Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 41,558
- 64,966
Ni biashara ipi, kwa uwekezaji mdogo usiozidi 100,000 inaweza kukupa faida ya shilingi 5,000 kwa siku?
Ina maana unakuwa unaizungusha ile ile laki ya mwanzo, baada ya kutoa faida; bila kuongeza mtaji mwingine, je ni biashara ipi hiyo?Kama kila siku utakua unaweka 100k aina iyo ya biashara zipo nyingi
Za kuingiza elfu 5 kwa siku ziko nyingi mno ila sasa inategemea mazingira yako ulipo na hobby yako ni nini.Ni biashara ipi, kwa uwekezaji mdogo usiozidi 100,000 inaweza kukupa faida ya shilingi 5,000 kwa siku?
Nimejaribu kutazama mbali kama ifuatavyo:- Uwe na point 100, na kila point ikupatie faida ya 5000 kwa siku. Mapato kwa mwezi yatakuwa= 5000 x 30 x 100 = 15,000,000/=; ndio nafikiria ni biashara ipi inayoweza kuleta hicho kiasi.Za kuingiza elfu 5 kwa siku ziko nyingi mno ila sasa inategemea mazingira yako ulipo na hobby yako ni nini.
Ila kama uko tayari kwa biashara yoyote tu fanya hivi nenda Karume kanunue mashati makali kwa elfu 5 wewe unatembeza mitaani na kwenye sehemu za starehe,anza na mashati 10 kwa elfu 50 hiyo elfu 50 nyingine iliyobaki itakuwa akiba kwa ajili ya mambo ya nauli.
Au kama unaona aibu kushikilia mashati na kutembeza uza kwa njia ya kupost mtandaoni mtu akihitaji unampelekea delivery,baadae biashara ikianza kuleta faida ongezea na viatu pamoja na pensi/suruali.
Biashara ziko nyingi mno ila nimekupa hiyo moja kwa sababu hii ni biashara ya vitu visivyooza wala kuharibika.
Kwenye upande wa vyakula andaa meza kisha ukanunue kuku 5 wa broilers kata vipande vipand ukaange kisha ukauze barabarani karibu na stendi au sehemu yoyote iliyochangamka hasahasa wanakopaki bodaboda utapata faida zaidi ya elfu 10 ukishazoeleka
Hii ya chenji watu ni wabahili, wataenda nyumba za ibada kupata chenji bure.Biashara ya Poor Brain anaiingiza faida elf 10 kila siku kwa mtaji wa laki.
Anauza chenji, katika kila elf 10 ana buku akiuza chenji za laki ana elf kumi anarudi kulala wala hatoki jasho anapeleka tu vituo vya daladala vitatu laki imeisha anarudi home kulala
😂😂😂😂😂 nimecheka sikuwahi kuwaza hiliHii ya chenji watu ni wabahili, wataenda nyumba za ibada kupata chenji bure.
Ebu zitaje mkuu, tuweze kujifunza na kuchukua hatua.Izo biashara za namna hiyo zipo za kutosha mkuu fungua akili yako wekeza
Zitaje mkuu, akili zinatofautianaIzo biashara za namna hiyo zipo za kutosha mkuu fungua akili yako wekeza
Ebu tuwekee mchanganuoAlkasus Mujarab.
Chupa zako 5 tu unaingiza elfu 10 faida buku 6
Siri ya utajiri ni siriEbu tuwekee mchanganuo
Biashara ya Poor Brain anaiingiza faida elf 10 kila siku kwa mtaji wa laki.
Anauza chenji, katika kila elf 10 ana buku akiuza chenji za laki ana elf kumi anarudi kulala wala hatoki jasho anapeleka tu vituo vya daladala vitatu laki imeisha anarudi home kulala
Ukitaka elf 5 unauza za elf 50 tu unarudi kulala 😃
Et akili zinatofautiana🤣Zitaje mkuu, akili zinatofautiana
Chupa za chai na zenyewe ni siriSiri ya utajiri ni siri
siri ni sehemu za siri tuSiri ya utajiri ni siri
Sehemu za siri ni siri kwasababu ni siri ya sirisiri ni sehemu za siri tu
Upo mkoa gani?Ina maana unakuwa unaizungusha ile ile laki ya mwanzo, baada ya kutoa faida; bila kuongeza mtaji mwingine, je ni biashara ipi hiyo?
Natamani wazo lifanyike nchi nzima, ndio maana nimekadiria point ziwe 100Upo mkoa gani?