Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Milioni 300 ukiamua kuitunza na kutumia kila mwezi 2M maana yake utakula maisha bila stress kwa miaka 20 ijayo. Sijui umri wako ila kama umri pia umeenda, kwa next 20 years maana yake utakuwa umekaribia kumaliza siku zako za kuishi. Kuja pesa ikakata, na wewe siku zako zinakuwa zinaelekea kukata. Yaani hapo ni kula 2M kwa mwezi bila stress za hii dunia. Maisha ya hapa Duniani ni kuchagua tu, maana utajiri hauingii nao kaburini. Kwanini kujipa stress ufe mapema?
Umeamua kuipa likizo akili
 
God bless thee!
Amen amen bro!!

Kuna selfish man mmoja kule kanda ya ziwa anafanya izi mambo na he wont share even an ounce of knowledge but look hapa nimepata madini si haba.
Selfishness is a form of immaturity, we you get to grow, one thing you understand is that maturity is all about helping others. Naamini kila mtu (including me) at a certain point in life alisaidiwa na mwingine, sasa kama watu wote wangebaki selfish na kile walichonacho duh sijui tungekuwa wapi wengine.[/QUOTE]

How long have you been in the field mkuu... Labda nikupe guiding vocabularies ili uflow vzuri zaidi in relation to the field...
It's about 3 years now.

from scratch adi kuwa level za ukonki ulipo.1. kota 2. Kuozesha kifusi 3. Etc etc yaani kiujumla all the things in that biz from a just a one hand hustler(small mpambanaji (limited by capital ofcourse)) to multilever fighter ( mtu iko na 300M) up can you try to give me a picture of that jungle
Ntajitahidi kueleza kwa kifupi lkn kwa ufasaha pia;

1. Kota (broker):
Watu wanaanza hata na 1m or even less. How?
Kwa Chunya, maeneo yanayo chimbwa yapo mengi sana na unlike other areas (Kahama,Geita na Nyamongo) mwamba wa Chunya uko very shallow (juu juu) na pia sehemu kubwa ni mwamba laini kiasi kwamba vijana wengi wanaanza na sururu tu kuchimba na kukusanya mawe na hatimaye kuyapeleka kusaga kwny crusher (karasha) na kukamatisha dhahabu.

Sasa kwa vijana km hawa, wewe kota unazama porini kuwafata wanapo chimba na kuongea nao unawawezesha kidogo fedha mfano ya vifaa (sururu nk) au sometimes hela ya chakula kwa makubaliano wakipata mzigo watakuuzia wewe kwa bei flani (ambayo ni ya chini kuliko ya kule soko la broker utapoenda kuuza wewe).

Na huwa ni fedha ndogo tu ya kuwadhamini inaweza isifike ht 100k. Kwa hyo ukipata makundi ya vijana ht matano hv ukawawezesha then ukawa unawabana unapata mzigo (grams kadhaa) na kwenda kuuza soko la broker, inakupa gape zuri la kuanza km kota then baadae ukikua unaweza kujisajili nawe km broker ukawa na ofisi ambapo unaweza kujidhamini kwa ofisi yako ukapewa fedha na dealers (wanunuzi wakubwa) kwa makubaliano ya uwe unawauzia mzigo wako. Hapa ni muhimu uwe na pikipiki kufanya hizi mishe zote.

2. Kuozesha kifusi/rudio/concetrates:
Hapa kuna namna mbili;
a) Uwe unanua kifusi/rudio kwny mialo ya kuoshea dhahabu kwa wale wenye makarasha au
b)Utafute sehemu wanapochimba ufunge karasha ww mwnyw ili ukusanye kifusi/rudio then baadae utaingiza plant kufanya processing kisha elution kuchenjua. Gharama za karasha inacheza kwa ss kati ya 8-9m lkn ukiwa kule field kuna makarasha yamewashinda watu kuyaendesha unaweza pata kwa 3-4.5m na linakuwa kwny hali nzuri sn kufanyia kazi.

Ukianza na ukota utapata connection nying tu sabab unakuwa uko kwny actual field. Utajua wapi kuna mwamba mzuri pa kuchimba/kufunga karasha, utapata kirahisi kujua hayo makarasha yaliowashinda watu nk nk.

