Amen amen bro!!
Selfishness is a form of immaturity, we you get to grow, one thing you understand is that maturity is all about helping others. Naamini kila mtu (including me) at a certain point in life alisaidiwa na mwingine, sasa kama watu wote wangebaki selfish na kile walichonacho duh sijui tungekuwa wapi wengine.
It's about 3 years now.
Ntajitahidi kueleza kwa kifupi lkn kwa ufasaha pia;
1. Kota (broker):
Watu wanaanza hata na 1m or even less. How?
Kwa Chunya, maeneo yanayo chimbwa yapo mengi sana na unlike other areas (Kahama,Geita na Nyamongo) mwamba wa Chunya uko very shallow (juu juu) na pia sehemu kubwa ni mwamba laini kiasi kwamba vijana wengi wanaanza na sururu tu kuchimba na kukusanya mawe na hatimaye kuyapeleka kusaga kwny crusher (karasha) na kukamatisha dhahabu.
Sasa kwa vijana km hawa, wewe kota unazama porini kuwafata wanapo chimba na kuongea nao unawawezesha kidogo fedha mfano ya vifaa (sururu nk) au sometimes hela ya chakula kwa makubaliano wakipata mzigo watakuuzia wewe kwa bei flani (ambayo ni ya chini kuliko ya kule soko la broker utapoenda kuuza wewe).
Na huwa ni fedha ndogo tu ya kuwadhamini inaweza isifike ht 100k. Kwa hyo ukipata makundi ya vijana ht matano hv ukawawezesha then ukawa unawabana unapata mzigo (grams kadhaa) na kwenda kuuza soko la broker, inakupa gape zuri la kuanza km kota then baadae ukikua unaweza kujisajili nawe km broker ukawa na ofisi ambapo unaweza kujidhamini kwa ofisi yako ukapewa fedha na dealers (wanunuzi wakubwa) kwa makubaliano ya uwe unawauzia mzigo wako. Hapa ni muhimu uwe na pikipiki kufanya hizi mishe zote.
2. Kuozesha kifusi/rudio/concetrates:
Hapa kuna namna mbili;
a) Uwe unanua kifusi/rudio kwny mialo ya kuoshea dhahabu kwa wale wenye makarasha au
b)Utafute sehemu wanapochimba ufunge karasha ww mwnyw ili ukusanye kifusi/rudio then baadae utaingiza plant kufanya processing kisha elution kuchenjua. Gharama za karasha inacheza kwa ss kati ya 8-9m lkn ukiwa kule field kuna makarasha yamewashinda watu kuyaendesha unaweza pata kwa 3-4.5m na linakuwa kwny hali nzuri sn kufanyia kazi.
Ukianza na ukota utapata connection nying tu sabab unakuwa uko kwny actual field. Utajua wapi kuna mwamba mzuri pa kuchimba/kufunga karasha, utapata kirahisi kujua hayo makarasha yaliowashinda watu nk nk.
Ukiweza kufikia hatua ya kuwa na karasha lako uko kwny hatua nzur sn 'kutoboa'. Kutegemea na sehem ulipolifunga unaweza tumia miezi 4-6 kukuza kifusi cha tani hadi 300. Kwa mfano km rudio lako litasoma 3.5ppm maana yake kwa kila tani 1 unaweza pata hadi gram 3.5 ya gold, kwa tani hzo 300 maana yake (3.5*300tons) = 1050grams = 1.05 kg ya gold ambayo kutegemea na %purity utaweza pata 100m+ km itakuwa 95%+ kwa bei ya ss.
Ofcourse, utatoa gharama za plant, kusomba kifusi hadi plant, madawa na elution. Inaweza fika hafi 30m, so roughly utabaki na 70m flan hiv of which is a handsome amount. Ukifika hatua hii ss ni ww tu kujitanua maana unakuwa na capital ss ya kufanya kazi.
Njia ya kufunga karasha ukifanikiwa ni nyepesi zaidi kwa kuwa linajiendesha lenyewe, hapo wanalipa kila wanapokuja kusaga mawe na pia unaweza kuwa unanunua dhahabu hapo na kwnda kuuza. Cha msingi ulifunge sehem nzuri yenye uzalishaji.