Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Kwa miaka yote, 15-25 kulingana na mkataba.
 
Kwa watu wenye B au zaidi ni sehemu nzuri ya kupumzishia hela
 
Uzuri wa humu kuna madini mazri sana, ila nachojua ni watu tufanye biashara za faida na tuache utani, mtu mwinginge anauza imradi ashike hella mingimingi
 
[emoji38]Wewe ndo umeongea sasa[emoji1474]. Maisha ndio haya haya pesa tumezikuta tutaziacha
 
Umeona ee. Mpaka unakamata 300 hata akili inakuwa ishakomaa hebu review thread's zake angalia akili yake.
Nadhani utakuwa "ke" kama nimekosea basi naomba uniwie radhi.

300m unaweza kuziona nyingi Kwa vile hauko nazo, ukiwa kwenye chain ya kumiliki pesa utagundua hizo 300m hazitoshi hata kujenga nyumba ya kisasa ya ndoto yako Kwa kipindi hicho

Kwa vile hii ni forum na hatujuani usitoe mawazo ya kijumla kama vile unafahamiana na huyo mtu

Nikuhakikishe tu kwamba hii pesa sio ya mkopo ni sehemu tu ya kiasi nilichoamua kuwekeza kwenye hii biashara mpya ambayo Bado haijatoa return nzuri
 

Ukweli ni kwamba huwezi kutoboa kwenye biashara bila kukwepa kodi/kukandamiza wengine/kufanya ulaghai na/au kupewa exemptions na serikali either by lobbying au illegally. Huu ndo ukweli halisi wa biashara zote duniani hasa kwenye hatua za awali.

Hapo ndo unasikia kuna watu walikua wanaiba mafuta bdae mnasikia wana vituo vya mafuta nchi nzima; wengine wametorosha madini hadi basi bdae ndo wanaanza kusafirisha rasmi, wengine hawalipi kodi nk nk. Ni lazima utafute kwa njia za panya halafu utakatishe hizo pesa. Learn it. Do it. Utatoboa.
 
Big point broh una kitu cha kipekee.
 
Vizuri sana ndugu,pambana hivyo hivyo utakuja kuanza kupata faida zaidi ya hiyo unayopata Sasa, biashara ni uzoefu,maarifa na uvumilivu pia.
Binafsi Kwa hiyo pesa Kwa kutumia maarifa na uzoefu wangu wa biashara mbalimbali,naweza tukafanya biashara Kwa ushirikiano na wewe na tukawa tunapata faida zaidi ya hiyo unayopata,hapo tumeshatoa gharama za uendeshaji wa biashara.Yaani tunapata net profit (faida halisi)sio gross profit(faida ya jumla).
Ukiwa tayari kupanua miradi mingine kupitia biashaara zingine tuwasiliane ndugu.
Kila kitu kitakuwa wazi na utaelewa tunapataje faida japo ya 2% Hadi 5 % Kwa mwezi.
Itategemea na mwezi husika biashara imeendaje ila haitashuka chini ya
2% Kwa mwezi kama faida(hapa uhakika)
Karibuni.
 
Kumbe ndio umeanza. Biashara inakua mkuu. Huwezi kuanza tu halafu mwezi huo huo upate faida kubwa. Tena una bahati kupata hata hio faida ndogo. Muhimu komaa tu utaona matunda yake.
Ni kweli, halafu faida unaanza kuihesabu pale ambapo
Faida bado sana , faida ni pale ambapo atapata m 300 plus hii itachukua zaidi ya miaka 5 kama atakuwa akikusanya 5 m kwa mwezi
 
Hi Ina mzuka sana

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Broo Extrovert umenikumbusha mbali San jinsi unavyodadavua somo la government bond umenikumbusha mwalimu wangu wa financial management nikiwa iaa Arusha pale ticha Yuko nondo mbaya na Uzi na wew umeifa sna ktk Bondi nafurahia mno somo unaloleta humu

Hkk nimeamini humu ndani Kuna watu Bado San hawajui kitu mpk mtu anauuliza bond Ni kitu gani na inafanyaje Kaz duh Kaz kweli ndio maan wanalalamika kila siku kuhusu biashara z mafrehemu na majumba

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Hahahah Elimu ni tatizo sana kwa raia wengi nchini.
 
Nimekuelewa mkuu...

