Betting: Niliamua kuacha kubeti baada ya kutumia zaidi ya Tsh. 450,000/- na kuambulia patupu pamoja na kutapeliwa Tsh. 100,000/-. Kuna funzo kubwa

Betting: Niliamua kuacha kubeti baada ya kutumia zaidi ya Tsh. 450,000/- na kuambulia patupu pamoja na kutapeliwa Tsh. 100,000/-. Kuna funzo kubwa

Hahaha... umesema umepoteza laki ngapi vile?! Huku kwenye kubeti hakyamungu tunaugulia maumivu kimya kimya acha tu.

Mechi ya Yanga Na Ihefu msimu ulopita wakati yanga wanakandwa 2:1 na ihefu, niliwaamini wanachi nikawapa 1M. Nikala Lost.

Juzi juzi, tar 2 mwezi huu huu, Napoli Vs Lazio. Nikasema Napoli tena, hapa mbona lazima mtu akae. Nikampa laki8. Kama ilivyo kuwa kwa yanga nae akakandwa 2:1. Nikala Lost

Hizi laki tano tano nimepigwa sana. Hizi laki laki ndo kama mvua. Inshort tangu nianze kubeti nshaliwa si chini ya 8M. Lakini nilizokula mimi sidhan hata kama inafika 1M. Sidhani. Shida yangu naweka stake kubwa halafu kila mara naambulia patupu. Imefika pahala sasa nataka nijitathmini kwanza. Je napaswa kuendelea kubeti au niamini haso zangu tuu!..
Kaaahhhh
 
Kubeti ni bahati tu,sio chanzo cha ajira wala utajiri,mi huwa nabeti 500 kwa funny tu..sijawahi tafta hela ya kula au kodi au bills kwa kutandika mikeka,cos hutaipata kamwe
 
Sio rahisi kiivyo, ukiweka laki kupata elf 30, ukiliwa hio laki inabidi utie laki 4 kwa mpigo ama ubeti kwa laki mara nne kuirudisha ulicholiwa.

Huyo mwanafunzi alieacha chuo alikuwa anacheza hizi na aliweza kuzibutua lakini kusuka mkeka wa timu mbili tu anaweza kukaa masaa, hali hii ilimfanya ashindwe hata kuhudhuria vipindi akaamua kuacha chuo ila uzuri aliacha chuo akiwa na mtaji wa kuanzisha biashara, mtaji huo alipata kwenye kubeti, pesa alizokuwa anapata hakupigia bata alikuwa anatunza (nidhamu ya fedha)
Fedha za kamari,haziji kuzaa kamwe,cos ni hela chafu...hata uwe na nidhamu gani bila kuzisafisha kiroho zitarudi zilikotoka tuu
 
Hahaha... umesema umepoteza laki ngapi vile?! Huku kwenye kubeti hakyamungu tunaugulia maumivu kimya kimya acha tu.

Mechi ya Yanga Na Ihefu msimu ulopita wakati yanga wanakandwa 2:1 na ihefu, niliwaamini wanachi nikawapa 1M. Nikala Lost.

Juzi juzi, tar 2 mwezi huu huu, Napoli Vs Lazio. Nikasema Napoli tena, hapa mbona lazima mtu akae. Nikampa laki8. Kama ilivyo kuwa kwa yanga nae akakandwa 2:1. Nikala Lost

Hizi laki tano tano nimepigwa sana. Hizi laki laki ndo kama mvua. Inshort tangu nianze kubeti nshaliwa si chini ya 8M. Lakini nilizokula mimi sidhan hata kama inafika 1M. Sidhani. Shida yangu naweka stake kubwa halafu kila mara naambulia patupu. Imefika pahala sasa nataka nijitathmini kwanza. Je napaswa kuendelea kubeti au niamini haso zangu tuu!..
Sasa unatakiwa uquite haraka sana.

Itakuwa ngumu jwa siku za mwanzo ipa pambana na hilo zimwi, ni hatari sana kwa uchimi wako.

Kamari hulete UFUKARA.

NB: ufukara ni tofauti na umasikini.
 
Sasa unatakiwa uquite haraka sana.

Itakuwa ngumu jwa siku za mwanzo ipa pambana na hilo zimwi, ni hatari sana kwa uchimi wako.

Kamari hulete UFUKARA.

NB: ufukara ni tofauti na umasikini.
UMASKINI uliopitilizaaaa
 
Kubet ni bahati tu haina mjunzi wala nani na jambo jingine betin, usiifanya kuwa sehemu ya maisha lazima ufeli tu, fanya kuwa burudani, tu, hiyo ni bahati nasibu.
 
