Betting: Niliamua kuacha kubeti baada ya kutumia zaidi ya Tsh. 450,000/- na kuambulia patupu pamoja na kutapeliwa Tsh. 100,000/-. Kuna funzo kubwa

Mvua ina uhakika, betting sio ya kulinganisha na mvua, "probability"
Hahahah sare ya magoli inakuwaga na odds 3 nayo.....

Hata hivyo mzeebb ulikuwa unacheza maoption magumu....odds 2 single sio kipolepole kutoa na ww ulikuwa unaweka mateam mengi.
 
Samahani mkuu Vipi wewe unaendesha maisha kupitia kamari mkuu?
 
Hahaha... umesema umepoteza laki ngapi vile?! Huku kwenye kubeti hakyamungu tunaugulia maumivu kimya kimya acha tu.

Mechi ya Yanga Na Ihefu msimu ulopita wakati yanga wanakandwa 2:1 na ihefu, niliwaamini wanachi nikawapa 1M. Nikala Lost.

Juzi juzi, tar 2 mwezi huu huu, Napoli Vs Lazio. Nikasema Napoli tena, hapa mbona lazima mtu akae. Nikampa laki8. Kama ilivyo kuwa kwa yanga nae akakandwa 2:1. Nikala Lost

Hizi laki tano tano nimepigwa sana. Hizi laki laki ndo kama mvua. Inshort tangu nianze kubeti nshaliwa si chini ya 8M. Lakini nilizokula mimi sidhan hata kama inafika 1M. Sidhani. Shida yangu naweka stake kubwa halafu kila mara naambulia patupu. Imefika pahala sasa nataka nijitathmini kwanza. Je napaswa kuendelea kubeti au niamini haso zangu tuu!..
 
Mzigo wote huo unacheza kiboya? njoo nipe jukumu la kukusukia mikeka uone kama hautoboi
 

Angalia tarehe hiyo ya jana tu kijana tumemchukua tayari mzungu huyo, tatizo wabet kwa mawazo sana unawaza sana kuhusu pesa yako😁,mpaka leo wajua idadi ya pesa ulioliwa ujue kabisa ulikua wabeti kwa kuwaza pesa yako na presha juu😂,punguza presha uncle njoo nikusuke vizuri tumpasue huyu mzungu wa serbia
 

Acha kulalama, hamna fixed, ila kuna kuotea, alafu betting ni akili, kuliwa kupo, kula kupo. Wewe ulikua mjinga enzi hizo. Betting ukitulia ukiwa na upepo wa machaguzi unakula. Laki nne kelele zote, hiyo tunaliwa masaa mawili tu, na baada ya siku mbili inarudi zaidi au kuliwa nyingine.
 

Attachments

  • A0AE30BE-F1AF-458D-AF4C-39B43EBAF3C3.png
    57.2 KB · Views: 74
  • FE0C571A-28FC-461A-91D8-3D1AA3770469.png
    58.1 KB · Views: 83
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…