Mkweche II
JF-Expert Member
- Aug 11, 2018
- 4,160
- 5,793
sio yangu lakini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mvua ina uhakika, betting sio ya kulinganisha na mvua, "probability"Endelea kubeti kijana utatoboa. Mkulima mbona haachi kulima huku akitegemea mvua ambayo hana uhakika nayo kama itanyesha au la.
Huyu jamaa ana hatari ila kwa kubet direct ana roho ngumu sana.View attachment 2762032
sio yangu lakini
Mvua ina uhakika, betting sio ya kulinganisha na mvua, "probability"
Hahahah sare ya magoli inakuwaga na odds 3 nayo.....Mwaka 2012 mwishoni nilishawishika kuanza kubeti baada ya kushuhudia rafiki yangu aliekuwa akibeti kwa muda mrefu hatimae katandika shilingi laki 4 na elf 30 kwa dau la elf 2 pekee, nilimsindikiza kwenda kuwithdraw na kwa macho yangu niliona akipewa pesa cash taslimu, nilipagawa!
Akaanza kunipa story kuna watu wanaishi mjini kwa kubeti, kuna jamaa alinunua pikipiki kwa kubeti, n.k. nilipata shauku sana nami nianze kubeti.
Akanipa pindi kama lisaa hivi kunielekeza jinis ya kusuka mkeka, aina ya michezo, n.k. na hapa nigusie nimeona siku hizi mambo yamebadilika, hapo zamani ilibidi upewe kwanza darasa ila siku hizi mtu hata asipojua handicap ama double chance ana paste code.
Basi katika kujitafuta ni aina gani ya betting ntajipata, nikaamua niwe nabeti kipindi gani kitakuwa na magoli mengi, first half odds zilikuwa 3.1 kwa mechi, second half ilikuwa 2.1 kwa mechi, sare nimesahau.
Kwa wiki nilikuwa nabeti kama mara 4 hivi, buku kila nikibeti, tangia nilipoanza mpaka 2015 nilitumia takribani shilingi laki 3 na elf 30 pasipo kuambulia chochote, empty, sifuri!
Kama ilivyo hulka ya wanaobeti wengi, sikutaka kuonekana boya, ilibidi niwe nawadanganya wenzangu kwamba napiga napiga elf 60 hadi laki, wenzangu wanaobeti nao walikuwa na tabia hizo hizo tu.
Nilijua hili maana nilikuwa na password zao za mbet na meridian bet kwa watu kama 30 hivi, nikiperuzi history zao zinatia huruma lakini mtu usoni anadanganya kwamba anapiga. Walikuwepo kama watano wanaokula ila ni mara moja moja na nikipiga hesabu walicholiwa kilizidi walichokula.
Ni moja tu niliona anamfilisi Muhindi na alikuwa anaweka mizigo mizito kama elf 50 hivi kwa mechi 2 ama 3, huyu alikuwa mwanafunzi chuoni, muda mwingi alitumia kusuka mikeka, kwa pesa alizotungua kwenye kubeti aliamua kuacha chuo afanye biashara. Nilisika moja ya biashara alijenga banda la kuonyeshea mpira.
Baada ya kuendelea kuambulia vipigo mfululizo nikaona wacha nimuige huyo mwanafunzi niliemuona ana nafuu kwa kuweka mizigo mizito kwa timu chache, kwa bahati mbaya alishaacha chuo na hata password zake alizibadili.
kuna waitaliano niliwahi kuwaona mtandaoni wanatoa sure bets na kweli nikicheki mikeka yao kibao ni ticket won, kuna videos walikuwa wameziweka wateja wao wanawithdraw mpunga waanahesabu noti za kutosha, nilizuzuka na kusema maisha si ndio haya !! kila kazi ina mwenye nayo cha kujitesa nini, wacha niwalipe!
Nililipia elf 60 ya wiki, siku ya kwanza nikaona nisiwe na haraka nicheki kwanza upepo kama watachotabiri kitatiki ili nipate uhakika zaidi, kilichotokea mwisho wa siku matokeo halisi yalikuwa kinyume na walichotabiri, nikaona sio mbaya kuna kukosea nisubiri siku ya pili, ikawa hivyo tena, yani hadi wiki inaisha kila mkeka waliotabiri hakuna uliotiki. Nikaendelea kubeti ule mchezo wangu wa buku buku ila vipigo viliendelea
Nikashawishika kurudi tena kulipia elf 60 ya odds, niliona labda kile kipindi cha kwanza ligi ilikuwa imeanza huenda ndio ilikuwa sababu, nikalipia wiki nikatumia mbinu ile ile nipime kwanza upepo, DUH !! mambo yale yale tu, kila walichotabiri ni kinyume na matokeo halisi.
