Betting na michezo yote ya kubahatisha ni mfumo maalumu uliobuniwa ili kuwandaa watu kuwa maskini

Betting na michezo yote ya kubahatisha ni mfumo maalumu uliobuniwa ili kuwandaa watu kuwa maskini

Hyrax

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2023
Posts
964
Reaction score
2,675
Mbali na dhambi kadha wa kadha zinazozalishwa baada ya mtu kuingia katika mfumo huu jambo kubwa na baya zaidi kwa mtu huyu ni kwamba mfumo utamdai UMASKINI in long term hata kama atafanikiwa kubutua hata bilioni 1+ bado mfumo utamdai awe MASKINI

Kama sio uchumi kuporomoka basi atabaki na pesa ila zitamtaka awe maskini kupitia starehe za wanawake, pombe, ulafi na over spending/purchase so baada ya muda depression, magonjwa na mauzauza yatakuua taratibu kuanzia rohoni mpaka mwilini

So kabla hujafa mfumo huu utakudai uwe maskini kwanza kupitia afya yako, uchumi, nafsi na kila kitu kinachokuzunguka. Huu mfumo ni hatari kwasasa duniani kuliko ugonjwa wa ukimwi.

Ngoja niishie hapa.
 
Ukweli mtupu, hii michezo huwa inawapa watu matumaini/illussion kwamba inawapa utajiri,
Na hawa kenge na vile vimashine, vyao wanaviweka maeneo ya watu wa daraja la chini, wanaoamini wakicheza wanaweza kuwa matajiri!
 
Mimi ni mdau mkubwa wa betting uliyobainisha ni kweli tutabisha tu kwa sababu tayari tu waraibu ila uhalisia betting ni hatari sana.

NB: KIEPUKENI KINDEGE NI HATARI MNO NA KWA SASA WANAWAKE WANAONGOZA KUCHEZA KINDEGE(AVIATOR)
images (42).jpeg
 
Screenshot_20250105-165951_Megapari.jpg
Unatafuta hela mdogo tu ya vocha, usibeti kila siku kwa kuweka matarajio makubwa.
 
Anayetoa sadaka kanisani na anayecheza kamari hawana tofauti yoyote.

Anayetoa sadaka kanisani anajua atapata baraka kutoka kwa Mungu, na anayebeti anajua atapata zaidi ya kile anachocheza.
 
Anayetoa sadaka kanisani na anayecheza kamari hawana tofauti yoyote.

Anayetoa sadaka kanisani anajua atapata baraka kutoka kwa Mungu, na anayebeti anajua atapata zaidi ya kile anachocheza.
Hakika,
Ata kumpa mwanamke Hela Ili umtege ni betting mkeka unawza kutiki au kuchanika
 
Back
Top Bottom