Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Niajiri mimi nikufanyie marketing ila mapenzi sipendagi napenda kazi .
Kama upo serious njoo pm nipo serious .
Hali sio mbaya kwako ila naweza kukusaidia ukapanda kidogo mshaara wangu ni 9 laki tisa
Hutaki mapenzi😲😲😲 y u gotta assume the worst in people?
 
Kuna muda unaweza kuwa kichaa kwenye haya mambo ya biashara.

Nimewekeza Tsh. Million mia tatu(300m+), nimeanza biashara napata return ya 5m yaani million tano kwa mwezi.

Hapo sijatoa mishahara ya wafanyakazi na gharama za kuendeshea ofisi.

Wafanyabiashara mna roho ngumu sana, presha nje nje!
Ningekuwa mimi ningeenda benki kuu ya Tanzania halafu ningenunua treasury bonds za miaka 25.


Kwa hela hiyo hata kama ningenunua za 250m,si hapa ningependa mgao mzuri wa kila nusu mwaka


Kwa 250m,ningepeta gawio zuri la kati ya 25m au 30m kwa mwaka,tena ni tax free,
(kama ntakuwa nimekosea hizo figure nakaribisha masahihisho)

Na baada ya miaka 25,narudishiwa 300m yangu na maisha yanaendelea
 
Ningekuwa mimi ningeenda benki kuu ya Tanzania halafu ningenunua treasury bonds za miaka 25.


Kwa hela hiyo hata kama ningenunua za 250m,si hapa ningependa mgao mzuri wa kila nusu mwaka


Kwa 250m,ningepeta gawio zuri la kati ya 25m au 30m kwa mwaka,tena ni tax free,
(kama ntakuwa nimekosea hizo figure nakaribisha masahihisho)

Na baada ya miaka 25,narudishiwa 300m yangu na maisha yanaendelea
Umeagana na Mungu?
 
Amen amen bro!!


Selfishness is a form of immaturity, we you get to grow, one thing you understand is that maturity is all about helping others. Naamini kila mtu (including me) at a certain point in life alisaidiwa na mwingine, sasa kama watu wote wangebaki selfish na kile walichonacho duh sijui tungekuwa wapi wengine.

It's about 3 years now.


Ntajitahidi kueleza kwa kifupi lkn kwa ufasaha pia;

1. Kota (broker):
Watu wanaanza hata na 1m or even less. How?
Kwa Chunya, maeneo yanayo chimbwa yapo mengi sana na unlike other areas (Kahama,Geita na Nyamongo) mwamba wa Chunya uko very shallow (juu juu) na pia sehemu kubwa ni mwamba laini kiasi kwamba vijana wengi wanaanza na sururu tu kuchimba na kukusanya mawe na hatimaye kuyapeleka kusaga kwny crusher (karasha) na kukamatisha dhahabu.

Sasa kwa vijana km hawa, wewe kota unazama porini kuwafata wanapo chimba na kuongea nao unawawezesha kidogo fedha mfano ya vifaa (sururu nk) au sometimes hela ya chakula kwa makubaliano wakipata mzigo watakuuzia wewe kwa bei flani (ambayo ni ya chini kuliko ya kule soko la broker utapoenda kuuza wewe).

Na huwa ni fedha ndogo tu ya kuwadhamini inaweza isifike ht 100k. Kwa hyo ukipata makundi ya vijana ht matano hv ukawawezesha then ukawa unawabana unapata mzigo (grams kadhaa) na kwenda kuuza soko la broker, inakupa gape zuri la kuanza km kota then baadae ukikua unaweza kujisajili nawe km broker ukawa na ofisi ambapo unaweza kujidhamini kwa ofisi yako ukapewa fedha na dealers (wanunuzi wakubwa) kwa makubaliano ya uwe unawauzia mzigo wako. Hapa ni muhimu uwe na pikipiki kufanya hizi mishe zote.

2. Kuozesha kifusi/rudio/concetrates:
Hapa kuna namna mbili;
a) Uwe unanua kifusi/rudio kwny mialo ya kuoshea dhahabu kwa wale wenye makarasha au
b)Utafute sehemu wanapochimba ufunge karasha ww mwnyw ili ukusanye kifusi/rudio then baadae utaingiza plant kufanya processing kisha elution kuchenjua. Gharama za karasha inacheza kwa ss kati ya 8-9m lkn ukiwa kule field kuna makarasha yamewashinda watu kuyaendesha unaweza pata kwa 3-4.5m na linakuwa kwny hali nzuri sn kufanyia kazi.

