Biashara gani ndogo kwa uwekezaji mdogo, inaweza kukupa faida ya shilingi 5000 kwa siku?

Biashara gani ndogo kwa uwekezaji mdogo, inaweza kukupa faida ya shilingi 5000 kwa siku?

Za kuingiza elfu 5 kwa siku ziko nyingi mno ila sasa inategemea mazingira yako ulipo na hobby yako ni nini.
Ila kama uko tayari kwa biashara yoyote tu fanya hivi nenda Karume kanunue mashati makali kwa elfu 5 wewe unatembeza mitaani na kwenye sehemu za starehe,anza na mashati 10 kwa elfu 50 hiyo elfu 50 nyingine iliyobaki itakuwa akiba kwa ajili ya mambo ya nauli.
Au kama unaona aibu kushikilia mashati na kutembeza uza kwa njia ya kupost mtandaoni mtu akihitaji unampelekea delivery,baadae biashara ikianza kuleta faida ongezea na viatu pamoja na pensi/suruali.
Biashara ziko nyingi mno ila nimekupa hiyo moja kwa sababu hii ni biashara ya vitu visivyooza wala kuharibika.
Kwenye upande wa vyakula andaa meza kisha ukanunue kuku 5 wa broilers kata vipande vipand ukaange kisha ukauze barabarani karibu na stendi au sehemu yoyote iliyochangamka hasahasa wanakopaki bodaboda utapata faida zaidi ya elfu 10 ukishazoeleka
Kuwa seriously kidogo mkuu...
Naomba nijue jina lako la IG 😃😃😃😃🫵🫵🫵
 
Biashara ya Poor Brain anaiingiza faida elf 10 kila siku kwa mtaji wa laki.

Anauza chenji, katika kila elf 10 ana buku akiuza chenji za laki ana elf kumi anarudi kulala wala hatoki jasho anapeleka tu vituo vya daladala vitatu laki imeisha anarudi home kulala

Ukitaka elf 5 unauza za elf 50 tu unarudi kulala 😃
sahiv zmeanda bei buku kwa mia nane na buku kumbi kwa elfu nane na hazipatikani kirahisi yaani.
 
😂😂😂😂😂🫵🫵🫵🫵🫵 Designer bana haya nielekeze kazi gani unatanya hapo... Twende kazi shuka
CV yangu haielezeki kwa urahisi mkuu imekaa zigzag yaani ni kama malaya wa kazi huwa situlii sehemu moja.
Nafanya kazi za aina mbalimbali na pia najihusisha na biashara za aina mbalimbali.
Haya niambie specifically umevutiwa na kitu gani zaidi unachopenda kufahamu
 
Nafurahi sana mkuu kusikia hivi..
😂😂😂😂😂😂😂 Nikisikiakama kumbe wewe ni multiple talented aiseee nafurahi sana aiseeee oky..

Naomba nambie unachofanya nn cha kufanya uwe busy masaaa 16
 
Kama upo DSM, nenda kanunue Maji Katoni 30 Kwa bei ya shilingi 3,300

Ukiyapoza kwenye fridge utaweza kuuza shilingi 800 Kwa Kila chupa 1

Ambapo ukifanikiwa kuuza Katoni zako 30 utaweza kuingiza shilingi

30x6x800=144,000

Iwapo utakuwa mikoani, shilingi 100,000 utapata Katoni 25

Ukiuza Katoni zote, utapata;
25x6x1,000=150,000
 
Bei hii ni kwa maji yenye lita ngapi?
 
Paka rangi kucha za wanawake safisha miguu yao. Oyaa ni biashara ya ******* lakini inalipa incentives kuona mapaja. Kwenye goli lako weka na chupi za kike na tunguo na tuviatu twa watoto
 
Kauze nguo za watoto na viatu vya watoto nje ya hospitali au kituo cha afya siku za kliniki utafurahi
 
Ni biashara ipi, kwa uwekezaji mdogo usiozidi 100,000 inaweza kukupa faida ya shilingi 5,000 kwa siku?​
1000030871.jpg
Biashara ziko Ziingi tu!
 
Back
Top Bottom