Ukiweza kufikia hatua ya kuwa na karasha lako uko kwny hatua nzur sn 'kutoboa'. Kutegemea na sehem ulipolifunga unaweza tumia miezi 4-6 kukuza kifusi cha tani hadi 300. Kwa mfano km rudio lako litasoma 3.5ppm maana yake kwa kila tani 1 unaweza pata hadi gram 3.5 ya gold, kwa tani hzo 300 maana yake (3.5*300tons) = 1050grams = 1.05 kg ya gold ambayo kutegemea na %purity utaweza pata 100m+ km itakuwa 95%+ kwa bei ya ss.
Ofcourse, utatoa gharama za plant, kusomba kifusi hadi plant, madawa na elution. Inaweza fika hafi 30m, so roughly utabaki na 70m flan hiv of which is a handsome amount. Ukifika hatua hii ss ni ww tu kujitanua maana unakuwa na capital ss ya kufanya kazi.

Njia ya kufunga karasha ukifanikiwa ni nyepesi zaidi kwa kuwa linajiendesha lenyewe, hapo wanalipa kila wanapokuja kusaga mawe na pia unaweza kuwa unanunua dhahabu hapo na kwnda kuuza. Cha msingi ulifunge sehem nzuri yenye uzalishaji.
 
Kuna muda unaweza kuwa kichaa kwenye haya mambo ya biashara.

Nimewekeza Tsh. Million mia tatu(300m+), nimeanza biashara napata return ya 5m yaani million tano kwa mwezi.

Hapo sijatoa mishahara ya wafanyakazi na gharama za kuendeshea ofisi.

Wafanyabiashara mna roho ngumu sana, presha nje nje!
Nahisi uliweka sehemu kubwa ya hela ulio nayo. Biashara inatakiwa kukua kidogo kidogo. Hupaswi kuweka mtaji wote kwenye biashara ambayo bado hujui cash flow yake.
Weka hata theluthi ya mtaji, uisome ujue cash flow yake.
 
Mkuu kwenye sector ya logistics hii pesa unaizungusha ndan ya muda mchache, ukitaka kama transporter (scania used imesimama unapata hata kwa USD 35,000) au kuchukua tender na wewe ugawe kwa sub contractors...logistics haijawahi kuangusha mtu makini! Watu wanatoka kwa mikopo.. wewe advantage mtaji unao! Kila la heri.
Fafanua jamani


Madini haya
 
Mmiliki wa ma-bus ya Princess Muro yeye alikamatwa kwa kujiunganishia bomba la mafuta Kule bandarini(TPA),Mmiliki mwingine wa ma-bus ya Arusha-Dar alikamatwa akiiba tairi za mabus kwny stoo ya watu huko na kumbuka huyo mtuana mabus zaidi ya 20 na kila siku yanaingiza pesa.

Sumri alisema sababu mojawapo ya sababu ya biashara ya mabus kumshinda ni wkt wewe unanunua Mafuta kwa Bei ya soko kumbe wenzako wanajua wanayoyapatia.

Au wewe unaenda kununua tairi za mabus yako kumbe wenzako wanaiba tu stoo.

So point ya msingi Ni biashara yoyoye ile Ni tamu kuisikia tu,Ila siri ya urembo Ni ukiingia Field ndipo utajua.

Sumry ni uongo huo

Ali acha watoto wakawa wanaendesha kampuni
Pesa za marejesho hazionekani
 
Kuna muda unaweza kuwa kichaa kwenye haya mambo ya biashara.

Nimewekeza Tsh. Million mia tatu(300m+), nimeanza biashara napata return ya 5m yaani million tano kwa mwezi.

Hapo sijatoa mishahara ya wafanyakazi na gharama za kuendeshea ofisi.

Wafanyabiashara mna roho ngumu sana, presha nje nje!
Faida kubwa za haraka (chap chap). Hii ndio ipo akilini mwa watu wengi wanaofanya biashara au kutaka kuingia kwenye biashara.

