Better late than never, CHADEMA anzisheni YouTube Online TV haraka iwezekanavyo


Hata mkianzisha You tube channel lazima mfate sheria na taratibu na pia lazima mpewe leseni na lazima mzingatie miiko ya uandishi wa habari ...mkiruhusu matusi na uchochezi sheria ziko wazi mtapigwa pin kama kawa !

Anzisheni lakini lazima mjue kuwa sheria ziko wazi hakuna mtu wa kirisk chombo chake kisa mropokaji
 
Na ndiyo maana sikumtaja mtu mkuu najua hili linafanyika kwa vyama vyote.

Mwisho wa siku hakuna hoja zinazojengwa kwenye kampeni zaidi ya kuzigeuza kuwa viwanja vya mipasho.

Ni vigumu kutomsema mpinzani wako ila inapokuwa hotuba nzima umeitumia kwa personal attacks matatizo yetu wananchi hayatajadiliwa kamwe.
 
..I totally agree with you.

..idara ya habari na PR ya CDM imedumaa sana.

..hata matukio wanayorusha wanafanya hovyo-hovyo tu.

..Inawezekana hii kazi inafanywa na watu ambao wana majukumu mengine, na hili la kupasha habari wananchi ni ziada.
Plus hizo media zinaweza kuiniza pesa kwenye matangazo ya biashara baada ya kampeni, zinakuwa chanzo cha mapato kwa ajili ya kampeni zijazo na kukuza chama.
Gari zile hazizalishi kihivyo baada ya kampeni ila zitakuwa zinakula pesa za ukarabati tu huku zikiendelea kuchakaa.
Walitakiwa wanunue gari kiasi na pesa nyingine iende kwenye bajeti ya media huko kwenye PR.
 
.....
 
Wanatakiwa na nani au na nini kuwa neutral?

CNN ya Marekani, kwa mfano, ipo neutral?
Demokrasia huambatana na fair access to the media kwa vyama vyote vya siasa.

Nchi kama Tanzania ina media ya taifa ambayo inaendeshwa kwa kodi za wananchi. Je, haitakiwi kuwa neutral ama kutoa fair coverage kwa vyama vyote?!
 
Lissu Ana ilani yake binafsi kwenye kichwa. Na anaamini yeye ni bora na anajua kuliko chadema wote, hakuna anayeweza kumshauri, anatakiwa aeleze sera na aache personal attack. Usitegemee TV ya taifa irushe maneno ya jazba na uchochezi.
Wala lisu hayuko hivyo. Na kama ulimskoa alisema yeye anatama kumuondoa magufuli madarakan sijamsiki akisema wewe fulan mpumbavu, au wewe fulan nitakuchakaza aama wewe mama fulan panua panua panua hadi wapi.

Alisema wazi anataka akishinda atangazwe kuwa kashinda na hata kubali kuonewa je hilo nalo.ni.neno baya?
 
Kazi kupost ela zetu za ruzuku zimenunua Magari [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Yan chadema mnafuraisha sana
Pesa za ruzuku wangewapa Wananchi maana magari si ni vitu, na wao hawataki maendeleo ya vitu.
 
Ipo chadema media TV

Sasa mbona haiko active kurusha matokeo? Hii kutegemea TV za wengine ndio nini wakati wanajua hali iliyopo sio? Kipindi hiki wahakikishe kuwa wanapata coverage kubwa mitandaoni, ndio silaha kubwa kwao.
 
Wanaweza kumuomba mtu anayeishi nje ya nchi kufungua youtube channel. Kisha watu wakawa wanashare link na video. Eg labda iite kampeni 2020. Wakitaka kuruka live huyo mtu aliye nje anaweza kuwapa credentials, au rtmp key, au stream key au restream account wakatumia kiulainiiiiii tu maana sheria haijazungumzia jinsi ya kuzuia youtube channel toka nje ya nchi. Pia sheria haijazungumza lolote juu ya rtmp.
 
Demokrasia huambatana na fair access to the media kwa vyama vyote vya siasa.

Nchi kama Tanzania ina media ya taifa ambayo inaendeshwa kwa kodi za wananchi. Je, haitakiwi kuwa neutral ama kutoa fair coverage kwa vyama vyote?!
Ni kweli.

Sizijui vizuri sheria zetu za vyombo vya habari hususan kuhusu coverage za vyama vya kisiasa.

Kama hakuna, basi kunapaswa kuwepo na ‘equal time rule’ kwa wagombea wote wa vyama.
 
Ushauri mzuri sana, hili ni jambo la msingi sana kuelekea kwenye mapambano ya kudai uhuru.
 
Naam!

Wanachomfanyia Lissu si sawa kabisa.

Sheria ya vyombo vya habari iko wazi mtu akitukana au akavunja sheria wewe ndio utawajibika! Shida ya Lissu atabiriki ndio maana vyombo vya habari vina jikinga ! Mbowe akiongea wanajua fika hakuna shida na hakuna tatizo lolote anaweza wasababishia
 
Huyu millard ayo atafute nchi ya kwenda kuanzia November mwaka huu maana huyu mtoto kazidi. Havumiliki tena
Mnalia kuna udikteta, ona nyie ambao mko ndotoni kama watawala tayari mmeshaanza kutimua watu huko huko ndotoni. Bora usingizi uishe maisha yaendelee.
 
Huo ni ushauri wako
 
Demokrasia huambatana na fair access to the media kwa vyama vyote vya siasa.

Nchi kama Tanzania ina media ya taifa ambayo inaendeshwa kwa kodi za wananchi. Je, haitakiwi kuwa neutral ama kutoa fair coverage kwa vyama vyote?!
Hata chombo cha umma kina taratibu na sheria zinazokiendesha,
Mfano bunge si la chama chochote ukiongea maneno yasiyokubaliana na sheria za huko unaambiwa toa hilo neno.

Kwa sababu lissu hatabiriki ataongea nini, ukiweka live utarrusha mambo mengine sio, so wanaona bora kumrecord kisha wataedit.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…