Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo

Kwa hiyo na wewe katika wote waliosemwa na huyo kichaa ya Zitto tu ndio uliona si ya kweli. Ila ya Membe na wengine, uliona ni sawa. Halafu leo wataka Membe amsamehe.
 
Kwani yeye Membe Hoteli anazomiliki alizipata wapi?kabla ya kuwa Waziri alikuwa anafanya Biashara gani zaidi ya kuwa mtumishi wa Umma!.
Ila Musiba utumishi WA umma aliacha muda na kumbukizi zinaonyesha Mali nyingi alipata Kwa kutukana Watu
 
Maaskofu uchwara kamwe hawawezi kuomba dua likakubalika! Hao ni chui waliovaaa ngozi ya kondoo!
 
Paskali, kuwakatalia maaskofu ni tofauti kabisa na kuwadharau. Membe hajawadharau maaskofu amekataa ushauri wao kwa logic ya kutoa fundisho kwa waropokaji ovyo.
 
Kaka paschal Mayalla amani ya bwana ipitayo amani zote itawale.....

Niliwai kua katika state ya kuto msamehe WATU...

Kuhusu musiba nashaur membe asisikilize chochote kutoka Kwa yeyote....
Kuna watu walijifanya wazalendo kuliko neno UZALENDO lenyewe......
Akat musiba anafanya ivyo hakujua ni maumivu mangap aliya sababisha Kwa MEMBE,
Wakati anatumika kama hakujua kua yeye ni sawa na toilet paper.......
Hufutiwa kwenye private party na kutupwa,
Akati anakaza FUVU na kujimwambafy hakua anajua MWACHENI Mali zake zipigwe mnada Ili iwe funzo Kwa vizazi vijavyo.....
 
Hivi Pascal,ulikuwa wapi wakati Musiba anawachafua watu?Pengo alikuwa wapi muda ule?Malasusa je? Ahaa,nimekumbuka!Mlikuwa upande wa mkandamizaji Magufuli.Mlikuwa mnafurahia kwakuwa wakosoaji wa magufuli walikuwa wanawaudhi.Ushauri wako haufai sasa kwakuwa hauzingatii haki ya waliojeruhiwa na Musiba.Halafu wewe na wenzako sii watu sahihi wa kumuombea msamaha kwakuwa hamna tofauti na Msiba
 
Naandika makusudi, bila kujali mada na maudhui yaliyotiririka.

Naamini kuna kesi nyingi kama hizi ambazo hazipewi kipaumbele kama huu uliotokea. Kwamba kesi hii imekaa kiupendeleo. Nipo tayari kusahihishwa.

Je, Kuna mikono na mifuko mirefu kupita mikono ya dola?
 
Nakanusha!! Musiba sio kichaa wala hajawah kua kichaa, usimbambikie ukichaa. Musiba amalizane na kachero nguli na si kusingizia ukichaa!!
 
Unawezaje kuthibitisha hayo mapepo (kama kweli yalikuwa yalikuwepo) yamemtoka na hayatamrudia huko mbeleni ?


Umemuita 'kichaa' halafu ukamwita tena 'kichwa'....Ina maana kuwa 'kichwa' hakukuepushi kuwa 'kichaa' ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…