Hapo kwa haraka haraka tunene mawili yaliyo mbele yako... mengine kunapo uzima tuta tafutana kwingineko tutateta kwa upana zaidi.

La kwanza...

Concept ya neno mauzo...
Navyofaham kidogo kuhusu hili ni kua jumla ya mauzo na uwiano wa faida inategemea na aina ya biashara, kuna baadhi ya biashara mauzo yanaweza kua makubwa sana kwa siku, week ama mwezi ila faida ikawa kisoda.

Most ya aina hii ya biashara huwa ni biashara ya bidhaa. Biashara ambayo yakupasa kununua kitu kisha kuuza kitu. Either baada ya kukiongezea thamani au kwa kuki'import sehem ambapo bidhaa huska hazipatikani. Hapa utakuta wanunua bidhaa husika kwa 100 kisha wauza kwa 120.

Na ni aina hii ya biashara ambayo mara nyingi huwa ina mzunguko mkubwa. Ingawa mzunguko mkubwa unategemea mahitaji ya watu walio eneo unalofanyia biashara.

Vile vile biashara inaweza kua na mzunguko kidogo ila ikawa na faida kubwa. Na aina hii ya biashara mara nyingi ni biashara upande wa huduma.

Kwa mfano, kreti la soda linauzwa 9,800/-. Zipo 24. Ukiziuza kwa jero kila moja kreti zima litakupa 12,000/-. Faida ya kama 2,200 hivi kwa kreti. Ili kupata ef 10 nje ya mtaji itakubidi uuze kreti walau 5. Hapa ndipo tunasema mzunguko mkubwa faida kisoda.

Upande wa pili kuna boda boda, safari ya kutoka "X" to "Z" ni 20k, huyu mteja mmoja tu kapata faida zaidi ya mauzo ya kreti tano za soda. Hapa ndipo ilipo ile maana yangu ya mzunguko mdogo ila faida kubwa.

Kwa ufupisho huo kuna picha tunaipata juu ya mahusiano ya mauzo na faida inayopatikana. Kwamba sio kila kwenye wingi wa mauzo kuna faida kubwa au kwenye uchache wa mauzo kuna faida ndogo. Ukubwa au hasa wa faida unategemea unafanya biashara ipi.

Pili tuje hapo unapokosa utulivu...

Hali hiyo nadhani haipo kwako tu, hilo ni janga la kila mtu pale anapokosa udhibiti from within. Kikubwa jaribu ku'control your desire, usiishie kutafuta wingi wa pesa tu maana hauna kikomo ule. Unaweza pata hata trillions dolali ukakosa utulivu kama hauna kiasi kwenye nafsi yako. Bali tafuta wingi wa pesa wenye kukidhi mahitaji ama malengo yako.

Ukiweza ku'control your desire, utauona utulivu unakuijia automatically. Afya yako ina thamani sana. Usiruhusu msongo wa mawazo uitafune na kuiporomoa.

Na kuhusu kama wafanya biashara wakubwa hutunza fedha bank au Laa.

Hapa nikujibu kwa experience kiasi niliyo nayo. Katika jamii ya watafutaji kuna watu wa aina mbili. Traders na Investors. Haya makundi mawili yana character za kipekee kwa kila kundi.

Hilo kundi la kwanza most ndio hujali bank wana kiasi gani. Ila kundi la pili hujali hupendelea kubadilisha fedha kua assets zenye kutunza thamani.

Nakutolea mfano mdogo, bwana 'P' kaweka Mil 500 bank mwaka jana. Alionelea ni better aweke savings za biashara yake katika Euro(huu ni just mfano tu) wakati huo Euro ilikuwa 2800, leo hii anaitaka savings yake ya biashara afanyie mambo mengine.

Lakini anaenda kuichukua akiba yake wakati ambao euro ni 2,400. Drop ya kama 14%. Maana ake ataenda kuchukua Mil 430 approx. Loss ya value karib Mil 70. (Exchange rate figure zinaweza zisiwe hundred percent correct) so hapa grasp the concept tu inatosha.

So kuhusu kua wanatunza fedha bank au laa inategemea na mindset ya mfanya biashara husika. Wengine hupendelea kuona wingi wa cash kwenye account zao. Na wengine ambao hata mie nawapenda zaidi wale ambao huzitumia hizo cash kuongeza assets kwenye biashara zao.

Nisamehe kwa gazeti refu na kama nimekujibu nje ya ulichouliza sorry pia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…