Ukianza na ukota utapata connection nying tu sabab unakuwa uko kwny actual field. Utajua wapi kuna mwamba mzuri pa kuchimba/kufunga karasha, utapata kirahisi kujua hayo makarasha yaliowashinda watu nk nk.

Ukiweza kufikia hatua ya kuwa na karasha lako uko kwny hatua nzur sn 'kutoboa'. Kutegemea na sehem ulipolifunga unaweza tumia miezi 4-6 kukuza kifusi cha tani hadi 300. Kwa mfano km rudio lako litasoma 3.5ppm maana yake kwa kila tani 1 unaweza pata hadi gram 3.5 ya gold, kwa tani hzo 300 maana yake (3.5*300tons) = 1050grams = 1.05 kg ya gold ambayo kutegemea na %purity utaweza pata 100m+ km itakuwa 95%+ kwa bei ya ss.
Ofcourse, utatoa gharama za plant, kusomba kifusi hadi plant, madawa na elution. Inaweza fika hafi 30m, so roughly utabaki na 70m flan hiv of which is a handsome amount. Ukifika hatua hii ss ni ww tu kujitanua maana unakuwa na capital ss ya kufanya kazi.

Njia ya kufunga karasha ukifanikiwa ni nyepesi zaidi kwa kuwa linajiendesha lenyewe, hapo wanalipa kila wanapokuja kusaga mawe na pia unaweza kuwa unanunua dhahabu hapo na kwnda kuuza. Cha msingi ulifunge sehem nzuri yenye uzalishaji.
Good analysis
 
Nissan civilian zinalipa sana kwa biashara ya dala dala , wapemba wengi zimewatoa .
Siri kuu ninkuwa tumia nissan kama Big G, ikiisha utamu unatupa!! Usije jaribu kutengemeza nissan.
Lakini sio kwa kununua milioni 50 then utegemee hesabu ya siku elf 80 au laki moja plus service ni juu yako.Hio m 50 itarudi rudi, daladala inalipa kama una vyanzo vingine au ajira,duka la spare,nk.
Coaster mpya inakwenda milioni 70 hadi 80,wengi wamiliki wanazitumia kutakatisha pesa tu au yupo kwenye kamba na hana pa kupeleka pesa. Maana hata kama utalaza laki 1.nusu kwa siku hio M 70 itarudi lini. Wapemba wengi upewa hizo daladala toka kwa ndugu zao nje
 
Milioni 300 ukiamua kuitunza na kutumia kila mwezi 2M maana yake utakula maisha bila stress kwa miaka 20 ijayo. Sijui umri wako ila kama umri pia umeenda, kwa next 20 years maana yake utakuwa umekaribia kumaliza siku zako za kuishi. Kuja pesa ikakata, na wewe siku zako zinakuwa zinaelekea kukata. Yaani hapo ni kula 2M kwa mwezi bila stress za hii dunia. Maisha ya hapa Duniani ni kuchagua tu, maana utajiri hauingii nao kaburini. Kwanini kujipa stress ufe mapema?
Word!!!!
Utajiri hauingii nao kaburini, sasa unatafuta hela w na kujinyima halafu unakufa unaacha bank accounts zinasoma b kadhaa na we wala hukuwai kuonjoi pesa yako!
Mabwashee imewacost sana hii miaka ya nyuma ndomaana siku hizi wamefungulia pombe na umalaya kwa pesa wanazotafuta, .
 
Kwamba ukiwa na milion 300 huwez kushindwa kurun bussines [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Kuna watu Wana Hadi billions Ila hawawezi kurun bussines sembuse milion 300
Na hizo pesa anakuwa kapataje cheef? Kama ni za urithi , za wizi au mkopo sawa.
 
Huyo b love mshamba na ana roho ya kimaskini
Wadogo zangu hebu jiongezeni basi. Hizo m300 au B nk unakuwa umezipataje? Za urithi za wizi au mkopo? Kama ume hustle mwenyewe toka inaitwa laki ikiwa million mara zikawa 10 zikawa 100 unakuwa umeshapitia ups an down nyingi ume solve challenge nyingi na unakuwa ushatengeneza connection kubwa na watu tofauti tofauti wenye vipato na fani tofauti tofauti. kiuhalisia hata ukipata hasara unakaa chini na Moja ktk mtandao wako mnayajenga . So jamaa anatupanga tu ila tulopitia situation hizo tunajua
 
Back
Top Bottom