Kubet ni bahati tu haina mjunzi wala nani na jambo jingine betin, usiifanya kuwa sehemu ya maisha lazima ufeli tu, fanya kuwa burudani, tu, hiyo ni bahati nasibu.
umesikia lakin betpawa kaliwa b53 vp bado huamin kama betting inautajir a kutosha kuna mzee juz kala m70 ka buku tu
 
Kaka achana na mambo ya ushindi tembea over au under mi cna mtaji tu lakin kupiti jero nakula co kila cku kwa mwez ckosi hela yan juzi hapa nimekosa laki 9 kwa timu 26 nimekosa timi 2
😂😂😂😂 Kwa kujipa moyo tu mko vizuri yani mtu akisoma anaona kama unapiga pesa kumbe unaugulia vipigo tu.
 
Mwaka 2012 mwishoni nilishawishika kuanza kubeti baada ya kushuhudia rafiki yangu aliekuwa akibeti kwa muda mrefu hatimae katandika shilingi laki 4 na elf 30 kwa dau la elf 2 pekee, nilimsindikiza kwenda kuwithdraw na kwa macho yangu niliona akipewa pesa cash taslimu, nilipagawa!

Akaanza kunipa story kuna watu wanaishi mjini kwa kubeti, kuna jamaa alinunua pikipiki kwa kubeti, n.k. nilipata shauku sana nami nianze kubeti.

Akanipa pindi kama lisaa hivi kunielekeza jinis ya kusuka mkeka, aina ya michezo, n.k. na hapa nigusie nimeona siku hizi mambo yamebadilika, hapo zamani ilibidi upewe kwanza darasa ila siku hizi mtu hata asipojua handicap ama double chance ana paste code.

Basi katika kujitafuta ni aina gani ya betting ntajipata, nikaamua niwe nabeti kipindi gani kitakuwa na magoli mengi, first half odds zilikuwa 3.1 kwa mechi, second half ilikuwa 2.1 kwa mechi, sare nimesahau.

Kwa wiki nilikuwa nabeti kama mara 4 hivi, buku kila nikibeti, tangia nilipoanza mpaka 2015 nilitumia takribani shilingi laki 3 na elf 30 pasipo kuambulia chochote, empty, sifuri!

Mara nyingi nikibeti ni timu mbili au moja inachana mkeka, napata matumaini kwamba "Ilibaki kidogo tu ngoja nijaribu tena", huku moyoni nikijipa matumaini "one day yes" lakini kiukeli mkeka ukichanika huwa umechanika haufai hata kama ni timu moja ilichana.

Kama ilivyo hulka ya wanaobeti wengi, sikutaka kuonekana boya, ilibidi niwe nawadanganya wenzangu kwamba napiga napiga elf 60 hadi laki, wenzangu wanaobeti nao walikuwa na tabia hizo hizo tu.

Nilijua hili maana nilikuwa na password zao za mbet na meridian bet kwa watu kama 30 hivi, nikiperuzi history zao zinatia huruma lakini mtu usoni anadanganya kwamba anapiga. Walikuwepo kama watano wanaokula ila ni mara moja moja na nikipiga hesabu walicholiwa kilizidi walichokula.

Ni moja tu niliona anamfilisi Muhindi na alikuwa anaweka mizigo mizito kama elf 50 hivi kwa mechi 2 ama 3, huyu alikuwa mwanafunzi chuoni, muda mwingi alitumia kusuka mikeka, kwa pesa alizotungua kwenye kubeti aliamua kuacha chuo afanye biashara. Nilisika moja ya biashara alijenga banda la kuonyeshea mpira.

Baada ya kuendelea kuambulia vipigo mfululizo nikaona wacha nimuige huyo mwanafunzi niliemuona ana nafuu kwa kuweka mizigo mizito kwa timu chache, kwa bahati mbaya alishaacha chuo na hata password zake alizibadili.

kuna waitaliano niliwahi kuwaona mtandaoni wanatoa sure bets na kweli nikicheki mikeka yao kibao ni ticket won, kuna videos walikuwa wameziweka wateja wao wanawithdraw mpunga waanahesabu noti za kutosha, nilizuzuka na kusema maisha si ndio haya !! kila kazi ina mwenye nayo cha kujitesa nini, wacha niwalipe!

