Upo vizuri mkuu nimesoma kila kituo...wewe inaoneka ni mshauri wa biashara.
Mi nina tatizo natamani nilianzishie uzi japo watu watasema ni chai.naomba nishauri hapa hapa
Mkuu mimi biashara yangu nimeanza 2020 mwezi dec ndo mzigo wangu wa kwaza kuingia.
Ki ukweli sijawahi kopa nimekisanya mtaji kidogo kidogo.
Mpaka sasa hivi biashara mtaji wako sio mkubwa ila mzunguko ni mkubwa sana.
Yaani kwa wiki 1M kawaida inategemea na mzigo ulioko dukani.maana miziho inakuja na kuomdoka tatizo langu ni hivi
1.kwa kuwa bado nahitaji kukuza mtaji basi nimekua mtu wa mawazo na usingizi kukata yaani silali.mwanzo hapo kati hata jf nilikua siingii ila sasa hivi naingia kupoteza mawazo..
Yaani nawaza sana kuliko kipindi sina ela.yaani mawazo yangu nikiinza lki nataka laki mbil..yaani siridhiki..sion faida saa ingine
Swali langu hivi kuna siku utafanya biashara ufikie hatua relax kweli au ni mateso tu
2.hivi wafanya biashara wakubwa pesa zao wanaweka bank kwwli?
Nimekuelewa mkuu...
Hapo kwa haraka haraka tunene mawili yaliyo mbele yako... mengine kunapo uzima tuta tafutana kwingineko tutateta kwa upana zaidi.
La kwanza...
Concept ya neno mauzo...
Navyofaham kidogo kuhusu hili ni kua jumla ya mauzo na uwiano wa faida inategemea na aina ya biashara, kuna baadhi ya biashara mauzo yanaweza kua makubwa sana kwa siku, week ama mwezi ila faida ikawa kisoda.
Most ya aina hii ya biashara huwa ni biashara ya bidhaa. Biashara ambayo yakupasa kununua kitu kisha kuuza kitu. Either baada ya kukiongezea thamani au kwa kuki'import sehem ambapo bidhaa huska hazipatikani. Hapa utakuta wanunua bidhaa husika kwa 100 kisha wauza kwa 120.
Na ni aina hii ya biashara ambayo mara nyingi huwa ina mzunguko mkubwa. Ingawa mzunguko mkubwa unategemea mahitaji ya watu walio eneo unalofanyia biashara.
Vile vile biashara inaweza kua na mzunguko kidogo ila ikawa na faida kubwa. Na aina hii ya biashara mara nyingi ni biashara upande wa huduma.
Kwa mfano, kreti la soda linauzwa 9,800/-. Zipo 24. Ukiziuza kwa jero kila moja kreti zima litakupa 12,000/-. Faida ya kama 2,200 hivi kwa kreti. Ili kupata ef 10 nje ya mtaji itakubidi uuze kreti walau 5. Hapa ndipo tunasema mzunguko mkubwa faida kisoda.
Upande wa pili kuna boda boda, safari ya kutoka "X" to "Z" ni 20k, huyu mteja mmoja tu kapata faida zaidi ya mauzo ya kreti tano za soda. Hapa ndipo ilipo ile maana yangu ya mzunguko mdogo ila faida kubwa.
Kwa ufupisho huo kuna picha tunaipata juu ya mahusiano ya mauzo na faida inayopatikana. Kwamba sio kila kwenye wingi wa mauzo kuna faida kubwa au kwenye uchache wa mauzo kuna faida ndogo. Ukubwa au hasa wa faida unategemea unafanya biashara ipi.
Pili tuje hapo unapokosa utulivu...
Hali hiyo nadhani haipo kwako tu, hilo ni janga la kila mtu pale anapokosa udhibiti from within. Kikubwa jaribu ku'control your desire, usiishie kutafuta wingi wa pesa tu maana hauna kikomo ule. Unaweza pata hata trillions dolali ukakosa utulivu kama hauna kiasi kwenye nafsi yako. Bali tafuta wingi wa pesa wenye kukidhi mahitaji ama malengo yako.
Ukiweza ku'control your desire, utauona utulivu unakuijia automatically. Afya yako ina thamani sana. Usiruhusu msongo wa mawazo uitafune na kuiporomoa.
Na kuhusu kama wafanya biashara wakubwa hutunza fedha bank au Laa.
Hapa nikujibu kwa experience kiasi niliyo nayo. Katika jamii ya watafutaji kuna watu wa aina mbili. Traders na Investors. Haya makundi mawili yana character za kipekee kwa kila kundi.
Hilo kundi la kwanza most ndio hujali bank wana kiasi gani. Ila kundi la pili hujali hupendelea kubadilisha fedha kua assets zenye kutunza thamani.
Nakutolea mfano mdogo, bwana 'P' kaweka Mil 500 bank mwaka jana. Alionelea ni better aweke savings za biashara yake katika Euro(huu ni just mfano tu) wakati huo Euro ilikuwa 2800, leo hii anaitaka savings yake ya biashara afanyie mambo mengine.
Lakini anaenda kuichukua akiba yake wakati ambao euro ni 2,400. Drop ya kama 14%. Maana ake ataenda kuchukua Mil 430 approx. Loss ya value karib Mil 70. (Exchange rate figure zinaweza zisiwe hundred percent correct) so hapa grasp the concept tu inatosha.
So kuhusu kua wanatunza fedha bank au laa inategemea na mindset ya mfanya biashara husika. Wengine hupendelea kuona wingi wa cash kwenye account zao. Na wengine ambao hata mie nawapenda zaidi wale ambao huzitumia hizo cash kuongeza assets kwenye biashara zao.
Nisamehe kwa gazeti refu na kama nimekujibu nje ya ulichouliza sorry pia!