Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Kila biashara ina returns zake mfano biashara ya spea ama accessories za magari zinalipa nusu kwa nusu. Kwa mwenye mtaji mkubwa hivyo unainjoy maana kila kitu unakua nacho mteja akija hakosi kitu
Hata mil 50 bado faida ndogo sana. Mtu unazungusha mtaji hauzid laki mbili na kila mwezi mtu anakunja faida mil na ushee.
 
Mkuu maelezo yako hayajakamilika hivyo ni ngumu kukushauri.

Biashara ina muda gani?

Una competitors unapofanya biashara?

Kuna maximum usage of resources ulizoweka katika biashara? Eg kama mashine ni zote zinafanya kazi na kadhalika

Business analysis document yako inasemaje kwa hatua uliyopo? Mapato na faida vinaendana na estimates zilizomo katika document kwa level ya biashara uliyopo?

Haya ni baadhi ya maswali ya kujibu ili angalau tujue jinsi ya kukusaidia zaidi.

Kwa perspective pesa unayoingiza inaweza ikawa sahihi kwa situation ya biashara uliyonayo. Japo kwa kuangalia haraka haraka 5 mil kwenye 300 mil si kubwa ila kwa mwaka hiyo ni gross ROI ya 20% kabla ya final expenses ambazo pia hatuzijui kwa sababu haujazieleza. Funguka tukusaidie zaidi.
 
Unayama sana
 
Kinachokusumbua ni kuwaza faida kwa haraka, kwamba wateja watakuja vuup kama uliwapang baada ya biashara wajitokeze. Kurudisha pesa ya biashara inawachukua watu miaka, na inategemea na channel yake ya wateja.
 
Faida ambayo haina stress lakini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…