Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo

Waache hukumu itekelezwa, hata kanisani pamoja na kutubu dhambi huwa kuna malipizi.

Hivyo kwa musiba, utekelezwaji wa hukumu ni malipizi yake.
Hii ili iwe rejea kwa wapuuzi wengine kuwa na staha dhidi ya binadamu wengine.
 
Hao maaskofu waache unafki tusije tukawatukana bure... Walikua wapi kuwaonya au kuwakataza wakat musiba na wapumbavu wenzake wanatukana kudhalilisha kuteka na kujigamba wanaweza kuua watu..?
MEMBE ukikubali kusamehe utakua mpumbavu wa mwisho, malipo ni hapahapa duniani, peponi watu hawaingii kwasabab walisamehe watu waliowafanyia ubaya... Show show
 
Mbona hao maaskofu hawakumshauri wakati anatoa matusi. Membe hakuna kusamehe kazia hapo hapo au maaskofu wako upande wake hawafai kuwa wasuluhishi maana anayesuluhisha hastahili kuwa na upande
Hapana, hauko hivyo na huu wako wala sio ushauri mwema kwa Benard Membe iwapo angekuomba umpe ushauri wa afanye nini...

Ndugu zangu hebu tuelewe kuwa, KUSAMEHE ni tendo la roho (sio la mdomoni) na ni jambo moja (la lazima na muhimu sana) na MTU KUWAJIBIKA KWA MATENDO YAKE iwe ni mazuri au mabaya pamoja na matokeo yake ni jambo jingine kabisa...

Mimi naamini Bernad Membe alishamsamehe Cyprian Musiba na kama ni hivyo, basi huyu (Membe), yeye alishafanya wajibu wake..

Cyprian Musiba kwa upande wake anapaswa kuupokea msamaha huo ili kuiponya roho yake na awajibike kwa matendo yake kwa kulipa fidia ya uharibifu na hasara aliyosababisha kwa watu wengine..

Hata Mungu hutusamehe dhambi lakini haondoi makovu ya matokeo ya matendo na makosa yetu yaliyopita. Tunaishi nayo lakini yakiwa hayana maumivu tena Kwa sbb ya nguvu ya msamaha ule...

Hata Cyprian Musiba anapaswa kufanya Kila analopaswa kufanya kama malipizi ya makosa yake kwa furaha na amani moyoni mwake. Kinyume chake, hataweza kubadilika...!!

Labda tunachoweza kumshauri Bernard Membe ni kukaa na nduguye Cyprian Musiba pamoja ili wajafiliane kupunguza kiwango cha malipizi (faini) ikibidi alipe gharama za kesi tu na mambo yaishie hapo. Na Musiba kama ni mtu wa kujifunza, basi atakuwa amepata fundisho muhimu sana ktk maisha yake...
 
To every action there's an equal and opposite reaction....

#SiempreURT

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Sawa tu, atalishwa wala usiwe na wasiwasi
 
Hapana mkuu kinachompa kiburi Musiba ni hivyo vijisenti vyake sasa dawa ni kuuza hivyo vitegauchumi vyake walau robo tatu akabakiza na robo tu, hapo ndo atatia adabu.
 
Paskali kaishakula chake toka kwa Musiba
 
Naunga mkono mawazo yako, watu kama Musiba ni rahisi sana kuingiza nchi kwenye machafuko sababu ya matumbo yao, Rwanda nao walikuwa hivihivi.
 
Membe alishapeleka malalamiko yake Mahakamani na Mahakama imekuja kuthibitisha kwamba Musiba ni Mkosaji na anahitaji kulipia gharama.[emoji1752][emoji1752]
 
Musiba lazima awajibike kwa matendo yake. Yono tutangazieni tarehe ya mnada wa vikorokoro vya cyprian musiba
 
Asante,atumie jukwaa like lile awaombe kusamehewa na wote aliowachonganisha,aliowatukana,aliowadhalilisha na akitoa mimacho vile vile,na huenda akasamehewa na Allah na malipizi yawe ni kulipa defamations zote.
Yeah hata tukiemdaga kuungama Kuna malipizi yanafanyika.

Musiba alipe hizo Hela kuhusu ataishi vipi atajua mwenyewe.

Kwani aliishi vipi wakati wa mZiLaNkeNdE
 
Nonsense
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…