Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Mkuu una madini, uko kwenye hii game nini?
 
Bank labda kama ya babu yake😀😀bank ni profit organisation ipo kumake doh sio kusaidia mtu , fixed account wanalipa pesa ndogo sana
Bank ni wanyonyaji mno bora hata kwenye bond huko
 
Achana na hicho unachokifanya
SCALP
NASDAQ, DW, US30, XAUSD
million 300 ni sawa na dollar 120000 hv
Ukikaza, hiyo million tano unapata kwa siku
Lakini hiyo shughuli yake kwanza, kwanza n'cheke
Kwahio hela kuchoma account forex ni majaliwa😂😂😂 hata akifungua position 10 za gold kwa lot size ya 3
 
hii kitu iliwah kuniliza nikamshikia mtu panga police wakaamulia... 20m zilipotelea makongorosi, kama isingekuwa shule nilikuwa naadhirika...sipapendi chunya daaah
Hapo nina wanangu wana mashimo wanajaza vifusi tu😂😂😂 nataka niende by december nikasome upepo
 
hii kitu iliwah kuniliza nikamshikia mtu panga police wakaamulia... 20m zilipotelea makongorosi, kama isingekuwa shule nilikuwa naadhirika...sipapendi chunya daaah
Kwenye madini watu wengi wanaingizwa mkenge hao wakina ferooz, idris sultan wote hao wamefirisika kwa kuingizwa mkenge, watu mgodi wanaujua vizuri wanakupa kitalu wanachojua utachimba miaka yote hautopata kitu utaishia kuingia costs tu😀😀na utauza kila kitu ukiamini utatusua one day
 
Tuweke mambo sawa, maana naona wajuaji wamekuwa wengi kidogo.
Huu mtaji niliowekeza sio kwamba nimefeli japo mambo yamekuwa kinyume na matarajio yangu.

Lengo langu lilikuwa kuwekeza mtaji zaidi ya huu, huu ndio mwezi wa wangu wa kwanza kwenye biashara naendelea kuona mavuno ya mtaji nilioweka Ili niamue kuongeza mtaji au la.

Nimeshindwa kufunguka zaidi baada ya kuona kuna ujuaji mwingi Tena Kwa watu ambao hata biashara hawaijui. Kila nyuzi wao wanajua ni uongo wa kutunga au chai, wao wakiona nyuzi ya 300m+ wanajua ni story za kusadikika

Anyway tuwe na usiku mwema, na niwaombee muwe na mapambano yenye baraka
 
Mwaga madini mkuu
 
Mjomba biashara gani unafanya? Maana kuna vitu unaficha
 
Yap benk nyingi 100mil kuendelea ni 10% kwa mwaka
Hiyo ilikuwa kitambo kidogo. In the last two years, rate imeshuka kufikia 7-8% only. Nyingi wanacheza na 7.5% kwa mwaka kuanzia investment ya mil 100 kuendelea (CRDB, NMB, etc - fixed deposit). Ila kama huna uzoefu na biashara au huna msimamizi mzuri kwenye biashara, na hiyo pesa huna kazi nayo immediately, hii bonds na fixed deposits ni safe investment
 
nenda mzee kasome ramani....hela yangu ilizama bana sema ntakuja kurudi tu ngoja nijipange...kule kuna makatil na watu wenye roho mbaya biila kukaza hutoboi....na panahitaj hela mingi pia
Jamaa mwenyewe ukimuona kama jambazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…