Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Tena si machinga pekee bali hata wapita njia na wanunuzi, maana hali ilivyo ni msongamano wa watu barabarani kutokana na kukosa njia ya kupita maana njia zote za watembea kwa miguu zimezibwa na machinga na kulazimika watu kupita barabara kuu kama magari ivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kugonjwa na gari, bajaji, bodaboda na wao wenyewe kugongana kwa kuwa wanapita kwa kulazimisha huku wakikwepa magari.
Wafanyabiashara wa hapa wamejimilikisha eneo la barabara na la watembea kwa miguu huku wakiwa hawana wasiwasi wa kuwa wanahatarisha maisha yao kwa kukaa barabara, wengine wameweka ndoo na kuzikalia huku wakiipa mgongo barabara hali ya kuwa wapo pembezoni mwa barabara na magari na vyombo vingine vya usafiri vikipita na wala hawajali wao huendelea kuuza bidhaa zao ambazo wameziweka kwenye kinjia kilichokuwa kimeachwa kwa ajili ya watembea kwa miguu.
Sijui mamlaka ziko usingizini au eneo hili hakuna viongozi wanaoweza kuona hatari kabla haijatokea na wakachukua hatua ya kudhibiti kabla ya majanga husika. Narudia tena siku ikitokea gari ikachochora hapo ni balaa tutabaki kulaumu wakati tungeweza kuzuia hali hiyo.
Hao machinga kama wameshindikana kuondolewa kama ambavyo mwanzo walikuwa wakitolewa basi wawekewe namna nzuri ya kukaa, wasikae barabarani, wasizuie njia za watembea kwa miguu ili kuepuka hatari ambayo inaweza kuepukika.
Machinga kwenye eneo hilo licha ya kuwa sababu au chanzo kero lakini wanahatarisha sana usalama wao na wateja wao ambao muda mwingi usimama kwenye eneo la barabara ili kuhudumiwa.
Lakini nimekuwa nikibakia kujiuliza hivi Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeshindwa kubaini changamoto hiyo na kuipatia suluhu kwa kuwaondoa wamachinga walioko kwenye maeneo hatarishi na yanayochangia kero au tunasubiri mpaka majanga makubwa yatokee ndio tuanze kuwajibika.
Viongozi wenye maono wanatakiwa kutatua changamoto kabla madhara makubwa hayajatokea tusijifungie, katika hili Viongozi wenye mamlaka ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo au ngazi ya Mkoa ni vyema mkaliona hili kwa uharaka mimi nimewadokeza, naamini wengi waliopitia njia hiyo mtaungana na mimi.