Nililipia elf 60 ya wiki, siku ya kwanza nikaona nisiwe na haraka nicheki kwanza upepo kama watachotabiri kitatiki ili nipate uhakika zaidi, kilichotokea mwisho wa siku matokeo halisi yalikuwa kinyume na walichotabiri, nikaona sio mbaya kuna kukosea nisubiri siku ya pili, ikawa hivyo tena, yani hadi wiki inaisha kila mkeka waliotabiri hakuna uliotiki.

Nikarudi tena kubeti ule mchezo wangu wa buku buku na nilicheza kama mwaka bila mafanikio, mwendo ule ule tu wa timu moja ama mbili zinachana mkeka.

Nikashawishika kurudi tena kulipia elf 60 ya odds, niliona labda kile kipindi cha kwanza ligi ilikuwa imeanza huenda ndio ilikuwa sababu, nikalipia wiki nikatumia mbinu ile ile nipime kwanza upepo, DUH !! mambo yale yale tu, kila walichotabiri ni kinyume na matokeo halisi.

Nikaja kugundua ni matepeli baada ya kuona mtandao flani waitaliano nao wanalalamika, kumbe uki log out unakuta mikeka iliyochanika inaonekana wameshinda, ukilipia account wanaonyesha kweli wamepigwa ila ni kwa muda uliolipia account, muda wako uliolipia ukiisha unaanza kuona wameanza kupatia, huku bongo nako siku hizi nimeona kuna wahuni huwa wana edit mikeka mechi zikiisha ili iwe chambo wapate uaminifu wa kupiga vichwa.

Baada ya miaka hio miwili na miezi kadhaa niliona betting sio fungu langu nikaiacha kabisa, laki 3 ya kubeti imeenda na laki 1 na 20 ya odds vip imeenda, jumla takribani laki 4 na nusu huko na sijaambulia chochote, damn!

Ila siku zote nachoamini hata kama uliwahi kufeli huwa kuna uzoefu unao wa kukutofautisha na mtu mgeni, Nilichojifunza ni kwamba kama mtu akitaka kufanya betting basi ni vizuri awe anajisukia mikeka kwa kutumia muda kufanya research, kufatilia na kupata uelewa kwa anachobetia, betting haina guarantee ila ukifanya haya walau kuna uwezekano, Siku hizi naona watu wanasubiri code tu.
unakulaa hutoiizakaa wanakuachaje
 
Ufanye Downloading Mahela Ukiwa Chumbani Kwako, Ndiyo Tuseme Tumelogwa Kiasi Hiki
 
Masoko uliyokuwa una bet ni magum kushinda mkuu, me binafs nabet ila sitegemei betting ktk maisha yangu.. na sijawahi kuwaza kupata pesa nyingi ktk betting.

Me kwa wiki na bet 5000 tu sizidishi hata 100, me na bet kama ziada tu kupata hela za vocha na vitu vidogo tu. Huwa nakula ila sio pesa nyingi.
mimi na bet mikeka mitatu tu kwa wiki , miwili ya 2000 na mmoja wa 1000 basi.

Ktk mikeka yangu siweki kushinda pesa nyingi, me lengo ni laki moja tu kila wiki ktk hiyo elfu 5 nayoitumia kubet.

Huwa ni mara chache sana mikeka yote mitatu kuchanika , na kila mkeka naoweka sirudii mechi hata 1.

Mnaoliwa na kupigwa sna ni nyie mnaotafuta utajiri au mnaotafuta maisha kwenye beting.

Ushauri wangu betting usiifanye ni ajira au chanzo cha kukutengenezea maisha, na kama huna kazi ni bora usibet.

Ila kama una issue zako unafanya za kukuingzia pesa unaweza kutenga hata 2000 kwa wiki kwa ajili ya muhindi. Usibet mechi nyingi sana , Kama una bet 2000 kwa mkeka mmoja usitake ule laki, mfano 2000 ww tengeneza mkeka wa 20,000 au 30,000 tu.

Watu wengi wana tamaa , kama hauajawahi kubet nakushauri usibet
Aseeee yani unajipa moyo adi raha yani unajiweka kwenye kundi ka wanaopiga kumbe hakuna lolote 😂😂😂 gamblers tunajuana bana adi maandishi
 
Mi nahisi sijaipatia tu machaguo mazuri. Pia nataka niandae mpunga mrefu niongeze rounds. Nikishindwa na hapo, na logoff.
Kwa stake unazoweka Njoo kwenye basketball maumivu utasahau,ngoja Leo nikupe odds za mfano halafu weka 5000 tu
IMG-20231122-WA0002.jpg

.
 
Back
Top Bottom