Nikaja kugundua ni matepeli baada ya kuona mtandao flani waitaliano nao wanalalamika, kumbe uki log out unakuta mikeka iliyochanika inaonekana wameshinda, ukilipia account wanaonyesha kweli wamepigwa ila ni kwa muda uliolipia account, muda wako uliolipia ukiisha unaanza kuona wameanza kupatia, huku bongo nako siku hizi nimeona kuna wahuni huwa wana edit mikeka mechi zikiisha ili iwe chambo wapate uaminifu wa kupiga vichwa.
Baada ya miaka hio miwili na miezi kadhaa niliona betting sio fungu langu nikaiacha kabisa, laki 3 ya kubeti imeenda na laki 1 na 20 ya odds vip imeenda, jumla takribani laki 4 na nusu huko na sijaambulia chochote, damn!
Ila siku zote nachoamini hata kama uliwahi kufeli huwa kuna uzoefu unao wa kukutofautisha na mtu mgeni, Nilichojifunza ni kwamba kama mtu akitaka kufanya betting basi ni vizuri awe anajisukia mikeka kwa kutumia muda kufanya research, kufatilia na kupata uelewa kwa anachobetia, betting haina guarantee ila ukifanya haya walau kuna uwezekano, Siku hizi naona watu wanasubiri code tu.
Samahani mkuu Vipi wewe unaendesha maisha kupitia kamari mkuu?Kuna watu ulaya wana maisha mazuri sana wanaishi kwa kubeti tu. Ni 1%au 2% ya wanaobeti wanapiga ela kila siku. Kwanza inabidi ku control tamaa. Halafu achana na buku kuleta milioni au laki 5, weka mechi moja tu weka mzigo wa kueleweka. Ni rahisi kuweka laki 1 ukapata faida ya elfu 30, kuliko buku kuzaa laki 6. All in all, kama huna kifua achana na kamali. Betting sio ya kila mtu.
Mzigo wote huo unacheza kiboya? njoo nipe jukumu la kukusukia mikeka uone kama hautoboiHahaha... umesema umepoteza laki ngapi vile?! Huku kwenye kubeti hakyamungu tunaugulia maumivu kimya kimya acha tu.
Mechi ya Yanga Na Ihefu msimu ulopita wakati yanga wanakandwa 2:1 na ihefu, niliwaamini wanachi nikawapa 1M. Nikala Lost.
Juzi juzi, tar 2 mwezi huu huu, Napoli Vs Lazio. Nikasema Napoli tena, hapa mbona lazima mtu akae. Nikampa laki8. Kama ilivyo kuwa kwa yanga nae akakandwa 2:1. Nikala Lost
Hizi laki tano tano nimepigwa sana. Hizi laki laki ndo kama mvua. Inshort tangu nianze kubeti nshaliwa si chini ya 8M. Lakini nilizokula mimi sidhan hata kama inafika 1M. Sidhani. Shida yangu naweka stake kubwa halafu kila mara naambulia patupu. Imefika pahala sasa nataka nijitathmini kwanza. Je napaswa kuendelea kubeti au niamini haso zangu tuu!..
Kama uko serious tu seal deal..Mzigo wote huo unacheza kiboya? njoo nipe jukumu la kukusukia mikeka uone kama hautoboi
Basi nenda kalime matikiti halafu ulete mrejesho.Mvua ina uhakika, betting sio ya kulinganisha na mvua, "probability"
Njoo PMKama uko serious tu seal deal..
Mmmmh! Hapa umetuokotakama hujui mfumo wa kubeti acha tu utafilisika
kifupi inatakiwa ubeti mara 100 au zaid ndo uingizwe kwenye mfumo wa kupata angalau kidogo
Direct Win ni noma mkuu muda wwote wanakulaza na viatu😁Huyu jamaa ana hatari ila kwa kubet direct ana roho ngumu sana.