Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo

unafiki wa kiwango cha rami.
 
Kwani huyo aliwatuma wakamuombee msamaha? au wame amua wao?

Kwakweli hata mimi nisingemsamehe tena ningetafuta fursa ya kuongeza mashtaka dhidi yake.!
Swali la kujiuliza hawakuyasikia wala kuona aliyokuwa akiyafanya?

Je walichukua hatua gani kimuita na kumuonya?

Kama mwenyewe hakuthubutu kumfuata mhusika na kumuomba msamaha wanadhani msamaha atakaopewa utamsaidia nini mbele ya MUUMBA wake?

Ukweli uliowazi HASTAHILI MSAMAHA
 
Safiiiii
 
Hii ni siasa ya kumwombea msamaha mtu mshenzi aliyeumiza wengi. Acha awe fundisho, Membe usifanye kosa chukua haki yako!
 
Sometimes huwa unachemka sana

Unataka kuhakikisha ushenzi aliofanya Musiba?

Huyu bwana Alipe ili iwe fundisho

Tusilee tabia za kishenzi
 
Paskal,

Leo ndio unasema Musiba ni kichaa, basi apelekwe milembe tujue ni kichaa. Kichaa anawezaje kuongea na maaskofu wamwombee msamaha? Mwache apate alichotaka. Na Fatma nasikia ameenda kukazia hukumu yake.
 
Hao maaskofu wasikufanye Membe mjinga, wao wamesamehe wangapi waliowakosea? Usipokuwa makini wenzako watalipwa kipande na Musiba
 
Kuomba asamehewe mtu mwovu, mwenye kiburi, aliyejineemesha kwa kuumiza watu wengine, ambaye kwake pesa zina thamani kuliko uhai wa binadamu wenzake aliohamasisha wauawe, ni kushiriki ushetani wa huyu wakala wa shetani.

Viongozi wa dini nadhani wanamwombea msamaha Musiba kama wao kutokana na mapenzi yao kwaajili yale ambayo Musiba alikuwa akiyatenda, na kwa yule aliyekuwa akimtumia.

Kwenye imani zetu tunaaswa kusamehe lakini kusamehe huko kuna kanuni zake. Siyo kila kitu husanehewa. Ndiyo maaba Muumba wetu, licha ya kuwa mwingi wa msamaha na huruma, lakini hakuwasamehe wafalme wenye viburi bali aliwaangamiza, hakuwasamehe waliokuwa na viburi wakati wa Nuhu, n.k. Kwa hiyo maaskofu wasiwe kichaka cha kuzuia waovu kulipwa sawa na matendo yao.

Kama maaskofu hawa wana dhamira ya kila mhalifu asamehewe bila ya kuwepo mipaka, wamwombe Rais Samia afute magereza yote, majambazi warudi mitaani, wauaji na wevi warudi mtaani, na Rais Samia asipotekeleza ombi la hao maaskofu la kutaka waovu wote wasamehewe na magereza yafutwe, akina Pascal wamhukumu Rais kwa kutotii maelekezo ya Maaskofu kwa vile tumeamua kuwa na nchi ambayo wasemaji wa mwisho katika haki na hukumu wawe maaskofu na siyo mahakama au kitu kingine.
 
Ndugu hawa kinachowasukuma siyo suala la msamaha bali wanajiona wanaguswa na haya yanayompata Musiba, maana na wao kwa namna na kiwango fulani, walikubali kutumika kwa kiasi fulani kama alivyotumika Musiba, japo Musiba alienda mbali zaidi. Kwa hiyo wanachokipigania ni kumkwamua mwenzao kutoka kwenye mkwamo mkali, mwenzao waliyemwona shujaa wao katika kutumika.

Membe hawezi kupatwa na chochote eti kwa kuwa hakuwatii maaskofu ambao nao walitumika wakati watu wakiangamizwa. Hawa maaskofu, ukimwacha Mwamakula aliyesimama kidete kutetea haki, hawa wawili, Malasusa na Pengo, japo ni viongozi wetu lakini hakika wakati wa utawala wa awamu ya 5 walikengeuka na kuamua kusimama na watawala hata pale watu walipokuwa wakiumizwa.
 
Mimi nigekuwa Musiba ningemlipa tu Membe halafu tuone kama ndio ataupata Urais.
Mbona unaleta hoja ambazo hazina uhusiano? Kwani Membe kuupata au kuukosa Urais, kunamtegemea Musiba au wanaomwombea wanamwombea msamaha? Kwanza una uhakika gani kuwa Membe atagombea Urais? Basi na Rais wetu awatoe gerezani wafungwa wote ili aupate Urais kwa sababu asipowatoa hatakuwa Rais!!
 
Nchi inahitaji viongozi wasio na urafiki na uovu. Inahitaji viongozi wanaouchukia uovu kwa matendo na kauli.

Mwalimu Nyerere aliwahi kunena, "tuliweka sheria kali sana dhidi ya wala rushwa, ndiyo maana tukasema kiongozi mla rushwa atachapwa fimbo siku ya kuingia gerezani na siku ya kutoka ili akamwoneshe na mke wake. Tukasikia waziri mmoja amekula rushwa, akaja kuniomba msamaha, nikamkatalia"

Tunataka viongozi wa namna hiyo.
 
Unasema musiba kawaheshimisha kwa kumiliki hizo mali ambazo alijipatia baada ya kudhalilisha watu, siku zote mwisho wa tamaa/ uchawa unajulikana, mnapaswa mjifunze kupitia hili na sio kutia huruma.
Yaani Pascal anaona Musiba amewaheshimisha kwa kuwa na mali alizozipata kama malipo ya kuhamasisha watu wauawe na kuwatukana baadhi ya binadamu wasio na hatia.

Tukiwa na fikra za namna hii ni laana na janga kubwa kwa Taifa. Tutayafurahia hata majambazi yanayotajirika baada ya kupora na kuua watu kwa vile tu kwa kupitia huo uovu, yamekuwa na mali.
 
Hakika naelewa
 
Kuna wakati mtu mmoj alipokuwa amebambikiwa kesi ya uhujumu uchumi, rafiki yake wa karibu, tena mtu maarufu alimwona Waziri mmoja akamwomba amwombe Rais kumtoa yule rafiki yake aliyekuwa ametupwa gerezani na kubambikiwa kesi ya uhujumu uchumi. Yule Waziri akamjibu kuwa yeye hawezi kumwambia Rais kitu chochote kuhusiana na hilo, na hata akimwambia anajua hatasikikizwa. Akamwambia kuwa "kuna watu wawili tu ambao Rais anaweza kuwasikiliza, Kadinali Pengo na mzee Mkapa. Hawa hata wakimpigia simu usiku wa saa 8, atapokea simu zao. Kama mnaweza mkawaone hawa".

Hiyo inaweza kueleza kwa nini leo Pengo anataka Musiba asiadhibiwe kwa uovu alioufanya kwenye utawala wa awamu ya 5.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…