KASORO ZILIZOPO.

1. Inaonyesha kabla ya kuwekeza hicho kiwango cha fedha haukufanya FINANCIAL PROJECTIONS sababu hauwezi iita TSH 5,000,000 faida wakati bado haujatoa gharama za uendeshaji.

2. Kama umewekeza zaidi ya Tsh. 300 MILLION na bado unaona ni shida juu ya hiyo biashara. Ni wazi kuwa BADO HUJAIJUA HIYO BIASHARA AU UMEDHARAU MISINGI YA HIYO BIASHARA.

UTATUZI

1. Rudi ubaoni (drawing board) na uichanganue upya hiyo biashara/uwekezaji uliofanya. Kupitia;
(a)Gharama za uendeshaji
(b)Kodi
(c) Bidhaa; je bei ipo sawa (inaweza ku-cover gharama za uendeshaji?)
(d) Kama umewekeza kwenye uzalishaji, jipe muda kabla ya kuaza kuona faida nono unazotamani kuzipata

KAZA MSULI, JIFUNGE KIBWEBWE
 
Tuweke mambo sawa, maana naona wajuaji wamekuwa wengi kidogo.
Huu mtaji niliowekeza sio kwamba nimefeli japo mambo yamekuwa kinyume na matarajio yangu.

Lengo langu lilikuwa kuwekeza mtaji zaidi ya huu, huu ndio mwezi wa wangu wa kwanza kwenye biashara naendelea kuona mavuno ya mtaji nilioweka Ili niamue kuongeza mtaji au la.

Nimeshindwa kufunguka zaidi baada ya kuona kuna ujuaji mwingi Tena Kwa watu ambao hata biashara hawaijui. Kila nyuzi wao wanajua ni uongo wa kutunga au chai, wao wakiona nyuzi ya 300m+ wanajua ni story za kusadikika

Anyway tuwe na usiku mwema, na niwaombee muwe na mapambano yenye baraka
Mkuu humu si sehemu salama ya kuomba ushauri kuna baadhi wapo real kweli na wanaongea na kushauri kutoka moyoni but kuna watu wa kuvunja moyo.. hivyo sidhani kama itakua vyema ww kureveal biashara unayofanya..

Kuna wengine wapo kwa ajili ya kukosoa tuu kuona uongo kila kitu mtu anachoandika utadhani wanamfahamu sanaa. So nakushauri pitia comments za watu waliochangia uzi wako kuna watu wana ushauri mzuri sana angalia hao nenda DM zao mpeane Abc's za bness huku achia watu watoe nyongo zao maana wengine maisha yana wastress hivyo kukosoa kunawapa amani ya moyo.
 
Kuna muda unaweza kuwa kichaa kwenye haya mambo ya biashara.

Nimewekeza Tsh. Million mia tatu(300m+), nimeanza biashara napata return ya 5m yaani million tano kwa mwezi.

Hapo sijatoa mishahara ya wafanyakazi na gharama za kuendeshea ofisi.

Wafanyabiashara mna roho ngumu sana, presha nje nje!
Siku zote mwanzo huwa mgumu.
Things will go smoothly day by day.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Kweli kabisa mkuu.
Nilifahamu huu uwekezaji kwa kuchelewa lakini ni afadhali kuliko nisingejua kabisa.

Mambo ya kujenga nyumba ya kupangisha unaanza kusumbuana na wapangaji kuhusu kodi ya pango, mara kodi ya zuio, property tax unaachana nayo...!
Kuna mtu aliuza ukumbi mbezi beach pamoja na plot ya barabarani akajumua na duka kariakoo akafunga biashara, alitengeneza kama 2.5B hivi yote akaipeleka BOT, ana watoto 7 hela anayogawana nao, yeye na kila mtoto anapata 4M kwa mwezi bila kutoka jasho kwa namna yeyote 😂😂😂! Anachofanyana sahizi ni jogging, gym na kula vizuri tu akicheza na wajukuu😂!

Mie nikipata 1B tu ujue im never going broke again! Yote ni BOT na sitaki shida tena na mtu nakula gawio langu tu
 
Back
Top Bottom