Bi. Mtumwa Kitete Muuza Uji na Vitumbua Mchango Wake Ndiyo Ulihitimisha Safari ya Nyerere UNO 1955

Bi. Mtumwa Kitete Muuza Uji na Vitumbua Mchango Wake Ndiyo Ulihitimisha Safari ya Nyerere UNO 1955

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
23,526
Reaction score
34,057
BI. MTUMWA KITETE MAMA MUUZA UJI NA VITUMBUA MCHANGO WAKE SAFARI YA NYERERE UNO 1955

Kuna jambo moja nimewahi kuelezwa na Bi. Mwamvua bint Mrisho maarufu kwa jina la Mama Daisy.

Wakati huu alikuwa akiishi Ali Hassan Mwinyi Road.
Ningependa ulizingatie na ufanye utafiti zaidi.

Bi Mwamvua aliniambia kuwa siku moja wakati mipango ya Mwalimu safari ya kwanza UNO ikikaribia kukamilika kulikuwa na upungufu wa pesa za safari.

Siku moja jioni mabwana watatu wa TANU, walikuja nyumbani kwetu Mtaa wa Stanley kama kawaida yao ifikapo jioni.

Walikuwa na kawaida ya kuja kwa ajili ya kupata chai na kufanya mazungumzo yao mengine.

Mabwana hao ni pamoja na mume wangu Abdulwahid, Mwalimu Nyerere, Dossa Aziz na Hamza Mwapachu.

Hata hivyo ujio wao kwa siku hiyo haukuwa wa kawaida.
Nyuso zao hazikuwa zenye tabasam na bashasha ya kawaida.

Bwana Abdul akaingia chumbani kwetu moja kwa moja.

Nikainuka na kumfuata ndani kama ilivyo ada ya mke na mumewe.

Nilipoingia nikamuliiza,"Je kuna salama Bwana Abdul?"

Akaniambia, "Salama kama si salama.

Kuna tatizo la nauli ya Nyerere kwenda UNO fedha bado hazijatimia."

Bwana Abdul akaniuliza kama nina akiba ya pesa ndani nimkopeshe.

Nikamjibu sina akiba ya pesa ila naweza kuwaelekeza wapi mtaweza kwenda na kupata nyongeza ya pesa.

Bi Mwamvua akamwambia, "Ikiwa utatoka wewe na Dossa,bnendeni New Street kuna bibi mmoja wa Kimanyema, muuza Uji na vitumbua anaitwa Mtumwa Kitete .

Bi Mwamvua anasema nyumba yake ilikuwa mahali ulipotobolewa Mtaa wa Mkunguni na New Street ndipo ilipokuwa nyumba yake akiishi hapo.

Mama Daisy anasema wakatoka Dossa na Abdul wakaenda hadi kwa Bi. Mtumwa wakaingia ndani na kuzumgumza nae.

Akaingia chumbani mwake na kutoka na pesa akawapa.

Bi Mwamvua akasema kuwa ikapendekezwa na wanawake kuwa Nyerere atakaporudi Bi. Mtumwa ndiye atakaemvika kitambi Nyerere akiwa Uwanja wa Ndege.

Mama Daisy anasema ikazuka fitna kubwa ya watu kuhoji kwa nini iwe Bi. Mtumwa Kitete apewe heshima hiyo na si wengine?

Ndipo siri hiyo ya Bi. Mtumwa kutoa fedha nyingi kwa safari ya Nyerere UNO ilipofichuliwa.

Bi Mwamvua anasema yeye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam.

Maneno haya ameyasema mbele yangu nikiwa na mtangazaji mmoja wa Radio Uhuru, Angel Akilimali ,ambaye nilifuatana naye siku hiyo katika kuandaa kipindi cha Bi Mwamvua.

Bi. Mwamvua siku hiyo hiyo, akanipeleka nyumbani kwa mpiga picha wa Ikulu Adarsh Nayar aliyekuwa akiishi jengo hilo alilokuwa akiishi Bi. Mwamvua hapo Upanga.

Mtaa wa Lumumba barabara ilipokuwa inapanuliwa na nyumba zilizoipa mgongo Mnazi Mmoja kuvunjwa nyumba ya Bi. Mtumwa ilikuwa Mtaa wa Mkunguni ilivunjwa ili ipite barabara ya Mkunguni kuelekea Soko Mjinga ikikata barabara ambayo leo inakata Bibi Titi Street.

Bi. Mtumwa akapewa kiwanja Mwananyamala.
(Kama alivyoandika Mpashaji Habari)

1754171209205.png

Bi. Mwamvua bint Mrisho na mumewe Abdulwahid Sykes
 
kumbukumbu njema ,upande huu ulikuwa mstari wa mbele kupigania uhuru kwa rasilimali zao ila hawakula matunda ya nchi
 
kumbukumbu njema ,upande huu ulikuwa mstari wa mbele kupigania uhuru kwa rasilimali zao ila hawakula matunda ya nchi
Mzee wetu unaandika vizuri sana.nikuombe pia uwe unatuwekea na taarifa zao kwasasa kama vile watoto wao au wajukuu zao ni vizuri tukawafahamu na kuwapa heshima zao.binafsi ndio nimeona hilo eneo huwa hulitendei haki.
 
Kabwe...
Nakushukuru kwa kuleta jambo hili.
Nawafahamu baadhi ya watoto wa wazalendo hawa.

Hali zao zitakutoa machozi.

Kueleza jinsi umasikini ulivyowapiga itakuwa sawa na
kuwafedhehesha.
 
Kabwe...
Nakushukuru kwa kuleta jambo hili.
Nawafahamu baadhi ya watoto wa wazalendo hawa.

Hali zao zitakutoa machozi.

Kueleza jinsi umasikini ulivyowapiga itakuwa sawa na
kuwafedhehesha.
Nimekuelewa mzee wangu.pamoja na hayo naimani utafanya jambo.wenzetu bangladesh msumbiji waliweka utaratibu kuthamini familia za wapigania uhuru japo wajanja wachache wametumia vibaya hizo fursa na kuleta vurugu nchini kwao.kwa namna unavyoandika ni kweli kuna familia hazijatendewa haki kwenye hili.
 
Jambo nimeshalifanya nalo ni kulieleza taifa hili historia ya kweli ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Nimekuelewa mzee wangu.pamoja na hayo naimani utafanya jambo.wenzetu bangladesh msumbiji waliweka utaratibu kuthamini familia za wapigania uhuru japo wajanja wachache wametumia vibaya hizo fursa na kuleta vurugu nchini kwao.kwa namna unavyoandika ni kweli kuna familia hazijatendewa haki kwenye hili.
Karibu kila familia iliyokuwepo kabla ya uhuru ilishiriki kwa namna yake kupigania uhuru. Wapo waliotoa michango ya fedha ili kufanikisha yote. Kama kina Nyerere wasingekuwa na sapoti ya wananchi ingekuwa ngumu kupata uhuru. Kwa hiyo tukisema tushukuru familia kadhaa itakuwa kutengeneza tabala lisilo na lazima.
 
Mama...
Itapendeza ikiwa utaandika historia ya ''kila familia'' kwani itasaidia kujifunza yale ambayo hayafahamiki.
 
Back
Top Bottom