea, hivyo sitaki Membe yamkute ya kumkuta!. Amsamehe tuu huyu kichaa, ameishajirudi, akili zimemrudia!, amekubali kosa, ametubu dhambi zake kwa viongozi wake wa dini, wanamuomba Membe amsamehe, Membe asamehe tuu.
Kumuombea msamaha kichaa huyu, hakuna maanishi naunga mkono ule ukichaa wake aliokuwa akiufanya!, no!, namuombea msamaha wa kibinaadamu tuu kwa kutambua udhaifu wa binadamu ni viumbe dhaifu na kuna wakati binadamu tunafanya makosa bila kujijua hivyo kujikuta mtu ametenda kosa bila kujua atendalo.
Kila binadamu anastahili a second chance.
Asamehewe.
Paskalisch