Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Huyu Membe pamoja na kusifiwa au kusifika kuwa ni jasusi mbobezi, lkn alishindwa mission na mzee Lowasa ya kuusambaratisha upinzani nchini kupitia akili kubwa na tamaa ya viongozi wa upinzani. Katika watu waliopewa mission ya kuusambaratisha upinzani toka nchi hii iingie kwenye siasa za vyama vingi, basi Lowasa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa mno tena katika muda muafaka ambao kuna watu walijidanganya kuwa mwenyekiti wa chama tawala wakati huo na mbobezi wa siasa za vizazi vyote mh JK chama kingemfia mkononi. Sasa matokeo yake wao ndio vyama vyao vimewasambaratikia mikononi yan hakuna cha ukawa wala uchawa. Big up mwenyekiti mstaafu mzee JK&Lowasa na pole kwa viongozi wa upinzani. Tamaa ilimponza mbuzi kwa kuwekewa chumvi akijua unga.